Baba Kiki nataka nikuambie kwanza hutakiwi kuamini sana hizi habari za haya magazeti ya kibongo ya kwamba sijui Ngassa afichwa Hotelini au vp,kabla ya kumhukumu Ngassa kuwa hakuandamana na team yake baada ya mchezo wa fainali ungefanya uchunguzi kwanza wachezaji wengine wa Azam baada ya mechi ile walikwenda wapi,je walirudi Kambini au walipewa ruhusa na kama walirudi Kambini Ngassa hakurudi Viongozi wa Azam walichukua hatua gani,manake taratibu za Kambi yeyote zinajulikana kama Ngassa alitoweka Kambini bila ruhusa walikuwa na haki ya kumchukulia hatua ksbb bado kisheria ni mchezaji wao regardless vitendo alivyovifanya vya kuonyesha mapenzi kwa team nyingine,wangeweza hata kumwadhibu kwa kumfungia.
Kuibusu logo ya Yanga mimi sioni kama inaweza ikawa issue saana ya kuanzisha haya yote,wapo wachezaji wa Ulaya baada ya kuhama wameshawahi kuonyesha mapenzi yao kwa team zao za zamani walizozichezea kwa mafanikio akiwemo Thiery Henry sasa kwanini kwa Ngassa iwe tatizo la kugharimu kipaji cha mtu, Ngassa kuipenda Yanga hajaanza leo,inawezekana tokea utotoni labda kabla hata hajaanza kucheza soka la ushindani,Azam walimchukua Ngassa kutoka Yanga wakifahamu ana mapenzi na Yanga,lkn still bado aliwafanyia kazi ksbb Ngassa kama mtu mzima anajua kuwa mpira ndo kazi yake na hivyo despite mapenzi yake kwa sehemu fulani lkn anapaswa kuutumikia mkataba wake ipasavyo kitu ambacho amekuwa akikifanya kwa kipindi chote alichokuwa Azam,sasa point hapa ni kuwa kama wao wanafikiria kuna vitu alivyokosea ilikuwa ni kumuonya,kumuwekea utaratibu mpya wa kazi au hata kumwadhibu jambo ambalo nina uhakika lingemfunza zaidi kuliko mbinu wanayotaka kutumia kumkomoa.
Point ya Simba kupanda dau zaidi ya Yanga,mimi nakuomba usiichukulie juujuu,unajua Yanga ndo walikuwa wa kwanza kubisha hodi Azam wakitaka kumchukua kwa mkopo,Azam wakakataa...Yanga wakataka waambiwe bei,still bado Azam wakagoma,wakasema hauzwi basi Yanga wakatulia,baada ya kuona mchezaji mwenyewe hawataki Azam wakatangaza bei US $ 50,000,ile hela Yanga wakaona kubwa,Azam wakawauliza Yanga wako tayari kutoa shing'api Yanga wakasema Mil 20,hapohapo Azam wakawasiliana na Simba wakawaambia offer ya Yanga,na wakawaambia wapande bei zaidi - yote ni katika kumkomoa Ngassa,Simba wakapanda Mil 25,Yanga wangefika 30,Simba wangepanda Mil 35...sasa biashara gani hiyo?
Kihalisia kabisa hapa hakuna biashara iliyofanyika hapa ni ujanjaujanja wa kutaka kumkomoa mchezaji basi, hlf sasa walivyo wajinga wanajichanganya mara ni mkopo,mkopo gani wa ada ya uhamisho? na mshahara anapokelea team yake mpya,gazeti moja limemnukuu kuwa atakipiga kwa mkopo Simba miaka miwili,wakati mkataba wake kwa Azam ulibakisha mwaka mmoja...mkopo gani una'exceed duration ya mkataba,hivyo ndo wanavyokopesha Unga na Cola zao?