Simulizi za Kasuku
Member
- May 20, 2017
- 7
- 0
RIWAYA; REHEMA WA NJIA PANDA
MTUNZI: Moringe John Mhagama
NITAFUTE; simulizizakasuku@yahoo.com au 0717308038 (Whatsap pekee) au
(0621081076 Meseji pekee)
KITABU CHA KWANZA
“Oyaa , madenti subirini abiria waingie!’’
‘’We dogo nitakufumua hembu sogeza kongoro zako pembeni" hizi zilikuwa ni miongoni mwa kauli zikaharishazo za makondakta kila asubuhi na mchana wanafunzi waelekeapo na watokapo shuleni.Ni wakati ambao makondakta wanakuwa na kiburi kwani wanakuwa na uhakika wa kuwapata abiria ambao wakati huo huwa wanaenda na kutoka kwenye mihangaiko ya kutafuta riziki.
Matusi na kusukumwa na hata kichaniwa sare za shule ni mambo yaliyoonekana kuzoeleka masikioni na machoni mwa watu japokuwa palionekana wachache waliokuwa wakikereka na hali hiyo huku kauli za kejeli kutoka kwa watu wengine zikiwakatisha tamaa watu hao walikuwa wakijaribu kuwatetea wanafunzi ambao serikali iliwapa haki ya kulipa nusu ya nauli ya kawaida.
Hayo yote yalikuwa yakitokea katika kituo kidogo cha mabasi cha Njia ya ng'ombe kilichokuwa nje kidogo ya mji wa Moshi.
Miongoni mwa wahanga wa kauli na manyanyaso hayo alikuwa Rehema Martin aliyekuwa akisoma darasa la tano katika shule ya msingi Kiwanja cha Ndege karibu kabisa na kituo hicho kidogo cha magari.Kama mwenye damu ya kunguni kwani alionekana kuchukiwa na karibu kila konda aliyekuwa pale stendi.Hiyo ilitokana na tukio lake la kudai kuwa alikuwa ameibiwa nauli ndani ya gari kila alipotakiwa kutoa nauli mara tano mfululizo tena kwenye magari tofauti kitu kilichomfanya kila kondakta na hata madereva kutomruhusu kupanda garini hata kama angewaonesha nauli kitendo chake cha kusafiri bure wiki nzima kilionekana kuwachukiza hata wanafunzi wenzake ambao wakifika stendi ilikuwa ni lazima kwao kumtambuilisha kwa kinda kuwa huyo ndo REHEMA WA NJIA PANDA kwani wiki alilokuwa akisafiri bure kama mchezo kila walipofika eneo lililoitwa Njia Panda alipotakiwa kutoa nauli alidai kuwa alikuwa ameibiwa hatimaye Rehema likawa jina lake na Njia Panda likawa jina la baba yake.
Baadaye ilikuwa ni vigumu kwake kupata gari la kupanda si asubuhi si mchana hata kama angekuwa na nauli na kupelekea kufikia uamuzi wa kuanza kutembea kwa miguu mara chache alibahatika kupata rifti mwenye magari mengine yasiyo ya abiria.
Kutoka kwao Rehema hadi shuleni alitumia saa moja na dakika kumi na tatu kutembea hivyo alikuwa akifika shuleni na nyumbani kwa kuchelewa tena akiwa hoi hali iliyopekea kuanza kushuka kitaaluma.
Alishawaeleza walimu wake na mama yake ambao waliguswa na jambo hilo.Kwa upande wa walimu hawakulichukulia umakini jambo hilo kwanza Rehema hakuwa miongoni mwa watoto watu waliokuwa wakifahamika pale shuleni ama kwa mali zao au umaarufu wao pia hakuwa miongoni mwa wanafunzi walikuwa na akili sana darasani hivyo mateso yalionekana ni haki yake kuipata.Kwa upande wa mama yake hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumwombea kwa Mungu wake ambaye kwake aliamini kama akimwadhibu kwa dhambi alizokuwa amezitenda ujanani mwake.
Alikumbuka historia yake iliyokuwa ikimuumiza siku zote huku akimwomba Mungu kumuadhibu kwa namna yoyote lakini si kwa kumfanya mwanaye apitie maisha kama yake akiwa hai ama akiwa mfu.Alijua kabisa hakumjua baba halisi wa mwanaye kutokana na matumizi ya ujana wake.
Siku zilikatika huku Rehema akizidi kuporomoka kitaaluma kutokana na mateso aliyoyapata kutembea masaa mawili na nusu kila siku ilikuwa ni zaidi ya mazoezi ya marathoni waliyokuwa wakiyafanya wanariadha kila ilipokaribia Februari ya kila mwaka.Marafiki wachache walianza kumpa sapoti hasa nyakati za jioni ili kumpa faraja binti huyo ambaye hadi umri huo hakumfahamu kwa jina wala sura baba yake ambaye mama yake alimwambia kuwa alifariki kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea siku mbili baada ya kuzaliwa kwake.
Alionekana ni mtu aliyekuwa na mateso makubwa sana kwa kila aliyemwangalia licha ya kulazimisha tabasamu usoni pake ,tabasamu ambalo lilikosa afya liliupoteza uzuri wa sura yake huku nywele zake ndefu nyeusi na rangi nyeupe iliyouficha weusi ulioonekana kwa mbali kwenye ngozi yake vilimfanya kila mtu amuweke kwenye kundi la watu waliochanganya damu ya kiafrika na kizungu.Lakini licha ya uchotara wake Rehema alionekana kuing'ang'ania sura ya kirembo aliyokuwa nayo mama yake Tumaini Martin ambaye kama si moshi wa kuni wakati wa kupika pombe ya kienyeji maarufu kwa jina la 'Dadii' ili kuikimu familia yake pangelitotea mashindano ya urembo basi angelikuwa miongoni mwa kumi bora ya akina mama warembo mjini Moshi.Miaka thelathini na sita aliyokuwa nayo aliiamini yeye pekee lakini kila aliyemwangalia alimwona kama binti wa miaka kumi na tisa ama ishirini na mbili.
Hakuwa na mtoto ama ndugu mwingine pale Moshi zaidi ya bintiye Rehema ambaye tangu akiwa mdogo alianza kukutana na mateso makali baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu uliomfanya avimbe kichwa upande mmoja.
******
Tumaini Martin wengi wakipenda kumwita Tuma alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto watano wa mzee Martin Kasuku na Lydia Kilongo waliokuwa wafanyabiashara mkoani Dodoma ,alikuwa miongoni mwa askari wastafu wa Jeshi la Wananchi aliyekuwa na cheo kikubwa jeshini.
Mzee huyu alikuwa na watoto wakiume wanne waliokuwa na sura za kutisha na mtoto mmoja wa kike ambaye alikuwa na sura nzuri illiyokuwa ikimvutia kila aliyeiona ama kusikia sifa zake.Wengi walimtuhumu Bi Lydia kuwa huenda alichepuka alivyoenda kuwasalimia wazazi wake huko Kyela kwani binti alikuwa mrembo haswa.Uzuri wake ulivumbuliwa tangu akiwa mdogo na kadri alivyokuwa akikua ndivyo vitu vingi vilivyokuwa vimejificha kwenye mwili wake vilijitokeza na kumfanya kila mzuri mjini pale alinganishwe kwanza na binti huyo ambaye aliiibua matumaini ya wazazi wake kupata mtoto wa kike na kupewa jina la Tumaini.
Akiwa darasa la saba Tumaini alikuwa ni miongoni mwa wanawake waliokuwa wakifuatiliwa kimapenzi na wanaume wengi mjini Dodoma.Wazee,vijana,matajiri , masikini waliokuwa na kazi na wale wenzangu na mimi kula kulala kwa mama walijaribu bahati yao suala alilolifikisha kwa baba yake kupitia mama yake ambaye hakuacha kuwaadhibu vijana aliokuwa akiwakuta na binti yake,adhabu za kikatili na mateso makubwa.
Siku moja jioni kama ilivyokuwa kawaida yake wakiwa jikoni na mama yake Tuma alionekana mtu mwenye wasiwasi sana hali iliyomfanya mama yake ahisi kuwa binti yake alikuwa na jambo lililomfanya awe katika hali hiyo.
"Mbona hivyo Tuma , kuna tatizo?" Aliuliza Lydia.
" Hakuna tatizo mama " alijibu Tuma huku akizuia machozi kushuka.
