Hali ya Uchumi

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
1,393
Reaction score
1,217
Wajameni naombeni mwenye ufahamu wa kina anijuze ni kwa nini uchumi wa zimbabwe uliporomoka mpaka akawa hawezi hata kutumia pesa yake kwa matumizi ya ndani ya nchi!!!!
 
Vikwazo vya wakubwa hii ilitokea baada ya rais Mugabe kuja na Sera ya kuwanyan'ganya masha wawekezaji wakubwa kwenye kilimo kwa kiswahili cha wapigania Uhuru wanawaita mabwanyenye .

Baada ya kuwatimua wengi walikimbilia nchi jirani haaa Africa kusini,malawi na n.k yale mashamba akawapa wazimbabwe ambao walishindwa kuyalima na wengine wakayauza au kuyakodisha hili aliwahi kukili hata yeye kuwa wazimbabwe ni wavivu sana

Mashamba haya yalikuwa na viwanda ndani settle agriculture economy viwanda navyo vikafa maana vilikosa Mali ghafi

Watu wakakosa kazi na kukimbilia nje ,serkal ikakosa kodi ikashindwa kujiendesha ,ikafilisika

Baada ya kufilisika na nchi za ulaya zikaiwekea vikwazo hasa vya kuuza bidhaa ghafi nje yakawa mapigo juu ya mapigo,

Zamani Zimbabwe ilikuwa ndio kinara wa uchumi bora kusini mwa jangwa LA sahara hata sisi tulinunua chakula kwao

Ukikaa sana madarakani unakuwa zuzu na mipango inakuishia na mazoea yanakujaa
 
unajua naogopa, are we in the right direction?!? nahofia yasijetukuta ya zimbabwe
 
Wajameni naombeni mwenye ufahamu wa kina anijuze ni kwa nini uchumi wa zimbabwe uliporomoka mpaka akawa hawezi hata kutumia pesa yake kwa matumizi ya ndani ya nchi!!!!

Walikuwa na Rais ambae alianzisha sera kama anazozi-implement jiwe wa kwetu.
 
Remote ya uchumi wa nchi za Kiafrika karibia zote imeshikwa na hao mnaowaita MABEBERU.(SO DON PLAY WITH MABEBERU)
Wajameni naombeni mwenye ufahamu wa kina anijuze ni kwa nini uchumi wa zimbabwe uliporomoka mpaka akawa hawezi hata kutumia pesa yake kwa matumizi ya ndani ya nchi!!!!
 
Hapo kwenye bold. Zimbabwe kama nchi haijawahi kuwekewa vikwazo vya aina yeyote isipokuwa nchi za magharibi ziliwawekea vikwazo Mugabe na washirika wake (vya kusafiri na kuzuia mali zao binafsi). Zimbabwe imeendelea kuuza bidhaa zake kama kawaida ila tatizo ilikuwa ni kushuka kwa uzalishaji.
 
Hapana hatuna MTU wa kutufikisha huko

Wewe endelea kujiaminisha hivyo. Ila ukweli ni kuwa jiwe tayari keshatufikisha huko
It is only a matter of time now kabla hatujawa Zimbabwe na/au Venezuela nyingine
 
We are not working in speculations
Wewe endelea kujiaminisha hivyo. Ila ukweli ni kuwa jiwe tayari keshatufikisha huko
It is only a matter of time now kabla hatujawa Zimbabwe na/au Venezuela nyingine
 
Aisee wewe unaishi wapi, hata mkataba wa Agoa alitupiwa virago
 
uzalishaji wetu unashuka au unapanda?!?
 
kama ni kweli napumua vizuri sasa, lakini bado nina wasiwasi kidogo,pamba hainunuliwi kwa nini?!?
Hivi...viwanda vya kuzalisha vitambaa tulivyonavyo havitoshi kununua pamba yote inayozalishwa na wakulima wetu?
 
Unapanda na kushuka ,tatizo hapa tz ni viwanda hata pamba unazosema hapa shida in viwanda
ninavyojua awamu hii imedhamiria kuibadili TZ iwe ya Viwanda,lakini kama tunataka viwanda kupitia PPP, je tutatoboa?!? maana nasikia wafanyabiashara hawaishi kulalamikia viwango vya kodi na pia sheria ngumu zinazotungwa kila kukicha, lakini pia uhakika wa sera zetu zinabadilika kila asubuhi, nilishtuka majuzi wakati bunge la bajeti likiendela nikamskia mbunge mmoja akisema transporters wengi wa nchi hii sasa hivi wanaagiza magari wanayapeleka Rwanda au Zambia wanayasajili huko kwa sababu mfumo wa kodi kule ni rafiki!. nilishtuka sana, nikakumbuka kipindi cha nyuma wafanyabiashaar pale tunduma walifunga maduka/biashara zao wakaenda kuzifungua nakonde(Zambia) tukasema wacha waende!!!. najiuliza sana haya maswali wajameni!!!
 
kwa hiyo hiyo pamba ya ziada tutamuuzia nani mabeberu wakiisusa?!?, nakumbuka korosho hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…