Amalrik TZ
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 341
- 303
Hatimaye siku ya kupiga kura imewadia. Taifa linaenda kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais siku ya jumatano tarehe 28 Oktoba.
“Siku ya uchaguzi inavyozidi kukaribia ndio matumaini ya kuwa huru yanavyozidi kuwa makubwa”. Hayo ni maneno ya Sheikh Ponda Issa Ponda aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii (Twitter) tarehe 21 Oktoba.
Maandiko Matakatifu kutoka kitabu cha Methali 14:34 yanasema “haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote”
Je, ndugu mtanzania mwenzangu unadhani Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kusimamia haki kwa vyama vyote siku ya kupiga kura na kutangaza matokeo?
Binafsi sina imani kabisa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Wote tunajua kwamba watendaji wa kuu wa tume wamechaguliwa na mgombea Urais wa CCM akitumia nafasi yake ya Urais kwa mujibu wa Katiba.
Ukiachilia mbali kwamba watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Wakurugenzi wa Wilaya ni makada wazuri wa Chama Cha Mapinduzi, wameamua kuikanyaga Katiba ya nchi hadharani na kupigania vyema maslahi ya chama chao katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Nadhani kila mmoja wetu anaikumbuka vyema kauli ya Rais Magufuli aliposema kwamba “haiwezekani mkurugenzi nikuteue mimi gari nikuwekee mafuta mimi posho nikulipe mimi alafu usimame kumtangaza mpinzania kuwa kashinda”.
Maneno haya ambayo rais aliyatoa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi watanzania tulio wengi hatukuyaweka akilini, lakini watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Wakurugenzi waliyaelewa na kuyashika vyema na sasa wanayafanyia kazi ipasavyo huku mioyo yao ikiogopa sana kumuangusha Mtukufu Rais.
Wote tumeona NEC inavyofanya kila namna kuwabana na kuwadhuia wapinzani. CHADEMA na ACT Wazalendo wamekuwa ndiyo wahanga wakubwa wa vitimbwi hivi kila siku.
CHADEMA imeingia kwenye uchaguzi huu huku zaidi ya wagombea wake zaidi ya 600 wa ngazi ya Udiwani na Ubunge wakitenguliwa kugombea kwa sababu zisizo na mashiko yoyote huku wagombea wa CCM wakipita bila kupingwa.
Haishangazi kwenye orodha ya waliopita bila kupingwa akiwemo January Makamba ambaye anatoka jimbo la Bumbuli, Nape Nnauye jimbo la Mtama pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jimbo la Ruangwa.
Hii inaonyesha dhahiri kuwa CCM na NEC ushirika wao ni kama ndoa ya Kikristo usio na talaka na kwenye uchaguzi huu wanajambo lao wanalotaka kulifanya.
Kampeni za mwaka huu hazijawa na usawa wala haki kwa vyama vyote vya kisiasa. Vyama vya upinzani hasa CHADEMA na ACT wazalendo vimebanwa sana mbavu kwenye kampeni za mwaka huu.
Wagombea Urais wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu na Maalim Seif wa ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar wote walipunguzwa spidi kwa kufungiwaa kufanya kampeni kwa vipindi tofauti.
Madhila hayo yalianza kumkumbaTundu Lissu pale ambapo Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) yalipomfungia kutokufanya kampeni kwa siku saba kwa maadai ambayo yalikuwa hayana hoja ndani yake.
Maalim Seif naye alikionja kikombe cha hukumu kutoka kwa Pilato pale ambao Kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilipotangaza kumfungia kutokufanya kampeni kwa siku tano kuanzia Oktoba 16-20 2020 kwa madai kwamba aliwahamasisha wananchi waende wakapige kura 27 Oktoba.
Ukiachilia mbali vihoja na hayo madhila ambayo wapinzani wanakabiliana nayo katika kipindi hiki cha kampeni kuna jambo ambalo NEC imewashtua wengi. NEC inasema kwema “Mpiga kura anaweza kuomba karatasi nyingine akikosea au kubadili maamuzi hayo ni maneno ambayo aliyasema ofisa wa NEC, Flora Mkama”
Kama hiyo haitoshi “Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema kukosewa na majina, picha au jinsia kwa baadhi ya wapigakura kwenye daftari la wapigakura kumechangiwa na wapigakura wenyewe kushindwa kufanya uhakiki wa taarifa zao wakati kazi hiyo ilipofanyanika” maneno hayo yaliripotiwa na @Darmpya Blog kwenye ukarasa wao wa kijamii (Twitter).
Utaratibu huu unatia mashaka mengi kwani unatoa nafasi kwa kufanyika hujuma kwa vyama vya upinzani siku ya kupiga kura na kukipa chama tawala faida kubwa.
Ngugu yangu mtanzania taifa letu kwa sasa haliongozwi kwa haki na usawa kwa watu wote. Uonevu kwa vyama vya upinzani umekuwa mwingi sana kwenye mchakato mnzima wa uchaguzi mwaka huu 2020.
Tukumbuke kwamba uhuru wa kweli wa watu kutoka kwa wenye dola hauwezi kuja kirahisi bila ya wananchi kusimama kidete na kuupigania kwa moyo wote.
Tarehe 28 Oktoba twendeni tukafanye mabadiliko ya kweli kwenye sanduku la kura.
Itoshe kusema kwamba uhuru tutaupate pale wote tutakapo kwenda kupiga kura.