Hakuna wajibu wa mtu wa tatu katika suala la Kashmir, India inasisitiza

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
INDIA imeshikilia msimamo hakuna jukumu la mtu wa tatu katika suala la Kashmir


Kauli hiyo imetolewa na S.Jainshankar, Waziri wa mambo ya nje (India) alipokuwa akijibu maoni ya Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardi na waziri wenzanke kutoka Ujerumani Annalena Baerblock katika Mkutano wa pamoja na vyombo vya habari uliofanyika Berlin Ijumaa.

Katika mkutano huo ,Jaishankar alisema India ilikataa wito wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan na Ujerumani kwa kuihusisha Umoja wa Mataifa kutafuta suluhu ya suala la Kashmir na akasema kwamba badala yake msisitizo unapaswa kuwekwa kwenye kukabiliana na suala linalohusiana na Magaidi wa Pakistan ambao wamezilenga Jammu na Kashmir kwa muda mrefu.

Wakati Baerbock alibainisha "ishara chanya" kama vile ushirikiano kati ya Pakistan na India kusambaza chakula kwa Afghanistan, mawaziri wote wa mambo ya nje walizungumza juu ya jukumu la Umoja wa Mataifa katika kutatua suala la Kashmir.

Majibu ya upande wa India pia yalirudisha nyuma ubishi wa Baerbock kwamba Ujerumani "ina jukumu na wajibu kuhusiana na hali ya Kashmir".

India imeshikilia kwamba Kashmir ni suala la nchi mbili pamoja na Pakistan na hakuna nafasi ya mtu wa tatu.

“Wanachama wote makini na waadilifu wa jumuiya ya kimataifa wana jukumu na wajibu wa kupinga ugaidi wa kimataifa, hasa wa asili ya mipaka,” Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Arindam Bagchi alisema akijibu maoni kuhusu J&K na mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani na Pakistan.

“Umoja wa jimbo la India wa Jammu na Kashmir zimekuwa zikikabiliana na Kampeni za ugaidi kwa miongo kadhaa. Hii inaendelea hadi sasa….. “alisema.

“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na FATF [Kikosi kazi cha kitengo Fedha] bado wanafuatilia magaidi wenye makao yake Pakistani waliohusika katika mashambulizi ya kutisha ya 26/11,” Bagchi alisema, akizungumzia mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa mjini Mumbai na timu ya Magaidi ya Lashkar-e-Taiba. (LeT)kutoka Pakistan. “Wakati mataifa hayatambui hatari kama hizo, ama kwa sababu ya ubinafsi au kutojali, hudhoofisha sababu ya amani, sio kuiendeleza. Pia wanafanya udhalimu kubwa kwa waathiriwa wa ugaidi,” aliongeza.

Katika hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa waandishi wa habari, Bhutto Zardari alidai kuwa

“ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu" unafanywa katika J&K, na hii inahatarisha amani na utulivu wa kikanda. Alisema amani katika Asia Kusini haitawezekana bila” suluhisho la amani ya mzozo wa Jammu na Kashmir kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Bhutto Zardari alisema Pakistan iliendelea kuibua suala la Kashmir, haswa baada ya matukio ya Agosti 2019 - wakati India iliondoa hadhi maalum ya Jammu na Kashmir - na kwamba sheria ya kimataifa inapaswa kutumika kila mahali.

“Tunatumai kuona siku ambayo Umoja wa Mataifa utachukua jukumu linalofaa kumaliza mzozo huu wa muda mrefu ili tuweze sio tu kuwa na amani ndani ya eneo letu, lakini tuweze kuimarisha maeneo ya ushirikiano,” aliongeza.
 
Back
Top Bottom