Hakuna changamoto isiyoweza kuwa fursa.

Hakuna changamoto isiyoweza kuwa fursa.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,305
Nitajikita kwenye hoja,
Maisha yanachangamoto nyingi mno ambazo zinakatisha tamaa,kuna wakati unaweza kudhani Mungu amekusahau kabisa pale unapoona wengine wanafanikiwa na wewe upo tu.
Jambo la msingi siyo kulalamika sana kwani kila mtu kwa hakika ana magumu yake,tajiri halali usingizi anahofia wezi,kodi,kufilisika nk.
Maskini halali usingizi anajiuliza kesho atakula nini,atatibiwa vipi akiugua nk,wanandoa hawana amani wanagombana kila siku,wivu,michepuko nk,wapweke nao wanakesha kuomba wapate wenza lakini bado.Unapomhadithia mtu matatizo yako jua na yeye anayake.
Lakufanya angalia fursa iliyomo kwenye hiyo changamoto na uitumie vizuri,kumbuka duniani hakuna ridhiko la kudumu la nafsi,maisha ni mahangaiko tu na kwa kuwa kesho huijui unaendelea kuwa na matumaini tu,ila sasa usiache kujitahidi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poa sana mkuu...Thanks
 
Back
Top Bottom