"Niambie mwanangu mie ni mama yako niambie jambo likusumbualo nitakusaidie"Alibembeleza mama yake.
" Hutoniamini mama"
"Niambie mwanangu nitakuamini ,mangapi umeniambia nikakuamini?"
"Yote yalikuwa madogo hili hamtaliamini mama"
" Au ndo hao wanaume wa kila siku ? We u mrembo lazima wakusumbue cha msingi kuyazingatia tuliyokueleza umri na wakati haujafika mwanangu" mama mtu alizidi kutoa nasaha.
" Ndiyo wanaume mama"
"Wanakutisha Leo?"
"Hata hawanitishi , ila huyu wa leo amenitisha"
"Namfahamu?"
"Ndiyo"
"Nani"
"Baba Zita"
"Acha kuchuma dhambi binti yangu , Baba Zita mchungaji? We mtoto unataka kugombanisha watu si bure"
"Ndo maaana nilise,,,,,,,"
"Kimya shetani wewe umetufanya watoto" Aliongea Bi Lydia kwa hasira akimalizia na kofi lililokwepwa kiustadi na kutua juu ya sufuria iliyotoa ukelee baada ya kufika sakafuni na kumshtua Mzee Martin aliyekuwa sebuleni na wanawe wa wawili mwisho na kuelekea jikoni.
Anord Mwakibale au Baba Zita kama wengine walivyozoea kumwita alikuwa Mchungaji wa kanisa la "These days" lililokuwa limeingia nchini miaka ya tisini huku likisifika kwa kuwa miongoni mwa makanisa machache yaliyokuwa na uwezo wa kuwaponya wagonjwa, kuwafanya vipofu waone,viziwi wakasikia na hata viwete wakatembea.Mchungaji Mwakibale alifahamika si tuu Dodoma pekee bali hata nje ya Afrika kutokana na kazi yake kubwa ya kuokoa maelfu ya wanadamu waliokuwa na shida mbalimbali kwa miujiza na wokovu.
Urafiki wake na mzee Martin ulianza miaka mingi iliyopita kipindi wapo shule ya sekondari ya wavulana Tabora.Walitengana kwenye mafunzo ya Jeshi La kujenga Taifa ambapo Martin alipelekwa Oljoro na Anord akipelekwa Kanembwa.Walikuja tena kukutana Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambako waliurejesha urafiki wao hadi walipomaliza na Martin aliporejea jeshini kwa Mara ya pili safari hii akiingia Jeshi la wananchi na Anord akipangiwa kazi mkoani Tabora kama Afisa manunuzi wa Mkoa
Miaka mitano baada ya kuanza kazi Anord alipatwa na ugonjwa wa ajabu.
Ilikuwa Siku ya jumamosi kama kawaida yake alikuwa na mazoea ya kufanya ziara za kushitukiza kwenye idara zilizokuwa chini yake wilayani.Akiwa ndani ya gari la serikali ambalo lilitumika tangu zama za ukoloni Anord alimwona mtu ambaye kama aliwahi kumwona mahali.Alimwamuru dereva wake asimamishe gari , kisha alishuka na kuelekea upande aliomwona yule mwanamke .Baada ya hatua kama tatu macho yake yakakutana na mwanamke aliyekuwa akimfuata akiwa amekaa chini ya mti wa maembe.
Alijikuta akishindwa kabisa kusogea ,akajaribu kunyanyua mdomo wake aseme kitu lakini mdomo wake nao ukawa mzito kutamka kitu .Wakabaki wakitazamana tuu bila kuongea chochote.
Macho yao yalijaribu kuzungumza lakini nayo yalipoteza uwezo huo, kila alipojaribu kumwongelesha kwa macho alishindwa.
Baada ya kuduwaa kwa takribani dakika mbili ,hatimaye macho yao yakazungumza.
" Njoo, mwenzako nateseka hapa"
" Mie siwezi mrembo wangu ,njoo wewe"
" Mie siwezi nipo kifungoni"
"Kifungoni! Kakufunga nani ? "
Waliendelea kujibishana kwa hisia huku kila mmoja akionekana kumhurumia mwenzake.
