Hapa ndo wanaume huwa tunafail

JOMI

Senior Member
Joined
Oct 9, 2012
Posts
144
Reaction score
118
Mwanaume mmoja aliwatongoza wanawake watatu tofauti na nia yake ni kufanya upembuzi yakinifu ili mmoja wao awe mkewe. Hivyo jamaa aliamua kuwapa jaribio kwa kuwapa Tsh. 500,000/= kila mmoja huku akitaka kujua ni namna gani watazitumia.

Mwanamke wa kwanza alitumia pesa yote kununua vipodozi. Alitembelea duka la vipodozi na urembo akajikwatua sawa sawa! Alivyorudi kwa mchumba wake akamwambia,

"nimeamua kutumia pesa yote kwa ajili ya kujipamba ili nizidi kukupendeza

machoni pako na kukuvutia maana nakupenda sana."

Hakika yule mwanaume akapendezwa sana na mpenzi wake.

Mwanamke wa pili alinunua zawadi kwa ajili ya bwana wake. Alinunua simu janja mpya kwa ajili ya bwana wake, saa ya kisasa, nguo na viatu vizuri. Alivyofika kwa bwana wake alimwambia,

"pesa yote nimeitumia kununua hizi zawadi zako maana nina kupenda sana."

Jamaa akafarijika sana

Mwanamke wa tatu aliwekeza zile pesa kwenye soko la hisa na baada ya muda fulani alipata faida ya shilingi 2,000,000/=. Mwanamke yule aliamua kumrudishia bwana wake ile pesa aliyokuwa amepewa yaani laki 5 na pesa iliyokuwa imebakia alifungua akaunti ya pamoja na bwana wake. Kisha yule mwanamke akamwambia yule jamaa,

"nahitaji kuwekeza na kuhifadhi kesho yetu kwa sababu nakupenda sana."

Hakika yule mwanamke alimfurahisha sana jamaa.

Jamaa akatafakari sana yale ambayo yalikuwa yamefanywa na wale wanawake baada ya kupewa laki 5. Lakini mwisho wa siku jamaa aliamua kumwoa mwanamke mwenye makalio makubwa! Wanaume tutabakia kuwa wanaume tu
 
Namuunga Mkono! Kama Ameweza Kutoa Laki Tano Kwa Kila Mmoja Mambo Yake Si Mabaya Acha Atafune Kitu Roho Inapenda
 
Haaaaaaaaaaaaaaaa
Stori nzuri hii
China technology, speaks for itself
^^
 
Hadithi yako haijakaa sawa hapo. Yupi sasa kati ya hao watatu ndiye mwenye makalio makubwa?
 
Hadithi yako haijakaa sawa hapo. Yupi sasa kati ya hao watatu ndiye mwenye makalio makubwa?

Itakuwa ni yule wa kwanza aliyekwenda saloon kujipodoa; si unajua tena wanawake wenye masaburi makubwa kwa kujipodoa!!!
 
Mhhh! Hatari aisee hv makalio makubwa huwa ni kwanini yanatuteka mi mpaka sasa sielewi
 
hata mi ningechukua mwenye makalio makubwa.
 
Huyo mwanaume yukwapi anipe namie hiyo laki tano, nile kitimoto nipige zoezi nikuze kalio
 
safi sana.... pesa zinatafutwa ili zitumiwe.....lazima mwanamke awe na blink show......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…