Hatari ya App za Mikopo kwenye simu

Hatari ya App za Mikopo kwenye simu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
1_20250517_143643_0000.png

Nchini India watu wengi wameathilika na program ambazo zinatoa mikopo ya pesa kwa kuweza kudhalilishwa kutokana na mikopo waliokopa.

Takribani zaidi ya wahindi 60 wamejiua baada ya kunyanyaswa na kutishiwa kwa namna moja au nyingine baada ya kuomba mikopo. Ni app ambazo zinapatikana Kwenye soko la play store inatoa mikopo kwa watu kwa namna moja au nyingine.

2_20250517_143643_0001.png

3_20250517_143644_0002.png

Ukifanikiwa kupata mkopo unapewa hapo hapo mkopo yani hakuna kusubiria siku mbili au moja ila shida yake inaanza unasumbuliwa Kwenye kurudisha maana mkopo wao ni zaidi ya "kausha Damu😃!".

Kwani ukifanikiwa kuinstall app Kwenye simu Yako basi inachukua picha zako kwa namna tofauti tofauti na kuanza kuzisambaza mtandaoni wakati mwingine wanakuweka mpaka kwenye kurasa za ngono nk.

4_20250517_143644_0003.png

6_20250517_143644_0005.png


Picha zako zinasambazwa mitandaoni jambo linalopelekea wahindi wengi kupatwa na msongo wa mawazo na kufikia hatua ya kujiua kwani unaweza pigiwa simu kwa siku zaidi ya 100 kutaka urudishe pesa.

5_20250517_143644_0004.png


7_20250517_143644_0006.png


Wakati mwingine wanawapigia ndugu, jamaa na marafiki zako na kuwasumbua, watu wengi walioathilikq ni wahindi, waafrika , watu wa Asia nk.

8_20250517_143644_0007.png


Mjihadhari na program za mikopo kwani Zingine zinachukua taarifa zako na kuzisambaza mtandaoni
 
Back
Top Bottom