Hapo zamani kidogo kulikuepo mfalme ambae aliongoza nchi fulani, Mfalme huyo aliongoza kwa weledi mkubwa huku akiwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi wake.
Siku moja mfale huyo aliwaamuru walinzi wake waweke mawe barabarani na kisha akajificha pamoja na walinzi wake kwenye kichaka pembeni kidogo ili aweze kuona ni nani atayatoa mawe yale.
Baadhi ya marafiki na wajakazi wa mfalme walipopita eneo lile walilizunguka (walipita pembeni) kisha wakaenda zao huku wengi wakiishia kulalamika utawala wa mfalme huyu kwa kutohakikisha barabara ni safi huku kati yao hakuna aliethubutu kuyaondoa mawe yale.
Baada ya siku kadhaa alipita kijana mmoja akiwa anaonekana mchafu mikononi akiwa anavuta tololi likiwa limejaa uchafu, Kijana yule alipofika tu aliweka mzigo wake chini kisha kuanza kusukuma mawe yale pembezoni mwa barabara, Baada ya kutumia nguvu kwa muda na maumivu mengi alifanikiwa kuyatoa mawe yale na kuamua kurudi kuchukua mzigo wake aendelee na safari.
Alipofika kuinua mzigo wake aligundua kuna pochi mahali alipoyatoa mawe yale na ndipo alipoamua kuichukua na kuangalia ndani, Hakuamini macho yake kwani pochi ile ilikua imejaa mawe ya dhahabu na almasi huku kikaratasi kidogo chenye mwandiko wa mfalme kikiandikwa "Nimeweka pochi hii kwa ajili ya yule atakaeyatoa mawe yaliyopo barabarani na hii itakua zawadi yake" ujumbe ule ulimfanya kijana yule aondoka mwenye furaha.
HADITHI HII INATUFUNDISHA NINI:
Kila gumu tunalokutana nalo ni alama njema ya mazuri yaliyo mbele yetu, na kwa wale tunaopenda kulalamikia mifumo tunajipotezea nafasi nyingi ambazo zingetupeleka kutimiza ndoto zetu.
#festongadaya