Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Inanikera, inanisikitisha na kunihuzunisha. Tuliokuwa watetezi wa rasilimali za nchi hii leo hii tumegeuka kuwa makuwadi wa mabepari na mabaka uchumi wa nchi hii. Hatujielewi na hatujitambui ama tumelamba chochote kitu kutoka kwa ACACIA.
Leo hii mtu na akili zake eti anasimama kupinga uamuzi wa Rais kuhusu makontena ya mchanga wa dhahabu. Kuna sababu ya kupima kiwango cha uzalendo wetu. Katika hili mwanasheria wangu, Tundu Lisu, Mwenyekiti wangu, Freeman Mbowe na wote mnaopingana na uamuzi wa Serikali juu ya mchanga wa dhahabu kwa kweli mmeifedhehesha CHADEMA yetu. Sijui wapi tunaelekea. Tangu Lowasa aje CHADEMA tumekuwa na akili za ajabu ajabu haijapata kutokea.
Wakati tunamfukuza Zitto Kabwe kwa kashfa ya za usaliti licha ya tishio la kutaka kutushtaki hatukusikiliza cha mtu. Tuliendelea na msimamo wetu kwa kuwa tuliamini ni kwa manufaa ya CHADEMA na Zitto akang'oka. Mbowe unajua na Lisu unajua. Leo hii eti tunajitutumua na kuinyooshea kidole Serikali pale inapolinda rasilimali zetu. Tumechanganyikiwa.
Niwaambie ninyi CCM, sisi CHADEMA tuna mipango mibaya sana kwa nchi hii. Tunataka mshindwe ili tuwe na kick 2020. Tunatamani hata leo hii serikali ianguke. Mkitusikiliza mtapotea vibaya sana. Huu ni mkakati tuliouandaa na umekamilika. Tutapinga kila jema la CCM na Serikali yake ili mkitusikiliza tunyanyue kwapa zetu kushangilia. Shauri yenu.