Hatumshangai Rais Magufuli, eti tunaishangaa CHADEMA?!!

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Wakati mwengine sisi watanzania sijui niseme tumepatwa na nini , mambo yetu tunayofanya na hasa siasa zetu zinachekesha na kukarihisha. Siasa zimetufanya vipofu (kumradhi) na tunafika mahala hatuoni mwelekeo wetu kama jamii yenye wasomi na weledi wa fani mbali mbali.

Leo hii na jana baada ya Katibu wa bunge letu kueleza kuwa eti CUF na Chadema hawakukamilisha utaratibu wa mchakato wa wawania ubunge wa vyama vyao huko EALA sababu ziko nyingi lakini zikiwemo za kukosa vigezo vya jinsia. Kweli hii ndio hoja ya msingi? na kwa haraka kuna makada ya vyama fulani wanakimbilia kuilaani chadema. Taarifa na ufafanuzi wenyewe wa 1/3 ya jinsia ya wanawake bado ina utata na haijitoshelezi.

Tuseme hilo iwe kweli ni kosa kwa chadema kama CCM na wafuasi wao wanavyotaka tuamini hivi nani tumshangae na kumlaumu?

Ningefikiri Tuanze kulilaumu Bunge kwa kushindwa kutoa ufafanuzi huo mapema lakini watu wanapeleka lawama chadema , CUF na wapinzani na vyombo vya habari vya mlengo vimeshupalia hilo.

Nije kwenye mada sasa, kwani kuna lipi jipya ikiwa hilo linalosemwa limetokea? ingekuwa vyema tumshangae rais magufuli kwa kutofuata sheria na taratibu zilizopo. Ni rais magufuli aliyezuiya mikutano ya vyama vya siasa kinyume na taratibu, ni rais Magufuli anayeshindwa kusimamia anachokisema(suala la vyeti feki na Bashite) ilihali kuna wengine waliokutwa na vyeti feki na kutumbuliwa, ni serikali ya rais magufuli inayopindisha haki ya dhamana kwa watuhumiwa (lema, uamsho), ni rais magufuli asiyezingatia usawa wa jinsia katika teuzi zake mbali mbali, Hivi haya hamuyaoni?

Tunajifanya kusahau ilihali tunaishi katika zama za giza na upendeleo wa wazi? Hili katika awamu hii ya tano ya rais Magufuli liko wazi mbona hatushangai? Tunaishangaa Chadema kwa hili la EALA ambalo jambo lenyewe lina utata wa tafsiri?

Zama za hadaa zimekwisha tuache mzaha ili tuendeleze siasa safi. Kuna cha kujifunza kutoka kwa Rais Magufuli na suala la kuzingatia jinsia kabla hatujaelekeza lawama kwa wengine.


Bastola ya nini?

Kishada.

cc. Vuta - nkuvute
 
Watalaam wa hesabu watupe ufafanuzi una 2 n'a unataka upate 1/3 ya hiyo mbili unafanyaje ??
 
Tanzania na siasa za hovyo hovyo.Mfano kushupalia kupata 1/3 kwenye watu wawili, Harafu kutokushangaa raisi kuchagua nafasi za utawala kikada bila kuzingatia utaalam na weledi kama ilivyotokea kwa wakurugenzi wa wilaya,manispaa na majiji
 
Tanzania na siasa za hovyo hovyo.Mfano kushupalia kupata 1/3 kwenye watu wawili, Harafu kutokushangaa raisi kuchagua nafasi za utawala kikada bila kuzingatia utaalam na weledi kama ilivyotokea kwa wakurugenzi wa wilaya,manispaa na majiji

Hayo ndio mambo ya kushangaza lakini tunakimbilia jiwe moja kuligawa ili tupate 1/3 ngumu
 
Back
Top Bottom