Hakuna mwanamke malaya, wala hakuna mwanaume bwege!
Mwanamke ambaye umekua ukimfwatilia kwa miezi 12 sasa ndiyo ametoka kulala na mwanaume ambaye wamekutana siku tatu tu zilizopita.
Mwanamke ambaye ulimtongoza na kumpata ndani ya wiki moja kuna jamaa mwaka wa pili sasa anafwatilia na ashaliwa pesa nyingi tu za kutosha wakati wewe hata hela ya bajaji hukutoa.
Kama ameona kitu kwako, akakupenda na kushindwa kujizuia ukampata kirahisi acha kupiga kelele na kumuita MALAYA.
Lakini kwa wanawake, huyo jamaa ambaye mmekutana juzi tu lakini kashakununulia iPhone, hajawahi kumtumia X wake hata vocha
Kama umebahatika akakupenda na kuchanganyikiwa kwa muda mfupi juu yako, acha kujidnaganya kwamba jamaa ni BWEGE ukaona hajitambui ni wa kuchuna tu!
Mwanamke akikupa mwili wake na kuchanganyikiwa juu yako haimaanishi kuwa ni MALAYA, hivyo hivyo mwanaume akiamua kukuheshimu na kukutunza haimaanishi kuwa ni BWEGE
.. Ni bora kupendwa na mtu sahihi maana vitu vinadanganya unaweza ona umefika kumbe unacheleweshwa na hivyo vitu unavyopewa..