Kwanza kabisa napenda kuchukuwa fursa hii kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kunipa pumzi hii adimu hadi leo gentamycine nimegonga miaka deshi deshi. Pia napenda kuwashukuru sana wazazi wangu baba na mama gentamycine kwa kuweza kunileta duniani, kunilea na kunionyesha upendo wa hali ya juu ambao hata siwezi kuulipa zaidi tu ya mimi kuwaombea kheri na fanaka tele hapa duniani.
Ila furaha yangu haitokamilika kama sitasema akhsante kwa wamiliki, uongozi na wafanyakazi wote wa jamii forum kwa ushirikiano wenu / wao kwangu japo hata mimi nimechezea sana tu ban zao hadi nimekoma. Hakika jamii forum imeniongezea upeo mkubwa wa kujenga hoja na kuyajua mengi mazuri na mabaya na nawatakieni kila la kheri ktk kuendelezo wa hili jamvi zuri na ninalolipenda.
Mwisho wa yote sitakuwa na furaha ya moyoni kama sitosema pia akhsante kwa wale wote ambao nimejenga nao urafiki humu jamvini ( ni wengi mno na siwezi kuwataja ) lakini napenda pia kuchukua fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliokwaruzana au tuliokwaruzana humu kwa hapa na pale na binafsi nasema samahani na naomba radhi sana kwenu kama nilitokea kuwakwaza siku moja.
Nikiwa naianza safari yangu mpya ya miaka yangu deshi deshi leo naomba maombi na dua zenu ili nizidi kuwa na maisha marefu na mema.
NB: Na naomba pia leo nitoe ruhusa hii maalum kwenu na imetoka moyoni kwangu kabisa ya kwamba kama nimekukwaza kwa jambo moja au jingine au hupendi kitu fulani ambacho labda huwa nakifanya humu jamvini tafadhali naomba mkiseme na nimetoa ruhusa japokuwa nasheherekea birthday yangu leo naomba wale wote wenye duku duku na gentamycine kuwa huru kunisiliba utakavyo na nitaheshimu yale yote mtakayosema.
Lakini pia kama kuna wale wanaompenda gentamycine kwa mambo kadha wa kadha basi siyo mbaya pia mkayasema yenu mazuri ya moyoni na hata akina dada labda mnaompenda na kumtaka gentamycine please fungukeni leo ili nimchague mmoja wa kuanza nae maisha kwani miss chagga na mahondaw tayari nimeshawaacha na mlango upo wazi kwenu.
Happy birthday gentamycine.
Nawapendeni nyote na mbarikiwe sana na mno na tupo pamoja.
Mwaaaaaaaaaaaah! Pokeeni busu la upendo.