Hawa Mameya ni kiboko kwa CCM, Chadema waleeni vizuri viongozi hawa

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Hawa mameya ni kutoka CHADEMA, Mh Calist Lazaro wa jiji la Arusha na Mh Boniphace Jacob wa Manispaa ya Ubungo jijini DSM. Ni mameya wanaotia fora sana kwa siasa zao na hasa wawapo majukwaani.

Nimejaribu kufuatilia misimamo na na hoja za hawa makamanda viongozi kwa kweli CHADEMA wana hazina ya viongozi makini kabisa ambao haya Uenyekiti au ukatibu wa chama TAIFA kwako ni kazi ndogo sana.

Hawa mameya ni makaa ya moto kwa CCM, wanaogopeka vibaya mno na CCM na wana uwezo makubwa sana wa kucheza na siasa za bongo.

Hawa ni viongozi wanaopaswa kulelewa na chama kwa gharama yeyote ili, sio watu wa mchezo mchezo hawa. Hata ukiwapa nchi wanaendesha bila wasiwasi hawa.
 
images-1.jpg
02.jpg
 
Hamchelewi kuwapoteza kama mlivyompoteza Ben Watch Nane,,hcho chama hakiwez kua na mwenye sauti au mvuto kama wewe sio wa upande uleeee wa watakatifuuu
 
Mkuu kweli kabisa.

Meya Boniface Jackob ndio kiboko ya Jambazi la vyeti Daudi Albert Bashite.

Kinachowapa nguvu hawa mameya ni hawana chembe ya uoga dhidi ya viongozi wa serikali hasa wakuu wa mikoa husika ambao wanajiona miungu watu.

Big Up sana Meya Boniface Jackob na Meya Calist Lazaro.. Ninyi ni hazina kubwa kwa CDM.
Hakuna kurudi nyuma.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hamchelewi kuwapoteza kama mlivyompoteza Ben Watch Nane,,hcho chama hakiwez kua na mwenye sauti au mvuto kama wewe sio wa upande uleeee wa watakatifuuu
Ebu wacha akili za kinyama wewe yaani ujue huyo unaye mdhihaki ana ndugu zake wana machungu na majonzi alafu wewe unaleta umalaya wako?
 
Mameya wa Chadema ni wasomi siyo kisomo cha ngumbaro kama wale wa mtaa wa Lumumba. Utafiti unasema CCM inapendwa na wenye walakini kwenye ubongo (Akili duni). Si uliona uchaguzi wa wabunge wa EALA? Masha utafikiri mtoto wa malkia wa uingereza. Wenje ndo usiseme. Lakini CCM wakaamua kuwapeleka warembo.
 
Calisti Lazaro ni safi

Shule zote madarasa safi

Madawati mengi

Mabarabara mitaani Arusha

Ila Diwani NGowi wa Kimandolu Kijenge anawaangusha

Barabara ya Kijenge Kimandolu ni Mawe na Mashimo
 
Hahahaha wakati nipo teenager mtaa wangu wa Sokon I ulikuwa kitovu cha siasa Arusha.

Ndiyo ilikuwa kata pekee iliyokuwa inakaliwa na upinzani TLP na nyingine zote zilikuwa CCM kabla ya vugu vugu la mageuzi kuanza 2010.

Sasa huyo Kalist Lazaro al maarufu 'Bush' alikuwaga ni CCM ambapo alihamia baada ya kutemwa TLP. Nakumbuka aliwahi kugombea uenyekiti wa mtaa lakini alikosa maana alikuwa CCM na kata yetu sokon 1 ilikuwa inasifika kwa upinzani Arusha.

Nampongeza sana Bush ametoka mbali, toka kushindwa uenyekiti wa kijiji, baadae akashindwa udiwani 2010 na Kivuyo ila sasa amekuwa Meya mashuhuri wa kupigiwa mfano.

Mungu ni mwema... Piga kazi Kalist Lazaro "Bush"
 
Hakika sitasahau siasa za kata ya Sokon I na Sombetini... Drama zote za siasa zinazotokea sasa kwa level ya Taifa.. Mimi nilikuwa nazishuhudia live nikiwa mdogo kabisa kama miaka 14 hiv...

Hakika ndo mana upinzani umenijaa damuni.

Kwa ujumla tuliokulia arusha kati ya miaka ta 2004-2010 tumepata taste halisi ya nini maana ya politics..

Enzi hiyo ndo bwana mdogo Lema ambaye alikuwa mgombea asiyepewa nafasi wa TLP kinda kabisa, aliangusha kisiki Filex Mrema.. 28 years old by the time.. Na alikuwa anatema cheche vibaya mno..

Daah..
 
Eeeeeka Saaah
 
Hawa mameya ni kutoka CHADEMA, Mh Calist Lazaro wa jiji la Arusha na Mh Boniphace Jacob wa Manispaa ya Ubungo jijini DSM. Ni mameya wanaotia fora sana kwa siasa zao na hasa wawapo majukwaani.

Nimejaribu kufuatilia misimamo na na hoja za hawa makamanda viongozi kwa kweli CHADEMA wana hazina ya viongozi makini kabisa ambao haya Uenyekiti au ukatibu wa chama TAIFA kwako ni kazi ndogo sana.

Hawa mameya ni makaa ya moto kwa CCM, wanaogopeka vibaya mno na CCM na wana uwezo makubwa sana wa kucheza na siasa za bongo.

Hawa ni viongozi wanaopaswa kulelewa na chama kwa gharama yeyote ili, sio watu wa mchezo mchezo hawa. Hata ukiwapa nchi wanaendesha bila wasiwasi hawa.

Yes ni Viongozi wazuri ila kusema kuwa wanaitetemesha CCM nadhani utakuwa umezidisha tu chumvi Mkuu. Kuifananisha CCM na CHADEMA ni sawa sawa na kumfananisha Lionel Messi FC Barcelona ( Spain ) na Simon Msuva wa Yanga FC ( Tanzania ). Uzoefu mkubwa wa CCM hauwezi kulinganishwa na Chama chochote hapa Tanzania labda tu vyenzie ANC cha Afrika ya Kusini, SWAPO cha Namibia na Zanu-PF cha Zimbabwe bila kukisahau kile cha China.
 
Hamchelewi kuwapoteza kama mlivyompoteza Ben Watch Nane,,hcho chama hakiwez kua na mwenye sauti au mvuto kama wewe sio wa upande uleeee wa watakatifuuu
......subiri Gwajima amefunga kwa ajili yake,,,,,yamukini Mungu atampa majibu alipo Ben.
......
 
Back
Top Bottom