Hatimaye Mr. Blue amuangukia Diamond Platnumz na kumuomba yaishe

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,464
21,197
Awali ya yote ngoja nicheke kihutu kwanza "Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii".

Kwa muda mrefu msanii Kheri Sameer (Mr Blue) amekuwa yupo kwenye bifu zito na Diamond Platnumz Simbaaaaaaaa mara kwa mara Blue amekuwa akimponda Diamond Platnumz lakini waswahili husema jibu la mjinga ni kumkalia kimya tu ipo siku ata erevuka,na siku zote kama unajua unajua tu watu watapiga kelele mwisho wa siku watanyoosha mikono bila kupenda.

Sasa bhana Diamond a.k .a mzee wa minyoosho anazidi kuwanyoosha tu watu , na mmoja mmoja anaanza kunyooka, alianza kunyooka ,Richi Mavoko,akafuatia H-baba akaja Baraka the Prince sasa zamu ya Mr Blue naye kanyooka bila kupenda. Ha ha ha ha team Kiba inazidi kusambaratika tu, hapo amebaki Tundaman na adui kuu Ally Kibanio

Yani Blue kanyooka haswaaa, tena kasindikiza na Caption Mungu ni mwema maana alijijua alichokuwa anakifanya ni kitendo cha kijinga kapitwa na fursa nyingi kwa kitendo chake cha kumchukia Diamond.

Diamond kiroho safi huwa hana hiyana siku zote ameupokea msamaha wa Mr Blue kwa moyo mkunjufu

IMG_20180601_152239_470.jpg
IMG_20180601_152223_450.jpg
 
Hili bifu ulikuwa hulijui wewe tu, wapenzi wote wa burudani wanalijua.
Hao si wapenzi wa burudani...labda tuwaite wabakaji wa burudani...

Kwa maneno mengine unataka tuaminisha kwamba kila anae feat. na kiba ana bifu na Diamond.

Haipo hiyo ndugu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom