Hata nipigwe bani, kamwe sitetereki!

BekaNurdin

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
2,267
2,041
Hata nipigwe bani, Kamwe sitetereki
Ninapopigwa bani, Hata kama si haki
Nitabaki kundini, Jeefu sitoroki

Siku tano kambani, Katu haz'zoeleki
Nimetengwa kundini, Na mods kindaki
Kwani uzito gani, Ya kwangu misiteki?

Wanagawiwa bani, Kana kwamba ni keki
Wawekwa gerezani, Na mamodi kindaki
Watiwa hatiani, Kosa bila hakiki

Mwapata sifa gani, Wengine piga loki?
Mwasutwa nafsini, Bila kutenda haki
Ukali legezeni, Jamvi liwe rafiki

Walio kifungoni, Furaha hailiki
Pia mahakamani, Mello we hukumbuki?
Na wengine kwa nini, Mwawatia maloki?

Mkizidisha bani, Mtazidisha chuki
Siredi za udini, Zinachochea chuki
Mwazipotezeani, Mbona hazifungiki?

Matusi ya nguoni, Na siasa za chuki
Zinaletwa jamvini, Na hazipigwi loki
Mkitaka amani, Mzingatie haki

Mods jipimeni, Kama mwatenda haki
Je anifea bani, Yawapandisha kiki?
Bure nisameheni, sienezagi chuki

Nimetoka kifungoni, Kwa madaha lukuki
N'taheshimu kanuni, Nitahubiri haki
Kuna ugumu gani, Kuzingatia haki?
 
Hata nipigwe bani, Kamwe sitetereki
Ninapopigwa bani, Hata kama si haki
Nitabaki kundini, Jeefu sitoroki

Siku tano kambani, Katu haz'zoeleki
Nimetengwa kundini, Na mods kindaki
Kwani uzito gani, Ya kwangu misiteki?

Wanagawiwa bani, Kana kwamba ni keki
Wawekwa gerezani, Na mamodi kindaki
Watiwa hatiani, Kosa bila hakiki

Mwapata sifa gani, Wengine piga loki?
Mwasutwa nafsini, Bila kutenda haki
Ukali legezeni, Jamvi liwe rafiki

Walio kifungoni, Furaha hailiki
Pia mahakamani, Mello we hukumbuki?
Na wengine kwa nini, Mwawatia maloki?

Mkizidisha bani, Mtazidisha chuki
Siredi za udini, Zinachochea chuki
Mwazipotezeani, Mbona hazifungiki?

Matusi ya nguoni, Na siasa za chuki
Zinaletwa jamvini, Na hazipigwi loki
Mkitaka amani, Mzingatie haki

Mods jipimeni, Kama mwatenda haki
Je anifea bani, Yawapandisha kiki?
Bure nisameheni, sienezagi chuki

Nimetoka kifungoni, Kwa madaha lukuki
N'taheshimu kanuni, Nitahubiri haki
Kuna ugumu gani, Kuzingatia haki?
Mods wana ubabe wa kisisiemu Mimi nilipigwa ban kisa nimesema siti ya kwanza hilo tu likanipa ban sasa kuwahi siti ni kosa au kuna wenye viti vyao humu dah mods mnapoteza credibility
 
Mods wana ubabe wa kisisiemu Mimi nilipigwa ban kisa nimesema siti ya kwanza hilo tu likanipa ban sasa kuwahi siti ni kosa au kuna wenye viti vyao humu dah mods mnapoteza credibility
Naskia ISIS kawa moderator chizi kapewa rungu daadeki😧😧
 
Mods wana ubabe wa kisisiemu Mimi nilipigwa ban kisa nimesema siti ya kwanza hilo tu likanipa ban sasa kuwahi siti ni kosa au kuna wenye viti vyao humu dah mods mnapoteza credibility

ngoja na mie nijaribu ..mods seat ya kwanza
Sema nini walikuonea


If it isn’t perfect ,it’s not good enough
 
yooo yoooo yoooo yooooo
asee ban ni kitu ibaya, haizoeleki hakyanani
siku yako inakua mbaya, ila kuchangia jukwwani,
nilikula ban moja, ni wiki mbili sio nyingi,
yoooo yooooo chikichiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom