Hali halisi: Hali ya uchumi wa Tanzania ni tete, uchumi wadorora, sera mbovu zawa chanzo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
Vyakula.jpg

Kwa ufupi
Hali hiyo inaashiria kudorora kwa uchumi huku baadhi wakiihusisha na uwapo wa sera zisizo rafiki kwa ukuaji wa uchumi.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Hali si nzuri katika sekta mbalimbali baada ya baadhi ya biashara kufungwa, kampuni kupunguza wafanyakazi na bidhaa kupanda bei, imeelezwa.

Hali hiyo inaashiria kudorora kwa uchumi huku baadhi wakiihusisha na uwapo wa sera zisizo rafiki kwa ukuaji wa uchumi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwenye baadhi ya masoko hapa nchini umebaini kuwa bidhaa mbalimbali zimepanda bei yakiwamo maharage ambayo yamepanda kutoka Sh1, 800 hadi kati ya Sh2, 700 na 3,000 kwa kilo.

Pia, sukari imepanda kutoka bei elekezi iliyotolewa na Serikali ya Sh1, 800 hadi Sh2,500, mchele kutoka Sh1,200 hadi 2,600 kwa kilo.

Unga wa sembe nao umepanda kutoka Sh1, 200 hadi Sh 2,000. Bidhaa nyingine zilizopanda ni mboga za majani ambapo fungu la mchicha, chainizi, tembele limepanda kutoka Sh200 hadi Sh400 na Sh500.

Hali hiyo inasadifiwa na ripoti za Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) zinazobainisha kuwa kasi ya mfumuko wa bei imekuwa ikiongezeka mwezi hadi mwezi kutoka asilimia 4.8 Novemba mwaka jana hadi asilimia 6.4 kwa mwaka unaoishia Machi mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai amesema kampuni hiyo imepunguza wafanyakazi kwa asilimia nane na kusimamisha ajira zote zilizokuwa zimeidhinishwa mwaka 2016/2017.

TDL ambayo ni kampuni tanzu ya Tanzania Breweries Limited (TBL) nayo mapema Machi 27 mwaka huu ilitangaza kupunguza wafanyakazi wake wasiozidi 50 ili kukabiliana na hali ya kiuchumi.
 
Mdororo utazidi kuwa mkubwa hasa kwa sisi wajasiria mali wadogo, kuna kundi LA matapeli limeibuka mitaani linajiita TRA Hawa kazi yao ni kuibia wafanyabiashara wenye kutumia risiti za TIN number, Hawa wanatake advantage ya risiti za machine kuwatisha watu nakuomba rushwa, ukienda TRA wanakuambia kama makadirio yako yanafikia million 14 uchukue machine ya EDF machine. Swali Je wenye makadirio ya milioni 13 kurudi chini nani anawasemea? Sisi wajasiria mali wadogo tukifunga biashara zetu kwa uhujumu HUU lawama zitarudi kwa MAMLAKA HUSIKA kwani matendo na matamko wanayotoa hawayafanyii utafiti Karla.
Ukiuza TOA risiti iwe ya machine au ya Mkono ulazima uwe na TIN number na unalipa, kauli kama hiyo ingeisaidia serikali kukusanya mapato tofauti na sasa hofu Kila kona, TANZANIA YANGU NAKUPENDA MAMA.
 
Yaani kwa Rais huyu, watanzania tusitegemee kwenda mbele kiuchumi isipokuwa tutarajie kurudi nyuma. Mzunguko wa fedha ni mdogo lakini mfumuko wa bei unazidi kupanda. Haya ni maajabu.
 
Mambo haya hayaongelewi sana, watu wako na petty issues. Yani tunapenda porojo kweli kuliko mambo ya msingi.
 
Sera mbovu zawa chanzo? Hapana sera mbovu na usimamizi mbovu wa sera husika zimekua chanzo miaka yote.
Hatuna dira na viongozi hawajifunzi kwa makosa wanayofanya kila siku.
 
Hizi ndio issue critical kabisa tunapaswa kujadili, hali imekuwa tete, mafuta ya kupikia yamepanda toka elfu 26 hadi elfu 38 kwa lita 10, kuna tatizo tena kubwa sana either kwenye utozaji kodi au treatments kwa wawekezaji Sio nzuri ndio maana kuna mfumuko mkubwa sana kwenye bei za bidhaa muhimu kabisa, kuna haja ya kupaza sauti kuhusu hali hii.
 
Ulichoandika ni mavi ya nguruwe na wewe pia ni nguruwe mkuu.
Endelea kutumikia Bwana zako Hapa kwa ujira wa senti.
Sisi tunatumia mnvua hizi za nadra kwa ufanisi.
Endelea kubrush viatu jukwaani
Unatumia mvua kutengeneza nini? Acha utoto na fikra potofu. Unaambiwa mzunguko wa hela hakuna, na mfumuko wa bei unapaa, baada ya kuja na hoja unakuja na ushuzi mmaake!! Hivi hizo Chinese, ua Tembele, mchicha ndio zitalete ongezeko la mzunguko, au haujui hatuko kwenye zama za ujima, ambazo ilikuwa bidhaa kwa bidhaa acha upoyoyo.
 
Vyakula.jpg

Kwa ufupi
Hali hiyo inaashiria kudorora kwa uchumi huku baadhi wakiihusisha na uwapo wa sera zisizo rafiki kwa ukuaji wa uchumi.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Hali si nzuri katika sekta mbalimbali baada ya baadhi ya biashara kufungwa, kampuni kupunguza wafanyakazi na bidhaa kupanda bei, imeelezwa.

Hali hiyo inaashiria kudorora kwa uchumi huku baadhi wakiihusisha na uwapo wa sera zisizo rafiki kwa ukuaji wa uchumi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwenye baadhi ya masoko hapa nchini umebaini kuwa bidhaa mbalimbali zimepanda bei yakiwamo maharage ambayo yamepanda kutoka Sh1, 800 hadi kati ya Sh2, 700 na 3,000 kwa kilo.

Pia, sukari imepanda kutoka bei elekezi iliyotolewa na Serikali ya Sh1, 800 hadi Sh2,500, mchele kutoka Sh1,200 hadi 2,600 kwa kilo.

Unga wa sembe nao umepanda kutoka Sh1, 200 hadi Sh 2,000. Bidhaa nyingine zilizopanda ni mboga za majani ambapo fungu la mchicha, chainizi, tembele limepanda kutoka Sh200 hadi Sh400 na Sh500.

Hali hiyo inasadifiwa na ripoti za Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) zinazobainisha kuwa kasi ya mfumuko wa bei imekuwa ikiongezeka mwezi hadi mwezi kutoka asilimia 4.8 Novemba mwaka jana hadi asilimia 6.4 kwa mwaka unaoishia Machi mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai amesema kampuni hiyo imepunguza wafanyakazi kwa asilimia nane na kusimamisha ajira zote zilizokuwa zimeidhinishwa mwaka 2016/2017.

TDL ambayo ni kampuni tanzu ya Tanzania Breweries Limited (TBL) nayo mapema Machi 27 mwaka huu ilitangaza kupunguza wafanyakazi wake wasiozidi 50 ili kukabiliana na hali ya kiuchumi.
Sera zetu siyo shirikishi ndiyo maana Malengo hayafikiwi
 
Tanzania ya viwanda bila kuimarisha kilimo ni kujidanganya tena ni ujinga kufikiria hilo.
 
Mi Hata simuelewi huyu kipara sa anakusanya hela ili afanyie nn!!! Ajengee viwanda!!!! Hapo amebugi Na njaa zikianza kazi hazifanyiki viwandani watu wapa nywea
 
Back
Top Bottom