Ni wapi kuna uthibitisho kuwa hizi sayari zitafikia mwisho wake..Maandiko yote yanazungumzia uhai ndio utakao kuwa na Mwisho. Kwa Mfano Uislamu unasema "Kila Nafsi itaonja Umauti". Hapa Kinachotajwa ni nafsi ambayo ina uhai na Dunia na Sayari zingine si sehemu ya vitu au viumbe vyenye nafsi. Kwa taafsiri ya Kawaida ni kwamba Dunia (Earth) na Sayari zingine ni za Milele.
Na mm nakufundisha kupitia hio hio Qur'an kua dunia na vilivyomo vina mwisho wake
{ إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ }
[Surah Al-Infiṭār: 1]
Mbingu itapo chanika,
{ وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ }
[Surah Al-Infiṭār: 2]
Na nyota zitapo tawanyika,
{ وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ }
[Surah Al-Infiṭār:
Na bahari zitakapo pasuliwa,
{ وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ }
[Surah Al-Infiṭār: 4]
Na makaburi yatapo fukuliwa,
{ عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ }
[Surah Al-Infiṭār: 5]
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
Hizi ni baadhi ya aya tu zinazoonyesha mwisho wa dunia