Hakimu Eliasi Bingasira ni Jipu kwa Haki ya Wananchi wa Muleba

KAMUGUNGA

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
238
269
Wakati Rais Magufuli akipambana na viongozi waliojilimbizia mali na wanaotumia madaraka vibaya (Maarufu kama utumbuaji Majipu), wananchi wa Muleba hasa kata za Mubunda, Karambi, Kyebitembe, Burungura, Kasharunga na nyingine za jirani wamekuwa wakiteseka na udhalimu, ubabe, upindishwaji wa sheria na matumizi mabaya ya nafasi yake kama Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyamilanda iliyoko kata Kyebitembe na Mahakama ya Mwanzo ya Mubunda ambapo anazihudumia kama Hakimu.

Hakimu huyu amekuwa akiamua mambo yake hata kama anajua maamuzi yake yanaenda kinyume na taratibu za utoaji haki na mbaya zaidi matendo hayo anayafanya kupitia chombo ambacho waliowengi wanakikimbilia ili kupata haki.

1. Boss huyu anaweka watu ndani pasipo kutoa dhamana hata kama mtu anatuhumiwa kumuangalia mwenzake kwa jicho baya. Wakati dhamana ni haki ya kila raia, boss huyu amekuwa akikatalia dhamana za watu kwa sababu zake anazozijua.

2. Boss huyu anatumiwa vibaya na wenye pesa zao kunyonga/kudhulumu haki kwa watu wasio na uwezo. Ukishitakiwa na mtu mwenye pesa zake anakuamria kabisa ni kwa siku ngapi atakuweka ndani maana anajua amri hiyo atampa boss huyo wa kugandamiza haki za watu.

3. Matajiri wanaomtumia boss huyu wamekuwa wakifungua kesi kwenye mahakama anazohudumia pasipo kujali hata umbali wa anakotoka mshitakiwa na pasipo kujali kuwa hata mshitaki na mshitakiwa wako karibu na mahakama nyingine ambayo yeye si hakimu pale.

Wito wangu, wananchi wa Kata nilizozitaja wanatoa kilio kwa Wakubwa wa Hakimu huyu kuhakikisha anakanywa na kuchukuliwa hatua stahiki ili wananchi waweze kuishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom