HAUJAISOMA NAMBA!!? BASI UTAKUWA UMESOMA TARAKIMU!

Apr 23, 2012
76
71
Tujikumbushe wimbo wetu maarufu sana...,

Tuliipenda wenyewe, ndi ndi..
Chaguo letu wenyewe, ndi ndi..
Wacha waisome namba weeee...
Wajinga waleeee..., CCM mbele kwa mbele..
(unasikia vigelegele na vifijo)

.., Sasa nikuulize wewe ndugu yangu uliyekuwa ukiimba wimbo huu mwezi oktoba, 2015.., namba unaisoma au bado haujaanza kuisoma!!?

> ukosefu wa dawa na vifaa tiba hospitali.
> kupanda kwa gharama za maisha.
> Mfumuko wa bei na bidhaa kwa kaya.
> kutopandishwa daraja la utumishi.
> Mshahara kutokupata Nyongeza mwezi Julai.
> wahitimu kada ya ualimu/Udaktari kutoajiriwa.
> wanafunzi wa vyuo vikuu kucheleweshewa mikopo.

Kama haujaisoma namba hadi sasa, basi utakuwa umesoma MAGAZIJUTO hadi sasa (yaani namba zote katika ukokotozi)!

Martin Maranja Masese
Mwananchi wa kawaida
 
Back
Top Bottom