Wanajamvi:
Kwa mtazamo wangu naona Maalim seif ni mnafiki tu kuhusu asemayo kwamba huwa hajibizani katika vyombo vya habari kwani kumjibu Hamad Rashid kwa waandishi wa habari atuambie ilikuwa nini?
Maalim Seif anatufanya mafala kabisa – kaita mkutano wa waandishi na hatujui iwapo aliwaita akiwa kama nani – Katibu Mkuu wa CUF au Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar?
Maana siku hizi amepata mwanya wa kuwa popo – yuko huku au kule, hata katika ziara zake – haziwekwi wazi. Kwa mfano wiki iliyopita alipokwenda Kilwa alikwenda kama nani?
Na kama jana aliongea kama Makamo wa Rais wa serikali ya Umoja Zanzibar kueleza mafanikio ya umoja huo basi Seif angekataa kata kata kuwajibu waandishi kuzungumzia yanayojiri katika chama hicho.
Maalim Seif hapo katumia ujanja tu -- eti kaita waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya serikali ya Umoja, kumbe hasa alipanga kumjibu Hamad Rashid kiaina, maana alipanga waandishi kumuuliza kuhusu hilo.
Hata kuzungumzia mafanikio ya serikali ya umoja yalikuwa ilikuwa geresha kwani hilo nijambo tayari Dr Shein alilizungumzia mwezi uliopita).