kensh
JF-Expert Member
- Jul 19, 2012
- 527
- 113
Hatimaye ile tamthilia yenye mbwembwe,vituko,uhuni na kila aina ya kihoja imeisha pale kalenga.Jumapili ya 16/3/2014 imehitimisha tamthilia hiyo,imetuacha na ama majibu machache kuliuko maswali,ama haijatupatia jibu lolote kwa maswali yetu.
Najiuliza,nani kaibuka mshindi? Na nani kapoteza? Kwanini?
Wapo ambao wakisoma swali la mwanzo,haraka wangebeza na kuona mleta hoja hajitambui au hajui lolote na ni mpiga kelele wa kawaida tu,na wangemtaja haraka alieshinda kuwa ni Mgimwa,yule mtoto wa marehemu William Mgimwa.
Na,wpo wale ambao wangesema mshindi ni Grace,yule mgombea wa Chadema,sababu wanazo.
Siwafahamu sana waliokuwa wakigombea,ila nawezasema jambo kuhusu nilivowafahamu kipindi kile cha kampeni,nilimuona Mgimwa,nilimsikiliza na kupima uwezo wake wa kujieleza na kupambanua mambo.Nilimsikiliza Grace pia,nilimfuatilia alivyojenga hoja,alivyofafanua mambo na kuwasilisha mbele ya jamii.Nilishawishika sana na namna Grace alivyojieleza,alionesha uwezo na uthibitisho wa alichokisema,alijenga hoja na kutoa ufafanuzi mbalimbali wa jambo ili wananchi welewe alichojaribu kuwaeleza,alithibitisha uwezo binafsi.Tofauti na Mgimwa,ambaye alionekana kukariri tu yale aliyoyasema,hakuwa na uwezo zaidi wa kuongezea hoja na kuzipambanua zaidi ya vile alivyokaririshwa,alisema kwa vituo vingi,akiashiria kujaribu kukumbuka sana yale aliyokaririshwa.
Hata iweje,Mgimwa ndie mbunge wa Kalenga kwa tiketi ya CCM,hayo ndiyo maajabu yaliyotokea Kalenga!
Kwanini Grace alipoteza?
Wapo walionichekesha walipokuwa wakijibu swali la namna hii,waliziziba akili zao zisitafakari wala kuona mambo kihalisi.Walimkimbilia mtu wao,walimtaja na kujenga hoja kuwa bila huyo Chadema haiwezi,si lolote wala chochote,wakapaaza sauti,wakamtaja kwa majina yake mtu huyo kuwa ni Zitto Zuberi Kabwe.Wakasema mzimu wa huyo,unaitesa Chadema.Nikajiuliza 'ANA MZIMU?'
Nikajikumbusha machache ya juu juu tu,kuwa je,kule Arumeru alishiriki huyo mwenye mzimu? Je,kule jimboni kwake,kuna madiwani wangapi wa Chadema waliopatikana kwa mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu? Na kigoma kwa ujumla ina madiwani wangapi wa Chadema waliopatikana 20101? Kata zilizonyakuliwa na CCM au NCCR kule Kigoma wakati wa uchaguzi mkuu,nani alikuwa na Mzimu kipindi hicho? Wanaojenga hoja kuwa kushindwa kwa Chadema kule Kalenga ni matokeo ya kutimuliwa kwa ZZK,ni watu hoi kifikra au wana mahaba ya kupindukia kwa ZZK kiasi kwamba kila jambo linaloenda kombo kule Chadema,wao husema sababu ni kutokuwepo kwa ZZK,hawajui kuwa ZZK ameikuta Chadema ikiwa na mafanikio yake na hata matatizo yake pia,na hakukua na mwenye mzimu! Kuna uwezekano kuwa wanaomtukuza ZZK wanafanya kusudi kumpotosha au wanatafuta fursa moyoni mwa ZZK,bila shaka wataipata huko ATC.
Nani adui wa Chadema Kalenga?
Bilashaka swali hili limejibiwa,tena labda kabla sijajiuliza.Wengi wamesema,mimi narudia au kuongezea tu.Adui wa chadema ni DAFTARI LA WAPIGA KURA na si mzimu wa ZZK! Kwanza hana Mzimu,na kama anao,basi anautumia kwa mengine, yake binafsi.
Daftari la wapiga kura ni kikwazo kikubwa kwa upinzani nchi hii.Ukitizama sana muamko wa siasa katika nchi hii,utaona jinsi vijana walivyo na hamasa ya kushiriki katika uchaguzi,wanataka kuleta mabadiliko HARAKA! Tatizo ni hilo DAFTARI. Daftari halijafanyiwa marekebisho yoyote ya maana,nakumbuka mimi nimeandikwa katika daftari 2004,kule kwetu Mbozi.Leo ninaishi Mwanza,je,nitashiriki vipi uchaguzi hapa Mwanza? Nirudi nyumbani pindi za uchaguzi ili tu nikapige kura? Nauli? Pia,je tangu 2004,ni vijana wangapi leo hii 2014 ambao wana sifa zote za kuwemo katika daftari na hawamo na wanashiriki sana katika kuhamasisha wakati wa kampeni za chaguzi mbalimbali? Wengi wa wapiga kura ni vijana na hawamo katika daftari la wapiga kura,na hao ndio hasa wanaotaka mabadiliko,ndio wanaotaka vyama mbadala,ndio wanaotaka chadema,cuf au nccr.
Endapo daftari la wapiga kura likiboreshwa leo,hakika nitavitia moyo vyama vyoote vya upinzani vishiriki katika chaguzi mbalimbali.Vinginevyo,vyama hivyo vya upinzani vitazidi kulialia tu kuwa vimechezewa rafu hii au ile bila kupata ufumbuzi.Vitalilia jeshi la polisi,vitalaumu green guard,vitalaumu kauli ya mwenyekiti wetu ile ya kuacha unyonge na wala havitapata ufumbuzi.
Vyama vya upinzani na wapenda demokrasia,waje pamoja,washirikiane na watanzania wengine,kwa pamoja tudai marekebisho ya DAFTARI LA WAPIGA KURA lifanyiwe marekebisho yoote muhimu ikiwa ni pamoja na kuandikwa kwa wengine woote wenye sifa za kuwemo katika daftari. IT CAN BE DONE! Vinginevyo,tutaendelea kutegemea mizimu ya akina Lisu,Mbatia,Mtikila na wakati mwingine hata mzimu wangu.
Chalinze hapatakuwa na jipya zaidi ya muendelezo wa kile kilichotokea Kalenga,ila daftari likiboreshwa kesho kabla ya uchaguzi,hakika Chalinze itashangaza wengi,itaenda upinzani.