Hatowahi kuwepo papa mweusi

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,481
Reaction score
1,450
Baadhi yenu mlifikiri hao makadinari wanaweza kupiga kura ya kumchagua Papa kutoka Africa? Kweli kabisa mliruhusu wendawazimu wa fikra uwaongoze kuwaza hivyo?

Africa kuwa na papa mweusi hiyo kamwe haitakaa ije kutokea. Hata kama dunia itatupa bonus ya kuishi miaka elf moja.

Ukweli ni kwamba, hakuna mzee wa ki Africa aliyewahi kupata hadhi na heshima ya kuwa papa. Na haitakaa itokee.

Simulizi ya Yesu na Biblia vililetwa Africa kwaajili ya kuwapumbaza wa Africa. Wa Africa muamini kuna mtu fulani mweupe aliitwa Yesu aliwahi kufa kwaajili ya dhambi zenu.

Hii ndio sababu mmekuwa mnazuzuka kwa kuwahusudu sana wazungu. Mmekuwa watumwa mnaosujudu dini na mila zao, huku mkizizika mila zenu za asili.

Wa Africa wengi huwa wanahisi fahari pale wanapovaa suti na kuonekana kama wazungu. Huwezi kuwalaumu.

Kimwili wapo huru, ila mikono ya bongo zao bado imefungwa minyororo ya mabaki ya utumwa wa fikra.

Najua hii ni moja ya post itayonitengenezea uadui wa kutisha barani Africa. Lakini suala la Africa kushindwa kutoa Papa wakati huu.

Labda hii itawaamsha wazikumbuke mila na tamaduni za mababu zao. Na wa Africa wanaojitambua wengi wataunga mkono nilichokiandika."
Bahatifur niturshop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…