Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,454
- 32,980
Mwinyi Mangara tafadhali soma historia hiyo hapo chini kutoka kitabu cha Abdul Sykes inayoendana na picha hiyo uliyotuwekea:
''Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao: Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Victor Mkello, Dhili Mgunya, Ali Mohamed, Abdallah Mohamed na Mohamed Sadik.
Peter Mhando alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya kwanza ya tawi la TANU mjini Tanga.
Mara tu baada ya mkutano huu wazee wa Tanga wakiongozwa na Makoko Rashid, mwanachama wa zamani wa TAA walianza kufanya kampeni kwa ajili ya TANU.
Chama kilipata msukumo mwingine na kuongezeka nguvu wakati Sadik Ali Patwa Muasia tajiri alipoingia TANU.
Patwa alikuwa Muislam wa madhehebu ya Shia.
Patwa alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Zanzibar mwaka 1918 baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Kwanza.
Pale Tanga Patwa alianzisha kiwanda cha soda na akatajirika.
Wakati huo wa zama za ukoloni wakati Waasia wenzake walikuwa wakiwabagua Waafrika, Patwa alikuwa akikaa na Waafrika wa rika lake akinywa nao kahawa.
Halikadhalika watoto wake wakawa wanacheza kandanda na vijana wenzao wa Kiafrika katika vilabu vya Tanga.
Hili lilikuwa jambo geni na lisilokuwa la kawaida kutoka kwa familia ya Kiasia wakati wa ukoloni.''
Patwa alisaidia harakati za kudai uhuru kwa hali na mali, na akaifanyia kampeni TANU miongoni mwa jamii yake mwenyewe ya Kiasia.
Wakati wa harakati Nyerere alikuwa akifanyiana maskhara na Patwa akimwambia, ‘’Mzee Patwa baada ya kupata uhuru nadhani tukuteuwa uwe balozi wetu India.’’
Lakini Patwa hakuiona Tanganyika huru, alifariki kabla ya uhuru kupatikana.
Picha:
1.Sadik Patwa na Julius Nyerere
2.Mwalimu Kihere
3.Peter Abdallah Mhando
4.Mamboleo Rashid Makoko
5.Hamisi Heri
6.Sheikh Abdallah Rashid Sembe