Hakuna kitu kinaniboa kama ukienda kuomba mkopo wanakwambia ukae kwenye vikundi

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Wakuu nimekua nikifuatilia Mkopo ambao hausiani na Salaried worker ujitegemee kwa ajili ya Biashara sasa tatizo ni Kukaa Kwenye Kikundi

Mimi Taangu nikiwa mdogo si mtu wa Makundi hata Kusoma mi nilikua napiga msuli peke yangu.

Kuna Compulsory groups chuoni lazima Ujiunge kutafuta Course work nao niliwasumbua sana.

Sasa Leo ninavyoenda bank halafu uniambie nikae Kwenye Kikundi for me Ni Most boring thing wakuu nimegundua ni vema Uka save kidogo kidogo mwenyewe utatoboa. Banks zina milolongo mingi na waoga kupata hasara.
 
Mkuu, sio wewe tu hata mimi ni mmoja wapo ambae sifagilii kabisa huo utaratibu mbovuu wa utoaji wa mikopo.

Kuna mama mmoja nilimskia juzi anaongelea kuhusu zile hela(50ml) za serikali ambazo zimetengewa kwa ajiri ya kuwawezesha vijana wanaohitaji mikopo, alifafanua sababu za wao kutoa mikopo kimakundi makundi. Sababu kuu hasa wanasema vijana hawana dhamana na dhamana pekee ni yeye kuwa na wenzake yaani wale wenzake anaochukua nao mkopo ndio dhamana.

Sasa kama ikitokea ukakosa watu wakukuunga mkono wazo lako la kijasirimali hili mtengeneze kikundi ina maana hauna chance ya kupata mkopo. Na kikawaida ni nadra sana watu watano wote mkutane mkiwa mna mawazo sawa na hata kama mkiridhia kulifanyia kazi wazo la mmoja hamuwezi mkalifanya kwa passion sababu ya mgongano wa mindsets, na mwisho wa siku output itakuwa ni zero tu.

Kiukweli mazingira ya kupata mkopo bongo hapa karibia sehemu zote ni magumu sana. Bora kuuza mali zako tu huku ukiwa na mikakati kabambe.
 
Unajua mfumo wa uchumi wa nchi yetu ni kama wote ni wakimbizi,nilienda Banki nikaambiwa lazima mtengeneze kikundi ili bra bra,nilisema moyoni kwa mfumo huu tutashikwa masiko na hakuna atakaefanikiwa nje ya ufisadi
 
Wakuu nimekua nikifuatilia Mkopo ambao hausiani na Salaried worker ujitegemee kwa ajili ya Biashara sasa tatizo ni Kukaa Kwenye Kikundi

Mimi Taangu nikiwa mdogo si mtu wa Makundi hata Kusoma mi nilikua napiga msuli peke yangu.

Kuna Compulsory groups chuoni lazima Ujiunge kutafuta Course work nao niliwasumbua sana.

Sasa Leo ninavyoenda bank halafu uniambie nikae Kwenye Kikundi for me Ni Most boring thing wakuu nimegundua ni vema Uka save kidogo kidogo mwenyewe utatoboa. Banks zina milolongo mingi na waoga kupata hasara.
Kuna sababu . Mambo ya fedha ni taaluma. Wana vigezo vyao vya kutoa mikopo. Benki huwa haitoi mkopo kwa mtu mmoja mmoja ambaye ndo anaanza biashara. Kama hutaki kuwekwa kwenye vikundi anza mwenyewe kwa mtaji wako, kisha hakikisha unafanya mahesabu na hela unapeleka benki kwa muda fulani ndo uwaibukie uone kama watakuambia ukae kwenye kikundi. Tusikimbilie tu kulaumu muda mwingine ni sisi hatuna maarifa ya kujua ni lini unapaswa ukope mkopo wa biashara. Mkopo wa binafsi wa kupitia mshahara huo watakupa tu maana wanajua uamue kuutumbua au kuuharibu bado watapata tu makato yao kwenye mshahara wako. Unakuta mtu ana wazo tu anaenda benki kuomba mkopo. Hivi benki wangekuwa wanatoa mikopo kwa watu wenye ideas tu si wangefulia maana Tanzania nzima kila mtu an idea. Ishu ni execution ya ile idea ndo si kitu lelemama.
 
