Hafeli mtu hapa: Kocha kaamua kutanua magoli baada ya wachezaji wake kushindwa kufunga

Ruzibiza

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
563
123
sitaki kuamini Tz imefirisika kiasi cha kushindwa kujua ni jinsi gani ya kuboresha elimu ili kuwa na wahitimu wenye ushindani (competitive) na badala yake inaamua kuweka mazingira yatakayo mfanya mwanafunzi iwe vigumu kufeli...sasa napata majibu ya migogoro iliyopo ya EAC, huwezi tegemea kufaidika na jumuiya kama una watu vilaza maana hawataweza kushindana na wenzao katika soko la pamoja la ajira...solution pekee ni kujifungia tufanye ya kwetu kibongo bongo huku tukidanganyana "tuna raslimali nyingi wenzetu wanatuonea wivu"
Je,utajifungia kwa muda gani au mara ngapi? ndiyo unawezafanikiwa kujificha waganda,wakenya,warundi nk wasikuone...vipi utajificha wapi wakija WTO?

"Tanua magoli wachezaji wetu kila mmoja afunge hat trick"....
 
Wameamua kumtoa golkeeper ili watu wafunge magoli kadiri wawezavyo, sasa tutakuja kuona mbona hata uwanjani wachezaji wabovu wapo yani yeye hata kutoa pasi hawezi, Ataweza kufunga??
 
waTZ!!!! MBONA KILA KITU MNALALAMIKA? KIPINDI KILE WALIONGEZA F HADI 34 MKALIA SANA, SASA WAMESHUSHA MNALIA TENA, MBONA HAMUELEWEKI?
 
Kwanza mitihani inasahihiswa kwa computer. Walimu hawafai hahahaaaa hesabu za kuchagua hana kuhangaika kukokotoa unyanyua shingo uka copy na kupest kidigitali zaidi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Someni vizuri taarifa ya Katibu mkuu wa wizara. Ipo wazi kabisa kwamba div IV imekua na makundi mawili yaani wenye wastani wa D na wale wa E ambao awali walikua kundi moja. Na divisheni mpya yaani divisheni V ni kwa wale walio na wastani wa F yaani masomo mengi wamescore between 0-19%. Kwa maoni yangu ukisoma vizuri huo mfumo ambao unachukua 60% ya Final exams na 15% form 2 final exam, 5% ya kila muhula wa kidato cha 3 na 5% na practical ni mfumo bora zaidi utakaoboresha ufaulu uwe sahihi zaidi na kupata wanafunzi wenye sifa kama ukisimamiwa vizuri. Kuhusu kufeli au kufaulu kwa wanafunzi kumbukeni kwamba kufeli kunaanzia nyumbani kwa mzazi, muda mwingi wa mwanafunzi kutumika kwenye mambo yasiyo ya kitaaluma kama kuangalia TV,simu, computer na aina mbali mbali za michezo na kazi za nyumbani,pili ni shuleni kwa aina ya walimu walio na maslahi duni, waliowengi ambao awali hawakufaulu vizuri, serikali inayowalipa maslahi duni walimu, mazingira magumu ya kazi na uhaba wa vitabu . Hili la div V wala si suala la kuzungumzia sabau zaidi linaondoa dhana mbaya kwa mtoto anayeangukia huko kujiona hafai tena kwa kila kitu na ni mbumbumbu mzungu wa reli wakati wapo wanaopata zero kwa bahati mbaya lakini kumbe wangeweza kufaulu vizuri hata kwa kiwango cha div 3
 
Wizara ya Elimu ina naibu Waziri kihiyo. Kwa kumbukumbu na heshima kwa mtaalam wetu Mulugo napendekeza wizara ya elimu iitwe, Wizara ya Mulugo na Vituko. Ukweli Mulugo utakumbukwa kwa mengi brother, keep it up!!!
 
Poa Mulugo - ni mambo ya elimu ya kuunga unga kama alivyosema Master pale mjengoni. Keep it up - ikiwezekana hata wanaopata 0% wahesabiwe ni wa division one. Hapo utapata vilaza wa kukusapoti
 
USINAMBIE HAYO MANENO MANENO ebu fuata hiyo link..Alama mpya sekondari

Back
Top Bottom