Heshima kwenu wakuu wote wakubwa kwa wadogo
Leo baada ya kutoka kibaruani nikasema ngoja nipitie Gua ang ghzo Garden ya pale bagamoyo road ili niweze kuwachimba biti hawa wachina wa Easy tv . Maana wamezidi kufanya biashara kimasikini vocha hamna wakala anaeuza Dar nzima !!!!!!!!!!!
Kufika pale nakutana na wamasai wananiambia " Rafiki ile ise tifii nahama hapa imehamia mwenge jengo la Tansanaiti karibu wanako usa finyago , karibu na kwa kakobe ""
Nikasema asante mzee nikapanda daladala nikashuka mwenge kuelekea lile jengo la Tanzanite.
Kufika kuuliza nikaaambiwa wapo hapo juu gorofa la nne ila uje kesho nikasema poa.
Nikashukuru nakuondoka ila nilichoka maana hela ya kununua king'amuzi kingine sina ni hichi cha easy shida kununua vocha mpaka uwe na namba zao wenyewe wakuunganishe mojakwa moja.
Alafu hawa wachina kama wamenipa libwata hivi sioni king'amuzi kinachokidhi haja yangu.
Daaa tabu hii .