Hakuna cha kukuzuia kufanikiwa

Hakuna cha kukuzuia kufanikiwa

The Guitarist

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2015
Posts
3,428
Reaction score
4,774
UDHAIFU WAKO NDIYO MAFANIKIO YAKO.

Miaka mingi kabla ya kuwa maarufu katika ulimwengu huu kwa kutumia uwezo wake wa kuburudisha na kuchekesha umati wa watu kama muhusika mkuu katika mfululizo wa filamu mbalimbali za vichekesho huku akijiita Mr Bean. Filamu hizi ndizo zilizomfanya akawa maarufu duniani huku akitajwa kama mwigizaji maarufu zaidi nchini Uingereza.

Bwana Rowan Atkinson alikuwa bado ni kijana mdogo tu kule mitaa ya Newcastle nchini Uingereza mwishoni mwa miaka ya 1950s mpaka mwanzoni mwa 1960s. Kutokana na ucheshi wake watu waliokuwa wakiishi mtaa mmoja na huyu mwamba walijikuta wakipata burudani kutoka kwa kijana huyo na wengi walimtabiria makubwa mbeleni
Alizaliwa January 06 mwaka 1955 katika familia ya kiwango cha kati yaani kama ni fedha basi walikuwa na zakuwatosha kubadilisha mboga tu na sio kuishi kifahari. Huyu jamaa ni msomi wa shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Oxford akibobea katika maswala ya uinjinia wa umeme.
Pamoja na hayo yote Rowan Atkinson almaarufu Mr Bean alikuwa na matamanio ya kuwa muigizaji nguli duniani hivyo kipindi alipokuwa chuo alijiingiza katika vikundi vya uigizaji na akafanikiwa kushiriki matamasha madogo madogo kama yale ya Edinburg Festivals Tringes
Hiyo ikawa kama hamasa ya yeye kutamani kuigiza katika kiwango cha juu zaidi na hapo ndipo matatizo yalipoanzia kwani kila alipojaribu kutafuta nafasi ya kujiunga na vipindi vya runinga alikataliwa sababu kuu ikiwa ni tatizo lake la KIGUGUMIZI japokua alijitahidi kutafuta nafasi zaidi na zaidi aliambulia jibu moja tu HUFAI.
Hapo ndipo akatambua kuwa jambo analopenda hawezi kulifanikisha kwasababu ya udhaifu alio nao. Siku moja akiwa katika mawazo mazito likamjia wazo kwamba kulingana na tatizo lake basi kuna uhusika anaoweza kuutumia ambao hautahitaji yeye kuongea zaidi ya kutenda alijikuta akipata furaha na nguvu ya ajabu. Akarejea tena kuomba nafasi na kuwasilisha wazo lake huku akisema “Nimegundua kwamba ninapoigiza kwa vitendo bila kuzungumza tatizo langu hutoweka”

Safari hii WALIMPUUZA kwa kumuambia hana sura yenye mvuto wala mwili uliojengeka kuvutia watazamaji. Hakika jibu hili lilihitimisha ndoto zake za kupata nafasi ya kuigiza. Hapo akajisemea mwenyewe huwenda sio kila ndoto ni lazima zitimie labda zingine tunaota ili kujifurahisha tu.
Siku zikasogea jamaa akawaza na kuwazua ndipo alipogundua kuwa mtaji wa maskini ni nguvu alizonazo na kama usipofanya wewe hakuna atakaye kufanyia. Na mwisho akaja na wazo la kuanzisha kipindi chake mwenyewe akishirikiana na marafiki zake hapo ndipo akaja na kipindi cha Mr Bean kama muujiza awamu ya kwanza ikawa na mafanikio makubwa hali iliyopelekea kutengenezwa kwa mfululizo wa filamu za Mr Bean na baadae Johnny English kwa mafanikio makubwa akatunukiwa tuzo mbalimbali akavuna na utajiri unaokadiriwa kuwa $130 milioni Huku akimiliki nyumba na magari ya kifahari.

