Hatma ya Community health course

mkanyipeda

Member
Joined
Mar 8, 2018
Posts
25
Reaction score
19
Habari wanajamvi,
Bila shaka mpo vizuri.
Niende moja kwa moja kwenye maada
Mwaka 2015 August,wizara ya afya ilitangaza kozi mpya "Community health"
Ambapo waombaji walilazimika kuwa na alama D(04),kwenye cheti cha form 4 na D ya biology ilikuwa lazima.
Mwaka 2015 October,applicant waliochaguliwa walianza masomo.....lengo la kuanzishwa kwa kozi ilikuwa kama ifuatavyo:
1.kuifuta kozi ya medical attendant so
Mbadala wake community health
2.kuongeza idadi ya wataalam wa afya
ngazi ya jamii
3.kuboresha utolewaji wa huduma za
Afya ya mama na motto
4.kupambana na magonjwa ya
Kuambukizwa na yale yasiyo ya
Kuambukizwa kuanzia ngazi ya
Familia hadi taifa kwa ujumla.
Aidha toka kuanzishwa kwa kozi jumla ya intake 4 zimemaliza.
Tatizo je kwanini watu hawa hawapewi furusa za ajira toka 2016-2018,jana wizara ya afya imetangaza nafasi but sijaona watu hawa wakipewa kipaumbele.
Vumilia .B.Mmari ukiwa kama Community health National training coordinator,kwanini upo kimya juu ya suala nyeti kama hili?
Je haukujipanga wakati ww na cabinet yako mnaandaa hii kozi?
Au mnaleta siasa kwenye masuala ya msingi?
Kaa fuatilia ajira za hili kundi!!!
Nawasilisha
Kwenu
Wanajamvi.
 
Kuna nafasi za medical attendant zimetangazwa tamisemi Dodoma. Zinawahusu.
 
Mkuu kama umenipata medical attendant course ilifutwa

Sawa zilifutwa lakini, tambua kwamba mtu aliyesoma community health anaajiliwa kwa cheo cha medical attendant.

Kwa kifupi course ya community health ni mbadala wa course ya medical attendant
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…