Hatimaye mvua zimeanza kunyesha sehemu mbalimbali Tanzania

LH XiV

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
346
350
Mvua zinazonyesha zitumike kwa kilimo
pic+mvua.jpg

Siku za karibuni kumekuwa na taarifa za upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi na kuleta wasiwasi wa kutokea ukame na njaa nchini, hali iliyoibua mjadala kutoka kwa viongozi wa Serikali, kisiasa na hata wa dini.

Kwa kawaida kuna mvua za masika ambazo huanza kunyesha kuanzia Machi hadi Mei na kufuatiwa na mvua za vuli ambazo huanza Oktoba hadi Desemba pamoja na mvua za msimu mmoja ambazo zina kawaida ya kuanza Novemba hadi Aprili.

Kwa msimu huu, vipindi hivyo vya mvua havikuanza kama ilivyozoeleka katika maeneo mengi ya nchi, hali iliyojenga hofu kwamba inawezekana nchi ikakumbwa na ukame. Hata hivyo, taarifa yenye matumaini ni kwamba kuna baadhi ya maeneo ya nchi yameanza kupata mvua.

Hata hivyo, kumekuwa na hisia tofauti kuhusu mvua hizo katika maeneo hayo. Baadhi ya wakulima wanaona kama hazina tija kwa kuwa zinanyesha kipindi ambacho wanaona ama zimechelewa au zimewahi.

Kutokana na hali hiyo, mvua zinazonyesha sasa hazionekani kuchangamkiwa na wakulima na hapo ndipo tunaona umuhimu wa Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutumia wataalamu wake kutoa elimu kwa wakulima ya namna ya kuzitumia mvua hizi kwa shughuli za kilimo.

TMA haina budi kuwatafsiria wakulima maana ya mvua zinazonyesha sasa katika maeneo yao, kwani kufanya hivyo kutaondoa dhana potofu ya kuziona mvua hizi kama zisizo na tija kwenye shughuli zao|.

Kwa kufanya hivyo, tunaamini TMA itakuwa imetekeleza majukumu yake ya kuelimisha wakulima kuhusu maana ya mvua zinazonyesha na umuhimu wake kwenye shughuli za kiuchumi.

Lakini si hivyo tu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo kwa siku za karibuni ilijipambanua kuongeza idadi ya maofisa ugani nchi nzima, inapaswa kuwatumia wataalamu hao kutoa mafunzo kwa wakulima, namna bora ya kuzitumia mvua zinazonyesha.

Tunaamini kuwa wakulima endapo maofisa hao watakuwa bega kwa bega na wakulima matumizi sahihi ya mvua hizi au hata unyevunyevu utakaokuwapo kwenye mashamba vitatumika inavyostahili.

Tunaamini wakulima watapewa mbinu za kuongeza uzalishaji na upandaji wa mazao, iwapo watazitumia vizuri mvua hizo.

Ni imani yetu kwamba wataalamu hao katika hali hii ya sasa ya mvua kusuasua, watatoa ushauri kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya ardhi na mbegu.

Pia, tunaamini kuwa hata pale palipo na uhaba wa unyevunyevu kwenye udongo kutokana na uhaba wa mvua, wakulima wataelimishwa namna ya kuzingatia mbinu za kuhifadhi maji na kudhibiti ubora wa ardhi.

Tunaamini kwamba watalaamu hao wa kilimo na wenzao wa TMA, ‘wakiweka kambi’ kwa wakulima, kilio cha uhaba wa mvua ambacho kinatishia uhakika wa chakula hakitakuwapo au athari zake hazitakuwa kubwa.

Rai yetu, wakulima wasiachwe wajiamulie wanavyotaka, Serikali kupitia kwa wataalamu wake iwe nao karibu kwa kuwapa ushauri wa kitaalamu wa namna bora ya kuzitumia mvua zinazonyesha.

Tunaamini ushauri wa wataalamu hao utasaidia shughuli za kilimo kufanyika kwa tija.

Tunasubiri kwa hamu kuona weledi wa wataalamu wa kilimo katika kipindi hiki kigumu katika kilimo.


==========

Kwa wale mlioko DAR hasa maeneo ya posta na viunga vyake mtakubaliana na mimi kwamba kuna kimvua Fulani AMAZING cha kupunguza vumbi mjini

Tulikuwa tunahofu kwamba mwaka huu kuna dalili ya kukosa chakula, pesa na pia mifugo kukosa malisho. Sasa mvua imeanza kunyesha.

Nina imani sasa vyote tunavyovihitaji tutaanza kupata. Hapa nilipo ilianza toka jana saa tisa mchana hadi hivi sasa saa kumi na moja inanyesha. Tunaendela kumwomba mungu aendelee kutunyeshea mazao yetu ambayo tunategemea kuyapanda hivi karibuni
Katika pitapita zangu huku na kule. Niliamua kuingia vijijni na mashambani nijionee hali halisi ya ukame na kilimo hasa Mahindi maeneo flani ya mkoa wa shinyanga. Kwa kweli moyo uliniuma nilipoona hali ya kukata tamaa ya wananchi maana mahindi WALIOKUWA WAMELIMA neo/wilaya hiyo yamesinyaa ila hayajakauka na walikuwa hawana cha kufanya. Siku moja baadae na kuendelea Ikiwapo na leo Usiku zimenyesha mvua kubwa. Ardhi ni tepe na yenye maji ya kutosha.

Matumaini sio kwa wakulima bali hata kwa mahindi yenyewe yaliyokuwa yamechoka kabisa yamerudi kwa kasi.
Tunapotoa habari mbaya, Tukumbuke na habari njema na kutoa mirejesho chanya kama Mungu anajibu Maombi ya wenye nia njema na watanzania na Taifa lao .

Hali ikiendelea hivi, basi mambo yatakuwa mazuri zaidi

TMA wanatakiwa kusema kitu juu ya mvua hizi, ni za kudumu? zina pita? Je watu walime mazao ya kustahimili ukame au ya kawaida?
Kuna haja taasisi hii nayo ikawa active sana wakati huu ambao tunahitaji kusikia sana kuhusu hali ya hewa ili kuebusha kufanya maamuzi yenye matokeo ya hasara
Tangu jana mvua zinanyesha hapa Mwanhuzi,Mwambegwa,Nkoma na Maeneo Karibu Hapa Wilayani!
Naiomba serikali iendelee kuwahamasisha wakulima zaidi,na pia nawasihi watanzania regardless ya vyama vyetu tuendelee kuiombea hii mvua!
Kama huko kwenu imenyesha ebu tujulishe!
cc: Nicodemas Tambo Mwikonzi

Habari wakuu.,

Kuanzia leo jioni tumejaliwa kuona baraka ya mvua kwa mkoa wa Kilimanjaro. Tumesikia Pande za Holili toka saa 11 mpaka sasa inanyesha, Huko Machame inanyesha kuanzia saa 10 jioni mpaka sasa,

Naomba kupata updates kwa maeneo mengine huko

Rombo
Marangu
Same

Arusha hali ipoje!

MUNGU Amesikia kilio chetu!
 
Niko mikocheni hamna cha mannyunyu wala nini jua tu na tumawingu kwa mbaliii
 
Back
Top Bottom