Mwaka 2001 akiwa katika ziara ya mapumziko nchini Kenya ndani ya ndege anayomiliki alikuwa pamoja na familia yake mke wake Sunetra Santry aliyemuoa miaka ya 1980s pamoja na watoto wao Ben na Lily rubani alipoteza fahamu ikamlazimu Mr Bean kukamata uhusika wa kuiendesha bila kuwa na uzoefu wala ujuzi wowote mpaka pale rubani aliporudiwa na fahamu kisha kutua salama katika uwanja Wa ndege wa Wilson Jijini Nairobi. Alipoulizwa aliwezaje kuendesha ndege akajibu alipata maelekezo kupitia sala alizokua akisali katika wakati huo wa hatari.
FUNDISHO
Mafanikio hayahitaji uwe na sura nzuri Pamoja na umbo linalovutia bali yanahitaji kujitoa kwa moyo na kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka. Kwakua hakuna binadamu aliyekamilika tujifunze kutumia udhaifu tulionao kama chachu ya kusonga mbele zaidi na zaidi mafanikio yapo kwa wale wanaoamini.

El Artista
 
Attachments

  • f26d73bbfcb6118d5c860948ad084a81.jpg
    f26d73bbfcb6118d5c860948ad084a81.jpg
    58.5 KB · Views: 36
Duniani bwana! Kuna watu maisha kwao rahisi kama tebo ya kumi,ila wengine sisi maisha yametukunjia ngumi.
 
Duniani bwana! Kuna watu maisha kwao rahisi kama tebo ya kumi,ila wengine sisi maisha yametukunjia ngumi.
Hatuna budi kupambana mkuu lazima tufungue na sisi boksi letu la mafanikio siku moja
 
Tom & Jerry,Charlie Chaplin & Mr Bean 😂.. nikiwa bored hawajawahi kuniangusha..
 
Mafanikio hayahitaji uwe na sura nzuri Pamoja na umbo linalovutia bali yanahitaji kujitoa kwa moyo na kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka. Kwakua hakuna binadamu aliyekamilika tujifunze kutumia udhaifu tulionao kama chachu ya kusonga mbele zaidi na zaidi mafanikio yapo kwa wale wanaoamini.
asante
mwanzo niliiona ndefu lakini nikakumbuka mimi pia ni mtu ninayeandika vitu virefu humu hivyo nikasoma kwa kujilazimisha lakini nikushukuru nimepata kitu kikubwa ambacho kinaweza kusaidia jamii kwa ulichokiandika.
 
Karibu mkuu Tuifanye JF kuwa sehemu ya kujifunza kwa mara nyingine tena
 
Karibu mkuu Tuifanye JF kuwa sehemu ya kujifunza kwa mara nyingine tena
mimi nafundisha sana lakini kinachonikera siku hizi maisha yangu hayaendi na ninachowaelekeza watu.
wao wanafanikiwa halafu miminaunga unga hapa ndio sielewi kabisa! nafikiri na mimi nahitaji kuelekezwa
 
Nilichojifunza kwenye maisha anayekutazama ndiye anayejua maendeleo yako ila wewe binafsi hutagundua kwa urahisi
 
Nilichojifunza kwenye maisha anayekutazama ndiye anayejua maendeleo yako ila wewe binafsi hutagundua kwa urahisi
inaweza kuwa kweli lakini wengi hawako tayari kukueleza udhaifu wako na nini ufanye uchomoke kwa kuwa kuna wakati unapoteza kabisa uelekeo.
 
inaweza kuwa kweli lakini wengi hawako tayari kukueleza udhaifu wako na nini ufanye uchomoke kwa kuwa kuna wakati unapoteza kabisa uelekeo.
Mara nyingi sisi wenyewe hatupendi kuambiwa ukweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom