chiqutitta
JF-Expert Member
- Nov 13, 2015
- 1,160
- 3,124
SEHEMU YA MWISHO YA SEASON HII YA KWANZA
. Kwakua mimi nilikua najua jinsi waislamu wanavyozika, wao niliwazika kwa kutanguliza na dua. Booker na Philipo niliwazika na kuwaombea walazwe mahala pema.
Nilitengeneza misalaba kama nionavyo wanavyoweka mbele ya makaburi yao. Haikuwa kazi rahisi kufnya hivyo. Ila msukumo wa kibinaadamu na mapenzi yangu juu yao ndio vilikua vitu vilivyonifanya nikubali kupoteza nguvu zangu na kuwazika kama binaadamu wa kawaida na hali ile ya mwanzo ya kutupwa. Machozi yangu yalinifanya niumwe kichwa huku sura yangu ikiwa haitamaniki kwa jinsi macho yalivyovimba kutoaka na kulia kwa muda mrefu. Hata sauti ilikata kutokana na kuitumia kama kipoozeo cha machungu yaliyokuwa moyoni wangu. Niliikumbuka sana siku niliyowapa ofa rafiki zangu kabla ya kuanza safari yetu ya kuchukua samaki tuliowatega siku mbili zilizopita kabla ya siku hiyo. Nililia zaidi nilipomkumbuka rafiki yangu Booker mzee wa totoz. Alikua mtu wa stori sana na mpenda utani. Hata kama nikiwa na hasira kiasi gani, basi nilimtumia Booker kama kuburudisho changu cha kuniondoa stress. Hakika ilikua zaidi ya uchungu ambao sikuwahi kuupata toka siku ya kuzaliwa kwangu.
Baada ya mazishi ya rafiki zangu. Nilirudi na kukaa huku siku hiyo nikiwa nimepoteza kabisa furaha. Usiku wa siku hiyo. Mbiu ililia na watu wote walikusanyika katika uwanja wa matukio. Sikua na hata hamu ya kwenda kushuhudia kitu kilichofanya watu waitwe.
Malikia alinifuata na kuniambia kuwa ni muhimu nihudhurie. Nilijikusanya kivivu na kuelekea kwenye huo uwanja wa matukio na kukaa kwenye nafasi yangu huku malikia akiwa karibu kabisa na mimi.
Kwakua mimi ndio nilikua mtu wa mwisho kufika, nilikuta watu wameshajipanga na kutulia tulii kusikiliza muito huo.
“mleteni”
Hiyo ilikua kauli ya malikia baada ya kusimama haikipita hata dakika moja. Nilimuona mpenzi wangu Shenaiza akiburuzwa na kuletwa pale tulipo huku wakiwa wamemfunga minyororo.
Roho iliniuma kwakua nilishaanza kumpenda kuikweli kabisa. Ila sikua na jinsi zaidi ya kukubali kutulia tu ili nione ni kitu gani walichokua wanataka kumfanya Shenaiza wangu.
“huyu ni jemedari msaliti. Na wasaliti adhabu yao ni kifo hadharani. Nadhani kila mtu anafahamu kuwa jemedari Shenaiza alijaribu kumtorosha mfalme. Na ametenda kosa hilo makusudi kabisa huku akiwa anafahamu kuwa kufanya hivyo ni makosa makubwa sana kwenye ardhi hii.” Aliongea malikia na watu wote wakaa na kutulia ili kuona nini malikia ataamua kufanya baada ya kuainisha makosa yake hadharani.
“adhabu yake,.. nitamuua mimi mwenyewe kwa mikono yagu kwa kukitenganisha kiungo kimoja baada ya kingine.” Aliongea malikia kauli ambayo ilinishtua sana. Sikutaka kushuhudia tukio lile kutokea mbele ya macho yangu. Niliamua kufumba macho yangu ili nisishuhudie kifo cha kikatili cha mpenzi wangu.
“aaaaaaaaaaaaaaaaaaagh!!!”
Ukelele mkubwa sana ulisikika na kunifanya nifumbue macho kutokana na kuisikia ile sauti. Nilipigwa na bumbuwazi baada ya kuona aliyechinjwa ni malikia na si mpenzi wangu.
Wakati nashangaa shangaa, alinifuata nilipo na kunishika mkono. Tulianza kukimbia huku tukiacha watu wakiwa hawaamini kitu kilichotokea. Tulipofika umbali kama wa mita mia hivi, alisimama na kunikumbatia.
Baada ya hapo alianza kupaa angani huku akiwa na kutua kwenye lile pango. Tuliingia ndani na kuchukua vito vingi tulivyoweza kubeba na kutoka navyo nje.
Tulipofika baharini, tulikuta boti imepaki. Tulifurahi sana na kuingia kwenye boti hiyo. Tulifurahi sana tulipokua njiani. Tuli fanikiwa kufika kwenye bandari ya salama tukiwa salama usalimini.
***************************
Baada ya Hijja kuelezea kilichomtokea akiwa huko kisiwani, waandishi wa habari walibaki wametulia kama wamemwagiwa maji ya baridi. Kila mmoja alijikuta anampigia makofi na kumpongeza. Pia walimpongeza sana Shenaiza ambaye wakati huo alikua anacheka tu wakati mume wake akielezea kisa cha ukweli kilichomtokea akiwa huko kisiwani.
“nina swali la nyongeza mfalme Hijja.” Aliongea muandishi wa habari na kuwafanya wote wacheke mle ndani.
“uliza” aliruhusu Hijja na kumsikiliza mtu huyo.
“tulipata taarifa za kwenda kisiwani humo kwa mara ya pili japokua hukukaa sana.. mambo yapo vipi huko ulipokwenda?” aliuliza yule muandishi wa habari na kufanya aungwe mkono na waandishi wote wa habari waliokuwemo kwenye ukumbi huo.
“safari yangu ya pili ilikua ni kwenda kumuoa huyu bibie nyumbani kwao… kama mtahitaji habari hii kwa undani naomba mnitafute siku nyingine. Maana ukweli kwa sasa nimechoka sana.” Aliongea Hijja na waandishi wa habari wakakubali kupanga siku nyingine kwa ajili ya kupata stori hiyo wakati Hijja alipokwenda kuoa.
Baada ya dunia kupata ukweli juu ya mtu mwengine aliyekuja kuvunja rekodi ya mwanasayansi wa zamani Mac Donald, jina la Hijja liliandikwa kwenye vitabu vya kihistoria vya watu waliofanya maajabu kwenye dunia hii.
********MWISHO************
MWISHO WA RIWAYA HII NDIO MWANZO WA HADITHI NYINGINE… TUPATE MAPUMZIKO YA SIKU MBILI TATU ILI TUJIPANGE TENA KATIKA THE GIRLS IN ISLND SEASON II
Kwa maoni, ushuri, na kama kuna mtu nimemkwaza kwa namna moja au nyingine, namuomba radhi na awe huru kuniambia kupitia in box na mimi nitajirekebisha. Maana na mimi ni binaadamu na kukosea nimeumbiwa.
Usikose season nyingine next time