Halotel wameanza utapeli nao?

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,435
Reaction score
1,995
Hapo nyuma ukinunua kifurushi cha air time au internet walikuwa
wanakupa ujumbe kamili wa SMS kwamfano: "umenunua kifurushi cha internet airtime dakika kadha za mtandao kadha na sms kadhaa MB 500 kwa siku au week nk"
Lakini sasa hawakwambii details za kifurushi na muda wake. Na ghafla unaambiwa 'kifurushi chako kimeisha" na hii inaweza kuwa baada ya masaa au siku moja tu baada ya kununua kifurushi!
Ukipiga 100 kutaka kujua kuhusu kifurushi chao utasikia maelezo kibao yasiyohusu shida yako na anaweza kuyumbishwa siku nzima bila kuongea na mhudumu directly ili mradi ukate tamaa?
Halotel, rudisheni utaratibu wa kutupa ujumbe kamili wa manunuzi ya vifurushi husika kwa SMS kwa record ya mteja ili iwe rahisi kufuatilia pindi ikibidi.
 
Aisee katika hili labda ni kwako tuu, hawa wa vietnam wako makini sana aisee,nilikuwa wilaya ya Nsimbo/katavi miezi kadhaa iliyopita nikipofika vijiji vya ndani sana ukipita hivyi itenka, imilamate nk huko nilitegemea kukuta watu hawaba mawasiliano maana mimi line yangu ya tigo ilikata mawasiliano nilipotoka tuu pale mjini/mpanda,ajabu nilikuta mawasiliano wanayo na katika kila watu 10 bhas walikuwa halotel na 1 ni voda na hapakuwa na mtu alilaumu kuhusu huduma zao halotel na hata mimi ilibidi nisajili halotel(wana mawakala mpaka mapolini hawa jamaa) na tokea nisajili sijawahi kukutana na hilo jambo unalosema... jalibu kuwasiliana nao uwaeleze tatizo lako yawezekana SimCard yako ikawa na tatizo.
 
Karibu tena Mpanda sheikh!
 
Mpanda mji mzuri sana ila ukiwa nje yake watu wanakujaza maneno mengi sana ya kukufanya uuogope haswa kuhusu uchawi,Panapo uhai nitaludi huko mwezi wa nane nikitokea Congo Shekh wangu.
Hapa ndio tumezaliwa na kukulia! Kwenye mitandao watu wanakuza Sana Mambo! Na kuhusu uchawi , upo popote, Seema tu mijini wachawi wamebadili styles, badala ya kuwanga usik wao wanafanya "Model Uchawi"..[emoji2][emoji2], utaskia wajiita Manabii , Mitume, Mara sheikh Majini nk....

Karibu tena kiongoz!
 
Hawa jamaa namalizia kifurushi chao nawahama,nilikua nanunua kifurushi kupitia halopesa napata chachuo sasahivi wamekitoa,kunakifurushi cha ajabu unapata gb 15 kwa mwezi chaajabu kinalimit kilasiku utumie mb 500 zikifika hapo huduma inasitishwa mpaka kesho
 
Kwa kweli halotel wamekuwa wezi mpka wanaboa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…