" Bosi si unaliona wingu twende barabara itachafuka" Sauti ya dereva wake ilimshtua Anord ambaye ni kama alikuwa amerudishwa kwenye ulimwengu mwingine na kumfanya afikiche macho kuhakikisha kama alikuwa akiota ama la.Hakumwona mtu mmoja bali watu wengi wakiendelea na shughuli zao za kila siku huku wakionekana kuchukua tahadhari ya mvua iliyoonekana kutarajiwa kunyesha.
" Hivi nimetumia muda mrefu sana?" Aliuliza baada ya kuingia garini.
" Umemaliza dakika arobaini ukishangaa watu"
"Acha uongo wako wewe hata dakika tano hazijafika"
" Tano?, we kweli umechanganyikiwa" aliongea akiondoa gari.
" Nimechanganyikiwa , mpumbavu mkubwa wewe kwa hiyo bosi wako amechanganyikiwa? Hembu nipishe hapa nimekuajiri upate kulisha familia yako nawe unajitia kidume kuniona nimechanganyikiwa, toka mpumbavu wewe" aliongea Anord kwa hasira huku uso wake ukibadilika na kuwa mwekundu.
Tangu aanze kufanya kazi kama dereva wa Afisa manunuzi wa mkoa ule miaka minne iliyopita hakuwahi kumwona bosi wake akiwa amefura kiasi kile huku akisifika kwa kuwa na utani mwingi kwa wafanyakazi waliokuwa chini yake.Alimtania na kutaniwa na kila mtu bila kujali nafasi yake au jinsi , mabinti walitania na kumaanisha kuhitaji ndoa naye lakini aliishia kuwaambia ataoa Mbeya tena mke wa kutafutiwa na bibi yake .
Lakini kwa wakati ule alionekana kutokuwa Anord aliyezoeleka, dereva alitoka garini kuzuia jambo lolote baya kumfika kutoka kwa bosi yule kinyonga aliyegeuka mbogo ghafla.
Baada ya dereva wake kushuka aliusogelea usukani akiwa na hasira na kutaka kuendesha gari lakini alijikuta akilegea na kuangukia usukani jambo lilimfanya dereva wake aliyekuwa akimwangalia arudi garini na kumwangalia bosi wake ambaye licha ya kumtimua garini muda mfupi uliopita alikuwa akimwona kama ndugu yake wa damu tangu siku ya kwanza ambapo alimchukua kwa shangazi yake miaka mitano iliyopita na kupeleka chuo cha ufundi Ifunda alikojifunza Umakanika na udereva kisha kumwajiri kama dereva wake.
Aliingia garini na kujaribu kumwinua ,Anord alijaribu kumzuia huku akijaribu kuzungumza kitu lakini alionekana kuishiwa nguvu kabisa hata zile ndita zilizokuwa usoni lake zilikosa nguvu na kuonesha sura iliyojaa unyonge.Alifanikiwa kumweka kwenye siti ya pembeni na kumfunga mkanda kabla ya kuwasha gari kwa kasi ya ajabu kuelekea hospitali.
Akiwa amefanikiwa kuiweka gari lile la kizamani barabarani kisawasawa hakuwaza kitu kingine zaidi ya kutaka kujaribu kuokoa maisha ya bosi wake.Akiwa katika kasi ya ajabu alishtuka kuona roli la kampuni ya tumbaku ikiwa ipo katikati ya Barabara huku watu kadhaa wakihangaika kufungua tairi la mbele , hakufanikiwa kufikiria kitu zaidi na kujikuta akijigonga kwenye kitu kizito na giza totoro lilikamata macho yake.
Mafundi waliokuwa wakitengeneza Lori walipoona gari ikija kasi mahali walipokuwa wamesimama waliamua kuyanusuru maisha yao kwa kukimbilia pembeni ambako waliamini wangekuwa salama.
Kilichofuta wengi walishindwa kukisimulia japokuwa walikuwa wamekishuhudia kwa macho yao mawili mazima bila hata kasoro yoyote.Kilichoshuhudiwa ni mwili mmoja kutolewa kupitia kioo cha mbele cha gari kabla ya kutua juu ya lori na kutua chini ambapo mapande ya nyama zenye damu yalionekana yakiwa yamesambazwa barabarani.
