WANAICHI WAKATAA KUBURUZWA.
Kwa namna isiyoitarajiwa leo tujikumbushe ule mstari wa biblia unaosema Enyi Wagalatia ni nani aliyewaroga? Wanainchi tulio wengi tunawafananisha Wagalatia na UKAWA kwa kweli. Maana Wagalatia walihasi imani yao kwa kutenda na kuyageukia yale ambayo walikuwa wanayakemea mwanzoni na kuyafanya kuwa ndio mtindo wa maisha yao. Hii haina tofauti sana na kilichotokea UKAWA kwani walilaani sana kuhusu ufisadi na walikuwa wanasubiria kwa hamu kuwa CCM wamteue mzee Lowassa tu ambaye viongozi wote wa UKAWA walimshutumu na kumtangaza kuwa mzee ni fisadi LAKINI BADO kawa mgombea wao nafasi ya uraisi.
Lakini leo hii bila aibu wanamnadii tena hadharani na kumtetea haswaaaa kwa kila kitu anachokifanya. Mmmhhh kweli UKAWA mmehasi imani yenu ya kuwachukia mafisadi na hakika tunashindwa kuelewa ni nani aliyewaroga kiasi hicho. Inakuwaje uchafu wa mtu ukasafishika kirahisi hvyo; au ule ubaya wake mliokuwa mnausema ukageuka kuwa wema ghafla?
Nadhani Tanzania inahitaji viongozi wenye msimamo pia kuongozwa na vyama vyenye misimamo. Zaidi ya yote inahitaji viongozi na chama ambacho kitaweza kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya wananchi. Wengi walidhani kuwa Mh.Kikwete atamteue babu kwa sababu ya urafiki wao; lakini tunampongeza Mh.Kikwete kwa kutambua kuwa maslahi ya nchi ni ya muhimu zaidi kuliko mahusiano ya kirafiki. Eti leo kwenye mitandao ya kijamii bila hata haya mnapost picha yenye maneno eti shujaa amezaliwa leo leo mnamuita shujaa wakati siku za nyuma mlimtangaza kama fisadi aliyekubuhu. Hakika mnahitaji kujichunguza ni wapi mlipokosea ili mpate kuirudia imani yenu.
Watanzania tunapaswa kuwa makini sana na wanasiasa wa namna hii,wasiojitambua na kuthamini maendeleo yetu, tusikubali kuburuzwa kwa manufaa ya kikundi kidogo:
October 25 tuudhihirishie ulimwengu kuwa tupo makini katika kipigania utaifa wetu na si vinginevyo.