Hakuna aijuaye kesho

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
25,307
Reaction score
40,940
Habari wanaJF,
Hujafa hujaumbika, sisi binadamu ukiwa mzima unashukuru MUNGU.

Nina jirani yangu,mpangaji mwenzangu,tumekuwa pamoja kama mwaka hivi na urafiki wetu nikwasababu tunashare interest moja,wote tunacheza mpira wa miguu. Kama kawaida asubuhi huwa tunawahi uwanjani tunapasha then 1230 kila mtu anawahi kwenye mishe zake.

Kama tufanyavyo kila siku,leo pia tuliwahi,lakini wakati mwenzangu anaenda kwenye mishe zake amegongwa na gari na kuvunjika miguu yote miwili,daah hili jambo limenisikitisha sana baada ya kumwona mchana MOI,kwakweli inasikitisha sana mtu aliyekuwa mzima saiz amepata ulemavu wa kudumu.

Kwakweli sisi binadamu thamani yetu ni ndogo sana jamani, nikama karatasi tu japokuwa ukiwa mzima unaweza jiona we ndokila kitu,binafsi nimepata mshituko sana pale nilipo muona,machozi yametoka involuntarily kwa namna nilivyomuona nacho mtu ambaye asubuhi tulikuwa tukipasiana mpira na kuona hana miguu tena.

Nimejifunza jambo kuwa sisi binadamu hatuna thamani kabisa,japo ukiwa mzima unajiona ww ndo kila kitu.

Tenda mema,mweshimu kila mtu,acha ujeuri na kiburi maana hujui kesho yako
 
POLE SANA MKUU KWA YALIYOMFIKA JIRANI YAKO
KUMBUKA HUJAFA HUJAUMBIKA PIA PUNGUZA WOGA MAJANGA YAPO TU NA TUMEUMBIWA BINADAMU
Inapasa ushukuru kwa yote na kusonga mbele
 
POLE SANA MKUU KWA YALIYOMFIKA JIRANI YAKO
KUMBUKA HUJAFA HUJAUMBIKA PIA PUNGUZA WOGA MAJANGA YAPO TU NA TUMEUMBIWA BINADAMU
Inapasa ushukuru kwa yote na kusonga mbele
Asante mkuu
 
Pole yake sana, inaumiza na inaweza kuwa ngumu kuikubali lkn hatuna budi kumshukuru Mungu Kwa kila jambo ,kuna wanaopata ajali wanakufa kbs , bora yake yeye kabaki na uhai. Ila kweli hujafa hujaumbika lolote laweza kutokea. Mungu amponye mgonjwa
Ameen,yaani acha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…