kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
MWANDISHI mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu, wiki iliyopita alitoa madai mawili ambayo imenipendeza na mimi nitoe mtazamo wangu kufuatia hoja zake. Alidai kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imeminya uhuru wa kujieleza na kuirudisha nchi nyuma miaka 50 na kwamba Rais mstaafu, Jakaya Kikwete anapaswa kushtakiwa mahakamani kwa kuisababishia hasara nchi kutokana na mabilioni ya shilingi yaliyotumika katika mchakato wa Katiba ambayo haikupatikana.
Ulimwengu ambaye mimi ninamheshimu sana ingawa lugha yake siku hiyo haikuwa na heshima niliyoitarajia kwa viongozi wetu, alitoa madai hayo wakati wa Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Nikianza na kuziba uhuru wa kutoa maoni, ninapata shida kujua wanaotoa madai hayo akiwemo Ulimwengu wanamaanisha kwamba kile kitendo tu cha kuzuia matangazo ya moja kwa moja bungeni kupitia televisheni ndiko kubana uhuru wa kutoa maoni au ni ile hatua ya wabunge wa upinzani kuamua kususa Bunge? Watu hawaongei na vyombo vya habari?
Mtu anaweza asikubaliane na hatua ya kusitisha matangazo ya Bunge ya moja kwa moja, hata mimi binafsi siungi mkono hatua hiyo, lakini huwezi kusema Tanzania imeminya uhuru wa kutoa maoni. Hii ni kwa sababu vyombo vya habari vina uhuru mkubwa na wananchi wana uhuru wa kuvitumia kadri wanavyotaka alimradi katika mipaka inayokubalika.
Na kuonesha kwamba uhuru huo haujaminywa ndio maana Ulimwengu akawa na ‘ubavu’ wa kusema alichokisema, kikanukuliwa na vyombo vya habari kote nchini. Mimi ninachoamini, katika nchi tunazoambiwa uhuru wa kutoa maoni unaminywa, Ulimwengu asingethubutu ‘kutukuna’ viongozi mbele ya kadamnasi na kama angelithubutu basi hivi ninavyoongea angelikuwa katika msukosuko mkubwa.
Tukija kwa wabunge wa upinzani waliosusa Bunge, inawezekana pia siku ile Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alipokataa hoja ya wanafunzi walioondolewa Udom isijadiliwe, hakuwa sahihi. Kama ndivyo, hata kama hakuna kanuni, kusimama na kupiga kelele kama ambavyo wapinzani walivyokuwa wamezoea kumfanyia Spika aliyestaafu Anne Makinda ndio uungwana?
Busara ya kawaida haikubali na kumbe kuna kunanuni ambazo zilikuwa zinawataka wafuate, yaani wakate rufaa kwenye Kamati ya Uongozi na Dk Tulia asingeruhusiwa kushiriki katika kujadili rufani dhidi yake, kamati ambayo hata wapinzani wamo! Na katika kuonesha kwamba uhuru wa kutoa maoni ni mkubwa nchini mwetu, kila siku wapinzani wako kwenye vyombo vya habari wakilalamika, wakisema hili na lile na hata kumtukana Naibu Spika.
Kwa mfano, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Jumatano ya Juni 15 asubuhi, alihojiwa na kituo cha ITV ambapo maneno yake hayakuwa na staha mpaka nikajiuliza kama Msigwa ni mchungaji kweli au la. Alidai kwamba eti anahisi Dk Tulia anaingia bungeni siku hizi akiwa amevaa pempasi ili kuwakomoa wapinzani baada ya kuamua kutoshiriki vikao anavyoviongoza kwa sababu akishakalia kiti haondoki.
Hiyo ni lugha inayofaa kweli kutumiwa na mbunge, halafu mbunge mwenyewe mchungaji? Mchakato kwa katiba na faida zake Tuje kwenye suala la Katiba mpya. Hakuna ubishi kwamba mchakato ule wa kusaka Katiba mpya ulitugharimu pesa nyingi. Lakini ni mtu asiyepima mambo kwa uzito wake anayeweza kumnyooshea Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kidole kwa sababu mchakato ule hata kama haukufika mwisho umeacha faida nyingi nyuma.
Kabla ya kuzitaja faida hizo, Jenerali angelikuwa muungwana, angelianza kwa hata kupongeza tu kwa hatua aliyoichukua Kikwete, hata kama haikufika mwisho. Hii ni kutokana na kuaminika kwamba alikuwa haungwi sana mkono na Chama chake Cha Mapinduzi kwa kuwa hilo halikuwemo kwenye ilani yao! Ikumbukwe pia kwamba madai ya kutaka Katiba Mpya yalianza mara tu baada nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi wakati huo Rais akiwa Ali Hassan Mwinyi na kama kumbukumbu zangu ni sahihi hata inayoitwa NCCRMageuzi haikuanza kama chama cha siasa bali chombo au kamati ya kudai mabadiliko, maana pana ikiwa ni Katiba Mpya.
