Hamad Rashid ‘anunua ugomvi’ wa Lipumba, Seif

Hamad Rashid ‘anunua ugomvi’ wa Lipumba, Seif

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,302
Wakati mgogoro wa uongozi kati ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi ukishika kasi, Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed amesema mgogoro huo unakolezwa na Maalimu Seif kutokana na kung’ang’ania madaraka.

upload_2017-8-21_11-26-20.gif


Akizungumza kwenye madhimisho ya miaka mitano ya ADC yaliyofanyika kwenye Makao Makuu yake Buguruni, Hamad alisema hatua hiyo inasababishwa na kutanguliza maslahi binafsi.

Hamad alisema kiongozi mzuri ni yule anayeendena na maneno yake kwa wanachama na wananchi, ili kuweza kujenga chama kama taasisi siyo chama cha mtu mmoja.

Hamad badala ya kuzungumzia maadhimisho ya chama chake, alijikita zaidi kwenye mgogoro wa CUF.

Pia, alisema hawataki viongozi wanaokipaka matope chama chake kwa kukiita CCM B. Alisema sera yao ni kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu kwa wanachama wake, ili kupata muda wa kuendeleza demokrasia inayoleta mabadiliko.

“Katika chama chetu hatuna sera ya vurugu wala migogoro binafsi hatukubali hata kidogo, mtu kutuharibia chama chetu. Kiongozi huwezi kufanya kazi kwenye fitina,” alisema.

Alisema kiongozi yeyote hawezi kuongoza chama au wananchi iwapo kuna migogoro inayosababishwa na viongozi wachache.

“Chama chetu hatuwezi kumvumilia kiongozi muongo tunaamini uongozi unaweza kupatikana katika sehemu mbili za mabadiliko na uchanguzi, hatutaki kufanya mabaya yanayofanyika kwenye vyama vingine,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo alisema ADC siyo chama cha vurungu kutokana na wao kuamini maendeleo hayawezi kupatikana kwa maandamano,

Pia, Doyo alisema kitendo cha viongozi kushindwa kuelewana ndani ya chama, ni jambo ambalo linaleta picha mbaya na kurudisha nyuma maendeleo ya ujenzi wa demokrasia.

“Tuna uwezo wa kusameheana iwapo kumetokea mtafaruku, tunawataka wanachama wote kufanya hivyo katika matawi yao,” alisema Doyo.


Chanzo: Mwananchi
 
AWE MPATANISHI WOTE ANAFAHAMU; WOTE WALIMUUMIZA.
 
Hamadi Rashid aliweka price tag akanunulika...sasa anamgeuka swahiba wake ambae walikaa wote ndani kama miaka 5 hivi....wakisota na kutafakari juu ya upinzani na siasa za Tanzania Bara na Visiwani!! Kweli njaa mbaya sanaa!! Hata Weweee!!!
 
Hahahaha hao ni wanachama wa ADC mchana usiku wako kwa Lipumba mtondogoo ccm
 
Wakati mgogoro wa uongozi kati ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi ukishika kasi, Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed amesema mgogoro huo unakolezwa na Maalimu Seif kutokana na kung’ang’ania madaraka
Maneno haya angeyazungumzia Zanzibar yangeleta maana, sio Buguruni!!!!!
 
Naona wameamua kuongeza wataalamu wa kuendelea kupambana na Maalim Seif.
 
Back
Top Bottom