singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
TAARIFA juu ya kuwepo kwa uhaba wa sukari nchini, si jambo la kufurahiwa.Ukosefu huu, kwa namna yoyote ile, basi lazima utakuwa na mazingira ya wazi ya hujuma ambayo inafanywa na wafanya biashara wa sukari nchini.
Nimejiuliza kwa nini sukari iadimike au ipande bei siku chache tu baada ya Rais Dk John Magufuli kupiga marufuku uingizaji holela sukari kutoka nje ya nchi. Itakumbukwa Februari 18 mwaka huu wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya wadau walioshiriki kwenye kampeni zake, kuelekea kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, Rais Magufuli alisema amedhamiria kwa dhati kufufua viwanda vya ndani na kwa kuanzia amepiga marufuku kiongozi yeyote wa serikali, kutoa kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi zaidi yake. Leo tunasikia kuwa sukari imeadimika mtaani na kama ipo, basi inauzwa kwa bei ya juu.
Hakika, hili halikubaliki na mamlaka husika hazina budi kuchukua hatua juu ya hili. Inakuwaje mzigo uwepo wa kutosha, halafu leo uadimike? Lazima kuna wafanyabiashara ambao wanataka kuitingisha serikali katika hili la uagizaji sukari nje ya nchi. Juzi Bodi ya Sukari Tanzania iliwataka wafanyabiashara kutopandisha bei ya sukari, huku ikiwasisitiza kuheshimu bei elekezi iliyopo.
Aidha, ilisema inazo taarifa kuhusu wafanyabiashara wakubwa, ambao kwa sababu wanazozijua, wameamua kuficha sukari ili hatimaye wapandishe bei, kitendo ambacho iliahidi itachukua hatua dhidi yao. Mimi nadhani huu ni wakati muafaka kwa Bodi ya Sukari, kuwataja wafanyabiashara hao wanaotaka kuwatesa wananchi kwa kuficha sukari au kuiuza ghali, ili tu waruhusiwe kuagiza sukari kama walivyozoea.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Simwanza alisema sukari inatakiwa kuuzwa Sh 1,800 katika jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani. Simwanza alisema upatikanaji wa sukari nchini ni wa kuridhisha na ipo akiba ya kutosheleza nchi nzima. Alisema pamoja na baadhi ya viwanda kusimamisha uzalishaji wa sukari kutokana na msimu kuisha, hali ya sukari nchini ni nzuri na ipo akiba zaidi ya tani 62,000.
Nadhani Bodi ya Sukari kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na maofisa wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wapitie maghala yote ya waliopewa leseni za kuingiza sukari nchini, kufanya msako na ikibainika kuwa kuna watu wamezuia uuzaji wa sukari wakamatwe na wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
Lakini wafanyabiashara hawa, watabainika kupitia wafanyabiashara wa sukari ambao huchukua mzigo kwao. Kama kuna mfanyabiashara ambaye ataenda sehemu na kukosa sukari, ilhali akiamini ghala hilo lina sukari ya kutosha, afike mamlaka husika na kutoa taarifa.
Bodi ya Sukari Tanzania kwa kushirikiana na Kamati Ufundi ya Uagizaji wa Sukari nchini na sekretarieti za mikoa, ifanye kazi kwa umakini ya kufuatilia kwa karibu kiasi cha sukari kilichopo nchini na mwenendo wa bei na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wafanyabiashara, watakaoharibu mwenendo wa soko.
Katika kuonesha kuwa habari za ukosefu wa sukari nchini si jambo la kufurahisha, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisemka juzi kuwa mfanyabiashara yeyote wa sukari aliyeficha sukari katika ghala lake, atalifungia ghala hilo.
Waziri Mwijage aliuthibitishia umma kuwa hakuna uhaba wa sukari nchini na kuwataka wafanyabiashara walio na leseni za kuingiza na kuuza bidhaa hiyo, kutoificha. Mwijage alitaka watu wenye taarifa juu ya mfanyabiashara aliyefungia sukari katika ghala lake, ampelekee ili afunge ghala husika mara moja.
Hivyo kama alivyosema Waziri Mwijage kuwa kwa sasa serikali inajikita zaidi katika uanzishaji wa viwanda vya sukari na kuongeza ajira na si kuagiza sukari kutoka nje. Kwa mujibu wa waziri huyo, ofisi yake inafanya mazungumzo na mwekezaji, anayetaka kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha sukari Kigoma.
Hili nalo ni la kuungwa mkono. Pia, ipo haja kwa wawekezaji waliopo sasa wa viwanda vya Sukari vya Kilombero, Mtibwa, TPC Moshi na Kagera, kuongeza uwekezaji wao na kuimarisha uzalishaji, kwani serikali iliyopo madarakani imedhamiria kuona viwanda vya ndani, vinazalisha na kuwa na soko la uhakika ndani.