Lakini katika kipindi cha Mwinyi hadi Benjamini Mkapa, madai ya Katiba Mpya yalikuwepo lakini neno hilo ‘Katiba Mpya’ libaki kama msamiati mgumu. Kikwete alipoingia madarakani katika kipindi chake cha pili akaamua kujitoa kimasomaso kama alivyojitoa Mwalimu Julius Nyerere kupigia upatu nchi kuruhusu demokrasia ya vyama vingi bila kujali ‘makunyanzi’ ya baadhi ya wahifidhina ndani ya CCM.
Kukwama kwa mchakato ule wa Katiba haumhusu mtu mmoja bali kunahitaji mjadala mkubwa wa kitaifa na kuangalia ni wapi tulipokosea na kubwa ambalo huwa ninaliona mimi ni kwamba tuliingia katika mchakato huo kabla ya kuwa na mwafaka wa kitaifa, basi. Tuliingia katika mchakato, huku kila mtu, kila chama kikiwa na mtazamo wake; kukiwa na watu waliokuwa kweli wanapigania maslahi ya taifa lakini wakiwemo wachoyo waliokuwa wakiangalia zaidi maslahi binafsi.
Ninaungana na Rais mstaafu Mkapa ambaye alipotakiwa na waandishi kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Jenerali, alisema ipo haja ya kujiuliza kwa nini Katiba hiyo ilikwama na kwamba hadi sasa hajasikia uchambuzi wa kina kuhusu jambo hilo. “Kuna haja ya kuwa na mjadala mkubwa lakini siyo kulaumiana tu. Siyo kudai tu. Kuwezesha uhuru wa kuzungumza ni jambo moja na kutumia uhuru huo ni kujadili, kuchambua na kupima na kufanya uamuzi sahihi kitu kingine kabisa,” alisema Mkapa.
Alisisitiza kuwa badala ya kumlaumu mtu mmoja mmoja, mjadala mpana wa kitaifa unahitajika ili kujua kilichosababisha Taifa kukosa Katiba Mpya. “Hakuna anayeandika ni wapi tulipokwama, tunalaumu na kumjadili mtu, wengine wanasema Katiba imekwamishwa na watu wachache kwa sababu za kimaslahi… Tunapaswa kuwa na mjadala wa kina kujua ni wapi tulipokwama,” alisema Mkapa.
Lakini pamoja na hayo, mchakato ule umetufundisha mengi na tulipoishia ambapo ni karibu na mwisho kabisa, siku tukianza upya hatutapata tabu sana. Pamoja na hayo, mchambuzi mmoja katika gazeti hili aliwahi kuonesha kwamba mambo mengi ambayo Serikali ya Rais John Magufuli inayatekeleza sasa bila kujali Katiba tunayoendelea nayo ya mwaka 1977 ni mwanga wa kile ambacho wananchi walijadili na kutaka kiwemo kwa Katiba iliyokuwa inapendekezwa.
Hata mimi ninakubaliana na mchambuzi huyo kwamba moja ya mambo ambayo wananchi walitaka katiba ijielekeze kwayo, ni kuhakikisha inahimiza uwajibikaji katika sekta ya umma na ulinzi thabiti wa rasilimali za nchi yetu, kitu ambacho kinafanywa na serikali yetu ya sasa na huenda kuna mchango kwenye mchakato huo wa Katiba.
Isitoshe, sisi siyo wa kwanza kuanzisha mchakato wa katiba na kushindwa kufika mwisho kwani kama kumbukumbu zangu ni sahihi, kabla ya Wakenya kupata katiba yao ya sasa, waliwahi pia kufanya jaribio la kusaka katiba mpya ambalo halikufanikiwa lakini likawa na mafunzo kwa mchakato wao wa pili.
Lakini nimalizie kwa kile ambacho nimekuwa nikikiona kama upungufu mkubwa kwa wanasiasa wetu na hata Jenerali aliuonesha katika hoja zake. Kitu hicho ni namna nzuri ya kuwasilisha hoja ya malalamiko kwa kiongozi na jambo hili, mimi kama Muislamu limefundishwa sana na Mtume wetu Muhammad (SAW).
Nasikia hata Jenerali ni Muislamu lakini sina hakika. Mafundisho hayo yanasema kwamba kiongozi wa umma hakaripiwi katika kumfikishia ujumbe, bali inatakiwa kuendewa kwa lugha yenye staha. Mfikisha ujumbe anaweza kuanza kwa kumsifia kwa yale mazuri aliyoyafanya kwa kuwa kiongozi yeyote hata awe dhalimu kiasi gani hakosi kuwa na mazuri yake.
Baada ya kutaja mazuri, ndipo mfikisha ujumbe sasa anaweza kusema “Lakini mheshimiwa ungeweza pia ukafanya hili na hili mambo yakawa mazuri zaidi.” Kimsingi, binadamu tulivyoumbwa hatupendi kukosolewa mbele ya tunaowaongoza, mbele ya watoto au mke/mume, iwe mimi, Jenerali au wewe unayesoma hapa sasa. Mtu unapofanya hivyo, hata kama uko sahihi unasababisha yule unayemkosoa asifikirie ushauri wako kwanza bali kule kumvunjia heshima.