Hakika Rais Magufuli ni kiboko yao, hebu jikumbushe hili

Mpunilevel

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
3,140
1,871
Baada ya serikali yake kupiga marufuku utolewaji wa vibari holela vya sukari nchini, na kuelekeza kwamba vibari vitatolewa na watu watatu, yaani yeye Rais, makamu wake na waziri mkuu tu, ili kulinda viwanda vya ndani, upotoshaji mkubwa ulianza kuenezwa na walanguzi na wakwepa kodi wakubwa wa sukari dhidi ya juhudi hii ya mheshimiwa Rais.

Lengo kubwa likiwa ni kupima ubavu na msimamo wa serikali Ya awamu ya Tano.Ilitumika propaganda kubwa sana, kwa kutumia media mbali mbali, baadhi kuponda maamuzi haya ya mheshimiwa Rais.

Lakini msimamo wa serikali ulibaki pale pale.
Sasa naweza Sema kundi lile limeshindwa na wamekua wapole, yaani kimya kabisa.Kupata uhakika wa hili ni kwamba kwenye media, issue ya sukari zimeachana nayo kabisa, heading za media si sukari tena.

Hongera Rais Magufuli kwa msimamo ulioonyesha kwenye sakata hili.
Na hakika nchi utaifikisha mahali ambapo kila mtanzania atafurahia matunda ya nchi hii na si kikundi cha wachache.
 
Nimeikuta leo kwa Mkuu wa Mkoa bei sh. 1800 nikaiona rahisi nikaenda dukani kununua ya sh. 3000.
 
Uzuri wa watanzania ni wasahaulifu.Shida zetu zinatufanya tusiwe wafuatiliaji wa jambo likitokea,mfano: Ishu za sukari,makontena,Masamaki na wenzake,Dowans,Milioni 7 kwa dakika 1,Lugumi nk.
 
Baada ya serikali yake kupiga marufuku utolewaji wa vibari holela vya sukari nchini, na kuelekeza kwamba vibari vitatolewa na watu watatu, yaani yeye Rais, makamu wake na waziri mkuu tu, ili kulinda viwanda vya ndani, upotoshaji mkubwa ulianza kuenezwa na walanguzi na wakwepa kodi wakubwa wa sukari dhidi ya juhudi hii ya mheshimiwa Rais.
Lengo kubwa likiwa ni kupima ubavu na msimamo wa serikali Ya awamu ya Tano.
Ilitumika propaganda kubwa sana, kwa kutumia media mbali mbali, baadhi kuponda maamuzi haya ya mheshimiwa Rais.

Lakini msimamo wa serikali ulibaki pale pale.
Sasa naweza Sema kundi lile limeshindwa na wamekua wapole, yaani kimya kabisa.
Kupata uhakika wa hili ni kwamba kwenye media, issue ya sukari zimeachana nayo kabisa, heading za media si sukari tena.
Hongera Rais Magufuli kwa msimamo ulioonyesha kwenye sakata hili.
Na hakika nchi utaifikisha mahali ambapo kila mtanzania atafurahia matunda ya nchi hii na si kikundi cha wachache.
Ni bora kikundi cha wachache kifaidike ili sukari iwe bei cheee. Sio tufaidike wote alafu bei juu
 
Back
Top Bottom