Hatari: Zanzibar ni zaidi ya inavyonenwa!

Dah! Tukiacha unafiki, adui mkubwa wa Zanzibar ni Wahafidhina wa CCM upande wa Zanzibar wanaojiona wana nguvu ya kuamua lolote watakalo juu ya Zanzibar ilihali ukweli ni kwamba hawana nguvu hiyo wanayoiringia!
Hawa ni watu ambao bila kificho nadiriki kusema ni "Watumwa Huru" wa Wahafidhina wa CCM Bara! Hawana lolote zaidi ya kutumiwa na CCM Bara! Hawana upendo kwa Nchi yao Zanzibar bali upendo wao ni kwa CCM Dodoma! Wanaongozwa kama ng'ombe wapelekwao machinjioni!
Wanazubaishwa na vijirupia kidogo kutoka bara,wakirembeshwa na vijiyoyozi vya magari ya kifahari toka kwenye pesa za mfalme wao CCM Tanganyika!
Hawana tofauti na yuda eskarioti!
Wamelewa madaraka! Hawapo tayari kuiona Zanzibar ya watoto wao ikiinuka ilihali wao hawapati chochote kitu! Walafi!
Nina imani hata Karume huko aliko anawalaani! Haishangazi sasa kuona ngome yao taratibu inadhoofika! Wanakataliwa nyumbani (Unguja) kama walivyokataliwa huko Pemba!
Wanae nabii wa kuwasaidia kuisogeza mbele Zanzibar yao (Seif) lkn ilinenwa na wenye hekima kwamba nabii huwa hakubaliki kwao!
Wanafiki wakubwa! Wameshindwa lkn wameharamisha ushindi! Sasa hata Shetani amegoma kuwapa sababu za maana za kufuta uchaguzi!
Shetani hapendi unafiki! Hachanganyi safi na chafu! Kwake chafu ni chafu na safi ni safi!
 
acheni uvivu someni yote mpate uwanja mpana wa kuchangia. japo baada ya kumaliza nimebaki njia panda nini kifanyike! mwisho wa siku ukweli utajulikana na utaiweka huru Zanzibar! kwa kifupi hakuna kiongozi ambaye alishawahi kujitosa kwa uaminifu kwa utashi wake akashughulikia kwa makini swala hili! kwangu naona Magufuli kwa hili watakuwa wanamuonea kwa kuwa in viporo vilivyoachwa na waliomtangulia yaanit salmin, mkapa,karume kikwete na Seif mwenyewe
 
Sasa hata Shetani amegoma kuwapa sababu za maana za kufuta uchaguzi!
Shetani hapendi unafiki! Hachanganyi safi na chafu! Kwake chafu ni chafu na safi ni safi!............aisee duh!
 
Between the lines Luqman you have a known leaning you cannot hide brother be true to your self
 
Makala nzuri ila jawabu lake ni mwongozo tuliojiwekea wa sheria na kanuni za uchaguzi ,Jecha hawezi na hana mamlaka ya kufuta uchaguzi ,jingine ambalo ni kubwa lao linalo mzamisha yeyote yule ,ni ile fomu ya malalamiko ambayo huwa inajazwa kwenye kituo ,ni wapi Jecha alipokea au alipelekewa fomu hio ,

Na je tukirudi kwa wahusika wa uchaguzi ambao ni vyama vilivyohusika na hapa ndipo palipo na target nzima ya matokeo ..Je kuna mdau yeyote alilalamika ??? Kama ni uelewa basi CUF walilalamika miaka ya nyuma kuwa uchaguzi umeporwa tokea 1995 ,na uchaguzi haukufutwa wala kurejewa ,tume ilimtangaza mshindi bila ya kujali ,iweje leo hakuna hata malalamiko ?

Haina haja ya melezo mengi kanuni za kiubunge na kiuwakilishi ni kufungua mashitaka kama tunavyoona hapa Tanganyika ,alindwae ni Raisi tu ,jecha ametoa sababu tisa za kufuta uchaguzi kwa nini hakupeleka mashitaka kwenye mahakama ni nani alimkabidhi malalamiko hayo tena baada ya siku tatu kupita na matokeo yameshabandikwa katika vituo vyote,

Ajabu leo hii watu au chama cha CCM ambacho kingehitaji kuwa cha mwanzo kulalamika kabla ya Jecha kinategemea sababu alizozizua Jecha !!! kama si ajabu ni kitu gani ?

Hapa hapahitaji maelezo za kutafuta kila kitu kipo open ,na kuhusu Seif kujitangaza excuse hio sna si ya kuitegemea maana unapobandika matangazo kwenye ukuta ndio umetangaza ,hivi matangazo ya Seif yalikuwa rasmi ? Au ni sawa na yale yaliobandikwa ukutani ? Wana sheria wapo hapa JF watueleze maana ya kutangaza !
 
If Luqman wants to discuss in largess then he should go back to the history of Zanzibar and the revolution of 1964 not to do "pick and choose," that is "Selective premise of data," It is unacceptable in researching. It is unacceptable as the real impact or outcome will not be realised.
 
Uchambuzi wako haujabakisha hata chembe moja ya ukweli..hongera mkuu
 
Uchambuzi mzuri sana, wenye uliozingatia misingi ya utafiti na tafakari huru.
Tatizo:
1. ''wasomi'' wetu hapa JF bongo zao zimechoka, zimeshazoea kusoma ujinga - unapowapa jambo linalohitaji kuzisumbua bongo zao hawajiwezi
2. Jambo lililoandikwa ni somo zuri ila kuna watu wanaleta kebehi za kijinga!
3. Maandiko haya yanafundisha na yanasisimua akili na kumpa msomaji fursa ya kuiona sintofahamu iliyopo katika mifumo yetu inayotegemewa kuongoza na kutoa haki!
 
Maneno mengi ya nini?
Zanzibar na hali yake ya kisiasa inajumuishwa na hili: kuna waliopindua serikali ya waarabu, na kuna waliopinduliwa na wazazi wao walikuwa katika srikali ya waarabu.
Mengine yote ni maji moto tu na hewa chafu.
Mzizi wa fitna upo hapo, na umoja wa kitaifa ni geresha toto tu.
 
Jiulize cuf ina majimbo pemba na unguja 9,wakati ccm haina jimbo hata moja pemba.
Tatizo waunguja hawataki kutawaliwa na cuf eti wanasema ni sawa na kumrudisha sultani.Ccm zanzibar inabebwa na bara sii wazanzibar.
Hivyo kura ni hadaa tuu kwa watanzania majibu wanayo mfukoni ccm
 
Mkuu usirudie tena ku QUOTE uzi mrefu kama huu unatuchosa watumia simu halafu vilevile kwa sheria za Jf ni kosa!
 
Kwa matokeo yalokwisha tangazwa na ZEC yakaonesha kuwa CUF walikuwa tayari wana majimbo tisa kutoka unguja, ni pathognomonic kuwa washindi, sema tu kuwa hata wakitangazwa kuwa washindi ccm Zanzibar itaanza ku behave kama CUF inavyo behave wakiwa nje ya dola
 
Mtoa post siku ukigundua uwezo wako utatoa kitabu na si hivi vimaandishi ambavyo nimesoma kwa dk 10.
Ila nimepata kitu kwa wa changamoto (shetani hapendi unafiki kwake nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…