Kaz/dhamira kuu ya wao kuhitaji dhamana ni nini?
 
Dhamira kuu ni kuhakikisha itapokuwa umeshindwa kulipa mkopo wana uhakika watatumia njia zingine ku recover hela yao. Lakini hawawezi kumpa mtu ambaye ana onyesha dalili kubwa kabisa atashindwa kulipa mkopo hata kama huyo mtu anayo dhamana. Na moja ya watu ambao si wazuri kuwakopesha ni wale ambao wanaanza biashara for the first time. Probability ya kufail ni zaidi ya silimia 90. Benki hawawezi kujiingiza mkenge kwenye risk za namna hiyo eti kisa una dhamana. Kuwa na dhamana pekee si guarantee ya kupata mkopo ambayo ni ya biashara. Tatizo wakisema tu wasiangalie uwezo wako wa kurudisha mkopo basi watabaki na kibarua cha kuuza collateral ambayo ni kazi nyingine. Wanataka waone biashara yako inavyorun na dhamana ni added advantage. Hizo collateral zinasumbua sana kuuza. Kuna mikopo watu walikopa wameshindwa kulipa, benki zinajaribu kuuza hizo collateral lakini wanakosa wateja wanaofikia bei ya kuweza kuu recover mkopo. Na ukumbuke mkopo una riba, kwa hiyo ukiweka hata collateral ambayo ni 120% ya mkopo unaoomba still inaweza isiweze fidia ya riba. Ikitokea kuna mikopo mingi ya aina hiyo (ambayo kuna defaulters wengi) basi benki inaweza ikaishiwa liquid asset na ikashindwa kujiendesha. Non-liquid asset ni mzigo kuigeuza kuwa liquid. Na benki wanahitaji cash kuendelea kufanya day to day transactions. Mfano umeona BOT wamefunga benki huko Mbinga ni sababu hiyo hiyo ya kuwa na defaultals wengi..

Tukija kwa vijana, changamoto nyingine pia unaweza kuta hawana hata hiyo collateral na wanataka mkopo. It is more feasible kusaidia wao as kikundi rather than mmoja mmoja. Wakiwa kikundi kitu cha kwanza wana mtaji wa human resource kwa wingi wao. Kwa hiyo kama ni shamba la nyanya ni rahisi kuli manage mkiwa kikundi kuliko ikiwa una deal na one individual ambaye hana experience. As kikundi inategmewa kutawa na kubadilishana mawazo kwa kiasi kikubwa kusaidia uboreshaji wa mradi. Na tunatofautiana strengths. Mtawalaumu sana benki kwa hili lakini lakini ndo policy wanazozitumia na kwa nchi zetu hizi kuna uncertainties nyingi mno. Moja ya changamoto ni uaminifu. Watu wamepewa mikopo ambapo hawakuchangia chochote wala kuweka dhamana yeyote, miradi ikiwashinda wanakimbia. Lakini kama nyumba yako imewekwa rehani huwezi kuukimbia mradi ukianza kupata changamoto.
 
Unajua mfumo wa uchumi wa nchi yetu ni kama wote ni wakimbizi,nilienda Banki nikaambiwa lazima mtengeneze kikundi ili bra bra,nilisema moyoni kwa mfumo huu tutashikwa masiko na hakuna atakaefanikiwa nje ya ufisadi
Bank gani hiyo? Huna biashara, dhamana je? Mbona mimi sijakutana na hizo habari za vikundi na wamenipa 10m?
 
Back
Top Bottom