Habari wana jamvi,sote tu wazima na pole kwa wale ambao wameamka hawako na afya njema.
Kama kichwa cha habari kinavyoonyesha hapo juu,mimi ni mtumiaji wa mtandao wa halotel. Na kila mara nikiweka vocha huwa napokea sms zilizoandikwa HALOWIN,wakiambatanisha na namba za bahati ambazo unatakiwa kutuma kwa namba fulani kisha ushinde.
Sasa naomba kuuliza,yupo mtumiaji yeyote ambae ashawahi kushinda chochote kuendana na sms hizo za halowin.??
Kwa maana nishakuwa mtumiaji wa mtandao huu kwa muda mrefu lakini sijawahi kusikia mtu akishinda chochote.
Kama hawashindi chochote,kwanini waendelee kutumia watu sms hizo??