Hatutaki Dom iwe kama Dar


well said mkuu
 
Dar ilitakiwa iwe somo kwa wenye mamlaka lakini utaona bado hakuna tulipojifunza na kuendelea kurudia makosa yaleyale..

90% ya wakazi wa dar tunaishi kwenye vibanda umiza, kifupi Dar hata uwe na nyumba nzuri vipi bado unaishi kwenye skwata area tu, huna pakutupa taka, huna barabara nzuri za kupita, kiwanja unachoishi ni 20mx20m, Ona Sinza, Msasani, Mikocheni, Kijitonyama kulivyobanana na watu wanavyosifia na kurank hayo maeneo lakini uhalisia maeneo hayo ni hatari kwa Afya kwasababu ya mbanano uliofunga mpaka njia za maji na mzunguko wa hewa..hapo bado eneo kubwa la Manzese, Tandale, Magomeni, Ubungo, Buguruni, Tandika, Vingunguti, Kiwalani, Mtoni, Tandika, Mbagala, Kariakoo, Kigogo nk.. Hivyo utaona sehemu kubwa ya jiji lilivyo chafu na ukiwa angani ndio utaelewa haya.. Makosa yaleyale yanarudiwa kwenye maeneo mapya kama, Mbezi, Goba, Bunju, Kijichi, Chamazi, Kibaha, kibamba, Kiluvya, Tegeta, Bunju, Boko nk..

Watanzania tujifunze sasa, kujenga kuachiwe makampuni yajenge apartments zilizopangiliwa kwa ramani za miji, watu wauziwe apartments kwa bei rafiki iwe cash au mikopo, Serikali isimamie hili kwa kutoa unafuu mkubwa wa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na viwanda vyote vinavyozarisha humu ndani vipewe punguzo kubwa ili bei ya bidhaa za ujenzi iwe nafuu na watanzania wakae kwenye nyumba bora, Biashara ya kupangisha nyumba waachiwe estates agency na si kila mtu ili pia nyumba hizo ziwe bora na nafuu..
 
 
Tuambie hapo ulipo ni eneo gani unaweza fanannisha na Mbagala?.au Tandale?.Dar kila kitu ndugu.Jiji la kukufikirisha jinsi ya kupata pesa,huku mikoani majitu ni mepesi kuridhika,vichwa butu.Ukikuta kachangamka jua huyo katoka Dar au Arusha,
Ndio maana viongozi wote nikutoka mikoani "vichwa butu" hata mkuu wenu hapo wa mikoani. Lini Dar au Tz iliongozwa na wajanja wa Dar au Arusha kama kauli yako?
 
Uko sahihi kabisa huku mji wa govt Mtumba hadi Chamwino Ikulu wangeanza project ya new Dodoma as New Cairo (samahani kwa mifano mingi ya Misri ndio nchi naijua sana tofauti na Tz? ) halafu kule kubaki old Dodoma ila wameshaanza mambo ya Dar kuvunja majengo ya zamani (Mliokuwa mnaijua Paradise Cinema) sasa ishavunjwa sijui wataenda kuvunja na NK?
 

Sidhani kamma maghorofa makubwa ni muafaka kwa Dodoma kutokana na suala la matetemeko ya ardhi kwa mji huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…