MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Rais Magufuli ana vita pevu kuhusu mstakabali wa sukari na hatima ya viwanda vya sukari nchini.
Sukari yote nchini inayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaagizwa na hawa matajiri wakubwa nchini kama wanavyoonekana kwenye picha.
Hawa ni baadhi ya matajiri ambao wanamiliki soko la sukari nchini ambalo wakati wa utawala wa Rais Kikwete, hakuweza kuwadhibiti ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini na afya za walaji.
Hawa kwenye picha hapo chini ni aina ya watu wanaoitwa sugar industries movers and shakers katika jumuiya ya wafanyabiashara nchini.
Kutoka kushoto ni Harun Daudi Zakaria ambaye juzi vikosi vya usalama nchini vilikuta kwenye magodauni yake huko Mbagala na Tabata tani zaidi ya 4,600 ambazo inasemakana zilikuwa zimefichwa, kwa lugha ya kisheria wanasema hoarding commodities. Huyu wakati mwingine alikuwa anapewa vibali ambavyo waingereza wanasema special/exclusive permit kununua au kuagiza sukari kwa ajili ya soko la Zanzibar.
Anayefuatia ni Said Salim Bakhresa ambaye hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani za sukari kama malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda vyake.
Anayefuatia ni Reginald Mengi ambaye ana viwanda vya vinywaji. Hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake mbali mbali.
Anayefuata ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye baada ya kushindwa vita ya sukari kutokana na nguvu kubwa waliyonayo hawa wafanyabiashara, akaamua kuacha mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake. Huu ulikuwa ni mwanzo kwa serikali kushindwa kufahamu kiwango cha sukari kilichoko ndani ya nchi, kiwango kinachoingia na pia kiwango kinachohitajika katika matumizi kwa mwaka.
Anayefuata ni Gulam Dewji ambaye ni Baba yake na Mohammed Dewji (Mo Dewji). Huyu ni Mwenyekiti wa MeTL Group na Mnunuzi na mwagizaji mkuu wa sukari kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake na pia kuuza kwenye soko laTanzania Bara. Huyu pia alikuwa anapewa special/exclusive permit ya kuagiza sukari. Kwa sasa serikali inafanya uchunguzi kutokana na utata wa maelezo ya sukari tani zaidi ya 1000 zilizokutwa kwenye ICD ambayo alidai haina mzigo wake.
Akiwa Kiwalani jana, Makonda ametoa saa 24 kwa kiwanda cha MeTL cha eneo hilo kupeleka nyaraka katika mamlaka husika kuthibitisha kama sukari 5,800 iliyokutwa katika kiwanda hicho inafaa kwa matumizi ya binadamu.
Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ghala hilo, Makonda alisema ameamua kuzuia sukari hiyo baada ya kukuta inafungashwa kwa matumizi ya kawaida ilihali ililetwa kwa ajili ya matumizi ya viwanda.
Aliitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kuchunguza sukari hiyo kama ni bora kwa matumizi na kuangalia kama kibali cha mamlaka hiyo cha kubadili sukari hiyo kuwa ya matumizi ya kawaida walichokionesha kama ni cha kweli.
Wa mwisho ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo ambaye ni mmoja wa inner circle ya Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons). Kwenye inner circle ya Sir Andy Chande huwezi kumkosa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Balozi Juma Mwapachu.
Kwa ku-refresh your mind, Unaweza kupitia hii Habari,
Wakati Watanzania wakiumizwa na bei ghali ya sukari, imebainika kuwa karibu tani 180,000 za bidhaa hiyo ‘zinaozea’ maghalani katika Jiji la Dar es Salaam na sasa wafanyabiashara wanasaka kibali cha kuiuza nje ya nchi.
Kiasi hicho cha sukari ni tofauti na zaidi ya tani 90,000 zilizozalishwa nchini zinazoendelea kuhifadhiwa kwenye ghala la Kilombero Sugar Co. Ltd, Dar es Salaam.
Kitendo hicho kimemkera Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza, na kumfanya ahoji sababu za kiasi hicho cha sukari kuendelea kuhifadhiwa maghalani badala ya kusambazwa iuzwe kwa bei nafuu.
Waziri huyo alieleza kushangazwa na ‘picha’ ya tani 180,000 za sukari iliyoagizwa kutoka India kushindwa kutoa unafuu wa bei kwa wananchi. Waziri alishuhudia sukari nyingi ikiwa imehifadhiwa katika maghala tofauti ya wafanyabiashara wakubwa jijini hapa, wakati alipofanya ziara ya kushitukiza, wiki iliyopita.