Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
HADITHI: Surprise ya Aibu
SEHEMU: 01
MTUNZI: DR AMBE
SIMU: 0713646500
Mazoea kwa kweli ni ugonjwa pamoja na kuwa na kila kitu katika maisha yangu hakuna nilicho kikosa. Nilikuwa na maisha mazuri watoto wangu wote wana maisha mazuri, lakini tabia zangu mbaya ambazo nilishindwa kuziacha ndizo zilizonifikisha hapa. Nilitamani dunia ipasuke kwani ilikuwa aibu ya mwaka mbele ya watoto wangu. Pamoja na kufanya za Siri lakini leo nimeumbuka mbele ya wanangu, nasema Mimi tena basi.
****
Simu iliendelea kulia Martin aliacha gazeti na kuichua, alipoangalia namba zilikuwa za mdogo wake anayeishi Canada aliipokea
"Haloo Edna lete story mdogo wangu."
"Shikamoo kaka."
"Marahaba, za Otawa?"
"Nzuri, sijui za huko Bongo?"
"Za huku safi, mbona kimya?"
"Si mimi au ninyi, nyie ndiyo uliye nisusa."
"Tuachane na hayo siku zote upigapo simu huwa una jipya."
"Ni kweli kaka"
"Ehe lete story."
"Kaka ni hivi jana nimempigia asimu mama lakini sikumpata nilitaka nimualifu yeye kwanza ndio niwataalifu nyinyi kaka zangu, vipi na Moses hajambo?"
"Mmh! Yule kaka yako mtu wa safari si mnajua kazi za serikali kila kukicha anazunguruka na mheshimiwa."
"Basi ina maana hata kwa mama hamjaenda muda mrefu?"
"Ni kweli, kwa upande wangu nina mwezi sasa."
"Aah! Jamani mama yetu ni mmoja inatakiwa tuwe tunamtembelea hasa nyinyi uliye karibu."
"Ni kweli, shughuli zimetubana lakini nilipanga wiki ijayo niende kwa bi mkubwa."
"Sasa ni hivi mimi nilikuwa nipo njiani kuja huko."
"He! Mbona ghafla kuna nini?"
"Aah! Kaka kuja nyumbani mpaka pawepo na kitu, kwa mama yetu ni muhimu hata kila siku kumuona. Nampenda sana mama yangu na nikiolewa naondoka naye."
"Yaani wewe ndiye mwenye mapenzi kuliko watoto wake wote?"
"Ninyi mpo karibu lakini mwezi unapita bila kumtembelea bi mkubwa."
"Edna tuachane na hayo ulikuwa unasemaje mdogo wangu?"
"Ni hivi kaka yangu, huku nimepata mchumba ambaye yupo tayari kufunga ndoa na mimi."
"Hongera, ni raia wa nchi gani?"
"Ni Mkanada mwenye asili ya Afrika."
"Mmh! Haya, sasa ulikuwa unasemaje?"
"Tumekubaliana mimi nitangulie kuwajulisha kisha yeye atafuata, sijui kwa hilo mnasemaje kaka yangu?"
"Siyo baya sasa unakuja lini?"
"Wiki ijayo."
"Itakuwa vizuri maana nina imani tutakutana kwa mama."
"Basi mjulishe na kaka Moses."
"Basi unganisha mawasiliano ya watu watatu ili tulizungumze kwa pamoja."
Edna aliunganmisha mawasiliano ya watu watatu na kuanza kuzungumza na kaka yake Moses ambaye anamfuata kwa mara ya pili ambaye alikuwa katibu mkuu ofisi ya Rais.
"Haloo kaka."
"Ooh! Bibie za Canada?"
"Nzuri tu kaka, shikamoo”
“Marahaba, naona leo umenikumbuka mdogo wangu.”
“Nitafanya nini na ninyi mmenisusa.”
“Hapana mdogo wangu kazi za serikali nimenibana ila nitatulia tu.”
“Haya kaka, za misafara maana nasikia kila alipo rais na wewe upo."
"Nitafanyaje na mimi nimeichagua hii kazi."
"Vipi upo wapi kwa sasa?"
"Nipo Denmark."
"Mmh!" Edna aliguna.
"Mbona una guna ulikuwa unasemaje?"
Edna anamueleza yote kama aliyomueleza kaka yake mkubwa Martin na jinsi walivyo panga kukutana kwa mama yao wiki ijayo.
"Kumbe ni hivyo, hakijaharibika kitu mdogo wangu, wiki ijayo nitakuwa Tanzania na nitakuwa na mapumziko marefu ya wiki tatu kwa hiyo safari ya kwenda kwa mama tutakuwa pamoja."
"Wawooo, itakuwa bonge la Surprise," Edna alifurahishwa na maneno ya kaka yake.
"Sasa ni hivi tusimjulishe mama tumzukie bila yeye kujua akiamka asubuhi atukute mlangoni kwake hiyo unasemaje?"
"Si mchezo ni Bonge la Surprise," Edna aliunga mkono.
"Kwa hiyo wote tukutane kwa bwana mkubwa Arusha siku moja kabla ya kwenda kwa mama."
Walikubaliana wote watatu ambao ni watoto wa mama mmoja lakini hawakubahatika kumuona baba yao. Baada ya kuelezwa na mama yao kuwa baba yao alimkimbia na kumuachia watoto. Mama yao ambaye aliwalea watoto wake na kufaniwa kuwasomesha iliyo ya juu, ambao baada ya masomo kila mmoja alipata kazi nzuri.
Historia ya maisha ya mama yao iliyowafikisha pale, iliwafanya watoto wake wamlee mama yao kama mboni ya macho yao. Kuonesha wanamjali mama yao walimjengea jumba la kifahari sehemu za Mbezi na kumwekea wafanyazi pamoja na magari ya kutembelea.
Kila mmoja alikuwa na hamu ya kukaa na mama yake, lakini aliwakatalia kwa kusema kila mtu aishi maisha yake ili mwenye hamu afunge safari kumfuata.
Walikuwa watoto watatu wawili wa kiume na mmoja wa kike, wa kiume mmoja alikuwa mfanya biashara mkubwa wa madini ambaye pamoja na elimu yake aliyoipata Marekani aliamua kujikita kwenye biashara ya madini na kuweza kumiliki migodi miwili. Biashara ile ilimuingizia pesa sana na kumnfanya kuwa mtu maarufu wenye kutikisa jiji la Arusha.
Wa pili yeye ni katibu mkuu ofisi ya Rais ambaye na yeye alikuwa na maisha mazuri, alikuwa na majumba na magari ya kifahari na wa mwisho alikuwa msichana ambaye yeye alibahatika kupata kazi katika shirika moja la utangazaji nchini Canada.
Baada ya kukubaliana wote walipanga siku ya kukutana jiji Arusha tayari kwenda jiji Dar kwa mama yao bila kumjulisha kwa kumshtukiza. Kwa Upande wa Edna alikuwa na furaha isiyo na kifani kukutana na ndugu zake kwa mama yao na kuweza kuwaeleza kupata kwake mchumba.
Aliomba siku ile ifike upesi ili wamfanyie mama yao surprise ya ajabu kwa watoto wake kukutana kwa pamoja asubuhi baada kufungua mlango awakute mlangoni.
Nini kitaendelea?