Kuna dada mmoja mmoja ambaye anafanya kazi kama mwalimu wa chuo cha ualimu katika mkoa fulani.Huyu dada kaolewa na jamaa mmoja ambaye naye pia ni mwalimu wa VETA.Inasemekana huyu jamaa alifanikiwa kupata hii kazi kutokana na influence ya mkewe.
Maisha yao ya ndoa yalikuwa yakienda vizuri tu lakini baadaye mawimbi yakaitikisa ndoa hii.Yule jamaa akaanzisha uhusiano na mwanafunzi mmoja wa kike wa chuo cha VETA.Mahusiano yakaenda mbali mpaka jamaa ikamtundika mimba huyu dada wa VETA.Mpaka anampa ujauzito huyu dada,huyu jamaa na mkewe walishafanikiwa kupata watoto wawili.
Sasa ukafika wakati wa yule dada kujifungua.yule jamaa akasingizia ana shughuli ya kikazi dar-es-salaam na akafanikiwa kuondoka na yule dada mpaka dar.
Akiwa dar,wambea wakampa yule mke wa jamaa mkanda mzima kuhusu safari ya mumewe dar.Yule dada msomi mzuri tu akafunga safari hadi kwa kalumanzila kwenda ku seti mitambo.Yaap,mitambo ikajibu,yule dada huku dar akapoteza maisha baada ya kujifungua na pia maskini kichanga kisicho na makosa kikapoteza uhai masaa machache baada ya kuzaliwa.
Yule dada alipozipata habari za maafa haya alishangilia huku akiongea kinafiki kwamba MUNGU amejibu maombi yangu.Baada ya kumalizika msiba,jamaa akaona hamna jinsi zaidi ya kurudi na kumwangukia mkewe na kuomba msamaha.Mke akamsamehe mume na kumpokea tayari kwa ukurasa mpya wa maisha.Lakini yule dada akaona haitoshi,kwani alijua wazi mumewe hampendi kwa dhati ukichukulia fact kwamba yeye mwanamke kampita miaka kadhaa mwanaume.
Mwanamke akafunga safari hadi mkoa mmoja kusini mwa TZ kwenda kumuona mtaalam.Akamwambia mganga;'Ninaomba umtengeneze mume wangu kiasi kwamba mpipi wake ufanye kazi kwangu mimi tu,kwa wengine nope!.
Yaap,aliporudi kwa mumewe,ile dawa ilifanikiwa lakini ikawa too much!!Ule mpipi umegoma kufanya kazi hata kwake yeye mwenye mali!.Maskini mwanaume mwenzetu kaharibiwa.Kwetu siye wanaume;tusikubali kuoa mwanamke tusiyempenda kutoka moyoni eti kisa unataka kulipa fadhila ya kitu alikusaidia maishani,utaishia kumsaliti na kumuumiza.Kwenu wanawake;Mapenzi halazimishwi hata kwa dawa!