Habari wana MMU?
Nilikua nina mpenzi wangu tuliependana sana kwa muda wa kama miaka miwili hivi. tumepitia migogoro kadhaa katika kujaribu kumshawishi awe vile nipendavyo naye kunifanya niwe vile apendavyo. na kwa kipindi chote hicho tumekua tukikosana na tunayazungumza wenyewe yanaisha ndani ya siku mbili au tatu. cha kushangaza mgogoro wetu wa mwisho ulitokea miezi kama mitatu na nusu iliyopita, najitahidi kusuruhisha tuanze upya mwenzangu amegoma kabisa na anaonesha kunichukia gafla pasipo kumwelewa kwa nini kabadirika ghafla maana tatizo hili la mwisho halikuwahi kuwa kubwa kama tuliyoyapitia na tukasuruhisha na mapenzi yetu kuwa na furaha kuliko ilivyokua kabla. sasa sielewi sijui mwenzangu kishapata mwingine anaemchanganya kiasi kwamba kasahau ghafla tulipotoka?
akikosea yeye msamaha lazima niombe mimi, nikikosea mimi inabidi nijipange haswa kuhakikisha ananisamehe,kifupi hawezi kukubali hata siku moja kua ana makosa, kwa kweli simuelewi kabisa.
wenye uzoefu,hiyo ni dalili ya nini kwa mwanamke?
Nahisi mmekuwa na gomvi nyingi sana mpaka dada amechoshwa. Raha ya mapenzi ni kufurahi na mfurahie penzi pamoja. Huenda mwenzio hafurahii tena na hiyo ndio ilikua gia ya kuondokea.
Tulia; tulizana wala usimwulize tena. Mwache apate kamuda alone labda atarudi au huenda asirudi vilevile. Kwahiyo wewe ona kuwa upo single kwasasa mpaka pale litapolotokea penzi tena. Pengine la huyuhuyu au pengine la mwingine.
Kila lakheri
Mbona ni kama umetoa majibu kabisa kabla ya kushauriwa. Hebu soma vizuri hizo paragraph za juu jibu lako liko hapo
Labda ugomvi wenu wa mwisho ulivuka mstari, akaona bora asepe mazima.
Habari wana MMU?
Nilikua nina mpenzi wangu tuliependana sana kwa muda wa kama miaka miwili hivi. tumepitia migogoro kadhaa katika kujaribu kumshawishi awe vile nipendavyo naye kunifanya niwe vile apendavyo. na kwa kipindi chote hicho tumekua tukikosana na tunayazungumza wenyewe yanaisha ndani ya siku mbili au tatu. cha kushangaza mgogoro wetu wa mwisho ulitokea miezi kama mitatu na nusu iliyopita, najitahidi kusuruhisha tuanze upya mwenzangu amegoma kabisa na anaonesha kunichukia gafla pasipo kumwelewa kwa nini kabadirika ghafla maana tatizo hili la mwisho halikuwahi kuwa kubwa kama tuliyoyapitia na tukasuruhisha na mapenzi yetu kuwa na furaha kuliko ilivyokua kabla. sasa sielewi sijui mwenzangu kishapata mwingine anaemchanganya kiasi kwamba kasahau ghafla tulipotoka?
akikosea yeye msamaha lazima niombe mimi, nikikosea mimi inabidi nijipange haswa kuhakikisha ananisamehe,kifupi hawezi kukubali hata siku moja kua ana makosa, kwa kweli simuelewi kabisa.
wenye uzoefu,hiyo ni dalili ya nini kwa mwanamke?
Je ww ni mwanamke au mwanaume?
Ukibebembeleza mtoto/mtu yeyote anayelia, unamuongezea hamu ya kulia zaidi...
Make it like this, kama ulishamwambia yaishe lakini yeye akataka ligi, mkuu kata uzi kwa muda, ukweli nakwambia km anakupenda, basi atajirudi..
Watoto wa kike wanapenda sana kutikisa buyu kuona kama kuna asali
Yawezekana makosa kwako madogo kwa mwenzio makubwa.Na kibaya zaidi ni makosa yanayojirudia rudia pia amekusoma kaona kama huna future naye."Kakosa yeye wewe unaomba msamaha" ni dalili ya mapenzi ya ubwana na mtwana
Kosa ni kosa, pole kwa unayopitia.
Ukiamua kukishusha sana kwa mwenzio hayo lazima hutokea. Hebu fanya kumpotezea. Hata akipiga simu ongea dry... usipoona akarudi kwa kasi...