Kanuni za kuendesha huduma za kifedha zinasemaje kuhusu ukadiriaji wa senti unaofanywa na huduma za pesa mtandao ?

Kanuni za kuendesha huduma za kifedha zinasemaje kuhusu ukadiriaji wa senti unaofanywa na huduma za pesa mtandao ?

Raskazimi

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
1,184
Reaction score
1,336
Kuna jambo nimeona kwenye kutumia huduma za fedha mtandao (Yas, kwa case yangu) likanitatiza. Wakati nikifanya malipo ya serikali kutumia app yao, sikuwa na namna ya kuingiza senti kuendana na nilichokua nalipia. Badala yake, mfumo ukafanya ukadiriaji wa juu (rounding up) na kunilazimu kulipia ziada. Licha ya hiyo, nikatumiwa ujumbe kutoka taasisi niliyokua nawalipa, kwamba wamepokea malipo yangu kwa kiasi kamili (hadi senti) na sio kile nilichokatwa kilichokadiriwa.

Ufanyaji kazi wa huu mfumo husababisha mara nyingine tunalipa gharama ambayo hazilingani na ankara kamili. Mfumo hu-“zungusha” senti ndogo ndogo, na matokeo yake ni kwamba mtumiaji hupoteza senti chache kila muamala.

Kwa mtu mmoja inaweza kuonekana ni kidogo tu, lakini je, ukifikiria mamilioni ya miamala kila siku — hizo senti zinaenda wapi? 🤔

Je, kampuni za mitandao zinarekodi kama faida ya ziada kwenye vitabu vyao vya mahesabu?

Au ni sehemu ya makusanyo ya serikali?

Na je, kuna uwazi wa kutosha kwa watumiaji kuhusu hili?

Ni haki kwa mtumiaji au inakubalika kwenye kanuni za mifumo ya fedha?
 
Back
Top Bottom