Gari liligonga lile lori na kutupwa pembeni na kama ilivyokuwa kawaida watu walilisogelea na kuanza kuchungulia kilichokuwemo ndani mwake.
Hakuna aliyeamini alichokishuhudia ndani ya lile gari dogo na kumfanya kila aliyeona asogee pembeni na kumtaka mwenzake aone alichokiona na kuhakikisha kama naye ataamini.
*****
"Mambo Anord"Sauti nyororo ilipenya kwenye ngoma za masikio ya Anord na kumfanya achungulie nje kupitia dirishani ili amwone mtu aliyemsalimia kwa nje.
" He! hata kama ni haraka ndo tunasalimiana nje nje tuu?" Anord aliuliza baada ya kumwona mtu aliyekuwa akimsalimia, japokuwa hakuwa akimfahamu alijikuta akitamani kuwa karibu na yule mtu.
"Nina haraka kidogo ndugu yangu naomba niende nipeleke mzigo huu kwa shangazi halafu nitakuja tusalimiane vizuri" Aliongea yule mrembo huku akionesha kikapu kilichokuwa na makopo.
" Jamani si unakaa kidogo tufahamiane halafu nakupeleka na gari yangu?" Anord alibembeleza.
" Mhhh kwa sababu umeniomba sana basi sikai sana shangazi yangu mkali sana" Alideka yule mrembo.
" Hapo umenena, karibu mgeni" Aliongea Anord akimpokea kikapu.
" Mhhh , mbona kikapu kizito sana umebeba majini nini?Alitania Anord akimpigapiga yule mrembo begani.
Japokuwa alihisiwa kuwa mwaminifu na mwenye msimamao sana kuhusiana na masuala ya mapenzi ofisini kwake Anord alijikuta amepoteza msimamo wake kwa yule mrembo.Ingawa hakumkumbuka kwa jina yule mrembo lakini alikuwa na uhakika kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa akionana naye kila siku kama siyo Urambo Bar alikokuwa akipoteza muda wake kwa kupata mishikaki na bia mbili tatu basi kazini kwao.
" Karibu ndani mgeni nikuandalie chakula gani? " Aliuliza Anord
" Umesema tusalimiane vizuri hujasema kula , kama chakula nitalamba asali basi nalidhika"
" Mbona nimeishiwa asali "
" Usijali mie ninayo hapa " aliongea yule mrembo akitoa moja ya makopo yaliyokuwa ndani ya kile kikapu.
" Mhh kwa hiyo hii yote asali?" Aliuliza Anord huku mate ya tamaa ya asali yakimshuka.
"Ndiyo kanituma baba nimpeleke shangazi " Alijibu yule mrembo na kumfanya Anord amkumbuke yule binti , alikuwa ni binti wa muuza asali maarufu kwenye soko la mjini.
" Si za kuuza hizi niuzie na mimi Sikujua" Alimkumbuka kwa jina.
" We unazitaka za nini wakati huna hata mke hapa?"Aliongea Sikujua akicheka.
" Halafu na jina langu nani kakutajia?"
" Jamani nisikujue mtoto wa mzee Masoud wa Bukene?"
" Haya tuachane na hayo we asali unaitumia na nani?"
"Peke yangu"
" Peke yako, unaitumiaje?"
" Nailamba"
" Mhh ngoja nikufundishe jinsi ya kuitumia"
"Kwa hiyo unataka kuipika?" Anord aliuliza baada ya kuingia jikoni.
''Nataka nikaoge kwanza ndo nije kukufundisha''
''Kuoga, hayo maji?"
''Ndiyo kuna tatizo?"
''Ndiyo tena kubwa tuu''
''Kuna tatizo mie kuoga maji ya moto?"Aliuliza Sikujua akimwangalia Anord kwa jicho la kichokozi ambalo bila hata kuelezwa alikuwa ameshaanza kupagawa na mikao ya kihasara hasara ya yule binti mara afungue kanga yake mara aifunge mara ajifanye kupandisha na kuliweka vema kufuri lake akishika nguo zake na kuibana kwa vidole vyake.Japokuwa Sikujua alikuwa binti mrembo hakuwahi hata siku moja kumshawishi Anord kimapenzi kwani akili yake siku zote ilikuwa kwa mchumba wake aliyekuwa huko kwao.Lakini siku ile alimwona Sikujua kama binti mpya aliyekuwa na kitu cha ziada tofauti na alivyodhania kabla.
