Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, imemthibitisha Mbunge wa Jimbo la Momba, Mkoa wa Songwe, David Silinde (Chadema) kuwa mbunge halali jimbo hilo baada ya kumbwanga aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo, Dk. Luca Siame (CCM).
Dk. Siame kupitia kwa wakili wake, Simon Mwakolo alifungua kesi akipinga ushindi wa Silinde alioupata kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana, huku akiwasilisha hoja kuu tatu za kuishawishi mahakama hiyo kutengua ushindi huo.
Hoja za Dk. Siame ni pamoja na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Anton Mwantona kukiuka taratibu na sheria za uchaguzi, kwa nyakati tofauti Silinde alitoa rushwa kwa wananchi ili waweze kumchagua, na hoja ya tatu ni kwamba kati ya vituo 207 vya kupigia kura vituo vya 110 vilibainika kuwa ni bandia hivyo uchaguzi ulikuwa batili.
Hata hivyo, hoja hizo zilipingwa na mawakili waliokuwa wakitetea Silinde, Benjamini Mwakagamba na Adrian Mhina walipinga kwa hoja na kuifanya mahakama hiyo kutupilia mbali. Akitoa hukumu hiyo ambayo ilichukua takribani masaa mawili na nusu, leo mchana Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea, John Mgetta aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alisema mahakama hiyo imesikiliza hoja za pande zote mbili zilizowasilisha na mlalamikaji (Dk. Siame) na walalamikiwa na ambao ni Mbunge Silinde, Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo na mwanasheria mkuu wa Serikali na baada ya mahakama hiyo kuzipitia hoja zote iliona Dk. Siame kujiridhisha katika uamuzi wake pasipokuacha shaka.
Amesema hoja zilizowasilishwa na Dk. Siame, dhidi ya Silinde, ni pamoja na Jaji Mgetta alisema katika hoja zote hizo zilipingwa vikali na upande wa walalalimikiwa ambao ni ameshindwa kutoa ushahidi wa kiina na mahakama ilikubaliana na hoja za upande wa utetezi.
"Shahidi namba 26, wa Dk. Siame aliiambia mahakama hii kwamba siku ya Jumamosi, wakati wa kampeni Silinde aliwakusanya wanawake 600 kwenye ukumbi wa kanisa katika Kijiji cha Mpapa na kuwagawia Sh2000 kila mmoja na shahidi mwingine akasema siku iliyofuata Silinde aliwakusanya vijana 600 nao akawapa sh 200 kila mmoja ili wamchagu".
"Kwa akili ya kawaida kabisa hivi Polisi, Takukuru walikuwa wapi? ina maana wanamuogopa Silinde hadi kutoa rushwa hadharani kiasi hicho?" alihoji Jaji Mgetta.
Mahakama hii, imepitia ushahidi wa mashahidi wote 31, wa Dk. Siame (Luca) na wote hao pamoja na ushahidi wake binafsi (Siame) umeshindwa kuthibitishwa ukweli wa madai yao pasipokuacha shaka hivyo, basi mahakama hii inamtangaza rasmi Divid Silinde kuwa Mbunge halali jimbo la Momba aliyechaguliwa na wananchi wa Momba.
Alisema pamoja na kutupilia mbali hoja hizo Jaji Mgetta alisema Dk. Siame atatakiwa kumlipa Silinde gharama zote alizotumia kuendesha kesi hiyo kadiri atakavyoona inafaa, lakini pia Dk. Siame ana haki ya kukataa rufaa kama ataona uamuzi huo haujamtendea haki.
*Silinde aapa kutomsamehe Dk. Siame.*
Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Silinde alisema mpinzani wake hakuwa na hoja zozote za msingi kupinga ushindi wake na badala yake alitaka kuwasumbuwa wananachi wa jimbo la Momba, huku akisisitiza kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010 alipinga matokeo yake na akashindwa kesi lakini akamsamehe gharama lakini kwa vile amerudia tena safari hii hatamsamehe.
"Ninashukuru mahakama imeona kabisa hoja za Dk. Siame hazina mashiko imenithibisha rasmi kuwa mbunge, ni kweli nimepoteza muda mwingi, nimetumia gharama kubwa sana hadi leo hii. Na kwa vile mwaka 2010 nilimsamehe gharama baada ya kumshinda lakini safari hii amerudia kunisumbua na mimi naasema sitamsamehe lazima anilipe gharama zangu zote, maana inaonekana amekosa fadhila," alisema Silinde.
Source: Mwananchi