Halmashauri ya Mkuranga uozo mtupu

ding'ano

Senior Member
Joined
Feb 24, 2013
Posts
182
Reaction score
265
Nilitembelea halimashauri ya mkuranga wiki mbili zilizopita,

nikakuta zogo kubwa sana,kati ya walimu wapya na mkurugenzi pamoja na maofisa utumishi,walimu wanadai mishahara yao hawajalipwa kwa miezi miwili( tokea walipoti kazini).Kwa mshangao mkubwa nikamuuliza mwalimu mmoja wapo akanieleza kuwa hawajaingizwa katika payroll kwa mwezi April na mwezi May,ingawa Mkuu wa mkoa aliwatangazia mapema kabisa kuwa katika mkoa wake hakuna tatizo la mishahara wamejipanga vizuri na serikali haitaki madeni.

Lakini hata mimi nilishingazwa sana kwani nilimsikia na kumuona waziri Hawa Ghasia bungeni akijibu swali,akasema walimu wote wapya waliotimiza taratibu za ajira (zaidi alisisitiza vyeti vyao) kuwa wamepata mishahara yao bila kuchelewa.
Nikaona ngoja niingie ndani kujua kulikoni hivi ndivyo vitu nilivyo vigundua katika halimashauri hii,

1. Uwajibikaji katika halimashauri hii ni hamna,Mkurugenzi hawezi kabisa kusimamia idara zake,hajui taratibu za mishahara,amekiri mwenyewe kuwa hata yeye hajui kama payroll haijakamilika,nilikuwepo kipindi akitoa hayo majibu katika kikao na walimu waliopandwa na hasira.

2.Maafisa utumishi ndio tatizo,hawaprocess data mapema,kuna uwezekano hawajui computer sababu payroll ina andaliwa na kutumwa online,lakini wa hapa mkuranga walisafiri hadi Temeke halimashauri wakapiga posho wakidai wanaogopa usumbufu,lakini hawakuweza kuandaa hizo payroll.

3. Bado kuna mawazo mgando katika halimashauri zetu,watumishi wengi hapa halimashauri hawaoni kuwa ni tatizo kwa watumishi wapya kukosa mishahara,majibu yao kuwa "komputa inatema majina" na mfumo mzima wa payroll ni kama bahati nasibu.Lakini majibu ya wakuu wa idara za elimu ndo kichekesho kabisa kuwa wao walikaa kwa miezi zaidi ya kumi walikuwa hawajalipwa hivyo ni kawaida.

4.Kuna idara ya mishahara na Afisa utumishi kwa jina la Mwakyusa ni kijana lakini ni tatizo kubwa,wao ndio wanatakiwa waandae payroll lakini kuna uwezekano mkubwa hawana ujuzi wa komputa katika kuprocess data.Lakini mwakyusa anatuhumiwa na walimu kuwa ni kikwazo na aliwekwa na mkuu wa mkoa aliestaafu hivyo anaogopwaingawa hajui kazi yake.

5. Kuna uwezekano mkubwa sana walimu hawa wapya wakaendelea kukosa mishahara kwa miezi mingine zaidi kutokana kwa haya UTUMISHI.

1.Wao wanapokea payroll kutoka halimashauri na idara zote za serikali na wanafanya kazi hadi usiku na muda mwingine week end,tatazo ni kuwa inatakiwa maafisa utumishi wakishatuma data inatakiwa wabaki online kwa marekebisho flani flani tatizo mkuranga wakishatuma tu wanakuwa offliene na hawulizii hadi watakapo ona payroll imepelekwa kwao na kuona waajiliwa wapya na hapo mda unakuwa umeisha.

2. Idara ya ICT utumishi na wanafanya kazi hadi usiku na wanakesha siku zingine (zamu) hasa tarehe za kuandaa payroll ili kusiwe na tatizo la sever kuwa down na mishahara kuchelewa. Kwa mtazamo wao mishahara kuchelwa serikalini ni tatizo la idara ya mishahara na maafisa utumishi wa halimashauri husika.

Watumishi wengine wa halimashauri ya mkuranga pia wamebainisha kuwaMkuranga ni halimashauri mbaya labda kuliko zote,hasa katika usimamizi wa miradi mbali mbali,mfano barabara ya Kimanzichana Mkamba,licha ya kutengewa pesa kila mwaka lakini hatengenezwi kwa kiwango cha changarawe na imebakia kuwa kati ya barabara mbovu zaidi.

Naomba kuwasilisha
 
Siyo hapo mkuranga tu bali nchi mzima ni uoza mtupu
 
kuhusu harimashauri hapa nchini waziri awe kama mwendawazimu kuna madudu kuna uchafu hakuna madiwani wakurugenzi wenyeviti mameya wote ukoo wa panya
 
Si halmashauri tu, public services kwa ujumla wake imeoza.
 
The whole government system is dysfunctional!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…