Hatuwezi kuwasifia CCM wakati ninyi hamjawahi kutusifu

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Hivi mnajua nini! Niujinga tena ujinga mkuu kusema upinzani kuwa upinzani kila siku kupinga tu na kusema hapana, wakati hao CCM hawajawahi kuisifia UKAWA hata siku moja.

Ni ujinga kumshutumu mtu eti hujawahi kupost vitu vizuri vinavyofanywa na CCM, wakati wewe pia hujawahi kuchukua simu yako ukapost mambo mazuri yaliyofanywa na UKAWA.

Ni ujinga kuhoji mshahara wa mwenyekiti CHADEMA bila kutaja mshahara wa mwenyekiti wa CCM.

Ni ujinga pia kufikiri wadhifa wa mwenyekiti una mshahara.

Ni ujinga kuifananisha CHADEMA na CCM.

Ni ujinga kumshutumu Seif kwa makosa ya Jecha na CCM yake.

Ni ujinga kujifanya huna akili wakati una akili timamu ya darasani na ulimwengu.

Ni ujinga mtu mwenye chama kidogo na dhaifu kukionea wivu chama kikuu cha upinzani kwa mafanikio yake.

Tuondoe ujinga vichwani mwetu ili taifa lisonge mbele sauti itasikika kwa waafidhina wote humu ndani na njejicho hili linaona husuda hadi ndani ya mioyo yenu kwa CHADEMA.
 
Ukweli mchungu, bongo wanasiasa hawajakomaa kabisa na wanaona kuiga jambo zuri ni kitu kibaya
 
Mtoa uzi siasa umeanza kufuatilia lini?

Basi nikukumbushe hata hii ya juzi wakati wa hotuba ya rais kwenye uzinduzi wa bunge alimsifia Zitto kabwe mwanzo na mwisho mwa hotuba yake

Au kwko upinzani ni Ukawa tu?
 
Mtoa uzi siasa umeanza kufuatilia lini?

Basi nikukumbushe hata hii ya juzi wakati wa hotuba ya rais kwenye uzinduzi wa bunge alimsifia Zitto kabwe mwanzo na mwisho mwa hotuba yake

Au kwko upinzani ni Ukawa tu?

Alimsifia ZZK kwa kufanya kinyume cha wapinzani wake wa dhati. Zitto alibaki ukumbini wakati UKAWA walitoka nje ya bunge
 
Back
Top Bottom