Hatima ya EAC

anjo

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2009
Posts
299
Reaction score
97
Moderator na Wanajamii,

NingependaCandid kutoa maoni yangu kuhusu jinsi tunavyojadili masuala mengi ikiwa ni pamoja na yale yanayohus EAC. Ningependa tufanye uchambuzi bila chuki na vilevile tutumie lugha iliyo bora zaidi.

Kuhusu EAC, ni vizuri tukafahamu mambo muhimu ya Jumuiya ili tuelelewe jinsi ya kuhusisha hayo na maendeleo yetu. Kuna miradi mingi inayozihusisha nchi zote tano. Katika hiyo miradi kuna corridor mbili: central and northern.

Central corridor ni hii ya Tanzania: kutokea bandari ya Dar, Morogoro, Dodoma, Singida, Igunga, Nzega, Isaka, Kahama, Ushirombo, Rusumo, Kigali/Bujumbura. Northern corridor ni ile ya kutoka Mombasa, Nairobi, Busia, Kampala, Kigali. Kutokana na hali hii, nchi za Kenya, Uganda na Rwanda walikutana ili kuharakisha ukuaji wa northern corridor. Miaka miwili iliyopita, Tanzania, Rwanda na Burundi walikutana kujadili central corridor na haikuwa tatizo kwa nchi za Uganda na Kenya. Kinachoweza kujadiliwa ni efficiency ya mikutano hiyo miwili. Wa central corridor umekuwa ukisuasua sana lambda ndo maana hata Rwanda inatafuta alternative na hivyo Burundi na hata DRC watajiunga. Hii ni kwa sababu si suala la siasa bali njia iliyo na unafuu wa kusafirisha mizigo.

Kinachozingatiwa ili mradi uwe wa Jumuiya ni pale ambapo utahusisha nje mbili au zaidi. Kutokana na hili, mkutano uliofanyika Uganda ulihusisha nchi tatu na wana haki ya kufanya hivyo kwani haikinzani na taratibu za EAC. Pia, kuwepo kwa EAC Kama forum hakuondoi mahusiano ya nchi mbili au tatu.

Kwa hiyo tunapojadili masuala, tusikimbilie kutoa maneno yasiyo sahihi na wenye kusababisha mkanganyiko kwa watu.

Anjo
 
mkuu pamoja na hayo uliyogusia,inasemekana baadhi ya maazimio ni siri ya Team KKK.na yalifanyika ktk kikao cha siri bila kuhusish media.hapo ndipo baadhi ya watz wanaingiwa hofu na hatima ya EAC.nisaidie hapo chief.
 
mkuu pamoja na hayo uliyogusia,inasemekana baadhi ya maazimio ni siri ya Team KKK.na yalifanyika ktk kikao cha siri bila kuhusish media.hapo ndipo baadhi ya watz wanaingiwa hofu na hatima ya EAC.nisaidie hapo chief.

Kama ni siri yao wewe umeyajuaje? Hofu ya nini? Itifaki si ipo? Ila ninachosahuri kwa upande wa TZ ni kwamba wawe wanapeleka watu wenye weledi kuanzia kwenye lugha inayozungumzwa na uelewa wa masuala yanayojadiliwa. Pasipo kuwa waangalifu katika suala hili tunaweza kujuta badaye. Nimewahi kuhudhuria mkutano mmoja wa hizi nchi tano kuhusiana na masuala la elimu. Wenzetu walileta watu wengi wenye uelewa on the issu, lakini sisi hata wale waliokuwako ili shida kuelewa the issue that was being discussed. ndugu zangu, siyo kila kitu ni siasa. Mambo mengine ni uelewa wa jambo husika na kuweza kuli-argue ili watu wakuelewe. Sasa watu wanachaguana kwa sura. Hii inaweza itatuathiri.
 
ka hiyo ujenzi wa bomba la mafuta nayo ni northern corridor? sidhani kama ww ni mtanzania. huna uchungu na nchi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…