''Mbona unaniangalia sana, hembu niletee chupa ya chai hapo''Sikujua aliongea kwa ukali wa kuigiza huku akimwangalia kwa macho ya kichokozi Anord ambaye akili yake haikuwaza kingine zaidi ya kutaka kumla samaki aliyekuwa mbele yake alianza kujilaumu kuchelewa kufikiria uzuri wa yule binti.Mawazo kwa mchumba wake ndiyo yaliyokuwa sababu ya kutoanza kuangalia uzuri wa wananawake wengine.
" Twende kuoga basi''Sikujua aliongea kwa sauti ambayo bila mashaka nyoka huweza kuliacha pango lake kutaka kujua nani aleyeitoa sauti.
''Kuoga nenda maji ya moto bafuni yapo nilikushangaa unajifanya kutenga maji ya kuoga kumbe unataka kahawa, hii nyumba ya kizungu hii kila huduma ipo ''Alijisifia Anord lakini kila alipomtazama Sikujua alijikuta akitamani kuwa naye mahali fulani akiutafiti uzuri wa msichana huyo.
"Twende wote we vipi?"
''Wote?"
''Ndiyo twende''Sikujua aliongea na bila kutarajia Anord alijikuta akivutwa kama mbuzi mtiifu hadi bafuni ambako hapakuwa mbali sana na walipokuwa wamesima.
Sikujua alifungulia maji yaliyomlowanisha Anord na kuyafunga kisha akutoka nje ambako alihakikisha kuwa mlango ulikuwa umefungwa na kurejea bafuni alikokuwa amemfungia Anord akiwa na kanga moja na sabuni fulani za kuogea zilizokuwa na marashi makali sana.
Anord alijikuta akilegeza msimamo wake kadri muda ulivyokuwa ukienda kwani hata pale Sikujua alipoanza kufungua vifungo vya shati lake lililokuwa limelowa upande mmoja na kisha suruali na kufungulia bomba mvua ambalo lilitoa maji ya vuguvugu yaliyotoka kwenye tanki lililokuwa juu ya nyumba ile kwa ajili ya kupasha maji , mfumo uliowekwa tangu zama za ukoloni na wafanyakazi wazawa wakawa wakiishi humo baada ya Tanganyika kupata Uhuru.
''Anord alijikuta akitoa sauti za kugugumia raha ya kusuguliwa mwili wake kuanzia kichwani hadi kwenye kucha zake ambazo zilioshwa na kung'aa kweli kweli.Harufu ya ile sabuni iliifanya bafuni paonekane kama mahali penye harufu nzuri kuliko pengine popote pale ndani ya ile nyumba.
Baada ka kumwogesha Anord Sikujua alimtaka naye amwogeshe huku akitoa kanga yake iliyokuwa imelowa na kugandiana mwilini.
Anord bila kupinga alianza kumwogesha huku Sikujua akiwa ameukomalia mwili wa Anord ambaye alijikuta yupo kwenye sayari nyingine huku zoezi la kumwogesha likikomea njiani bila kutarajia.
Anord alijikuta akivunja dafu mara mbili huku hamu ya kutaka kulila tunda ikiongezeka kadiri Sikujua alivyokuwa akizidisha manjonjo yake lakini alizuiwa na Skujua ambaye alitambua hilo baada ya Anord kumsogeza karibu tayari kulishambulia lango la timu pinzani.
''Wee! unataka kufanya nini? '' Sikujua alichoropoka mikononi mwa Anord na kukimbilia kanga yake kisha kujifunga na kukimbilia chumbani kwa Anord.
Kuna wakati Anord alikuwa akijiuliza imekuwaje yule dada aliizoea ile nyumba japokuwa hakuwahi kuingia pale nyumbani tangu akae pale na kabla yake nyumba ile ilikuwa ikikaliwa na DC wa kikoloni aliyekuwa na familia yake lakini nguvu ya kuhoji zaidi ilizidiwa na mambo aliyokuwa akifanyiwa kila dakika ilivyopita kwani baada ya kufika chumbani Sikujua alimfuta maji Anord kwa taulo safi ambalo lilitolewa chini ya kile kikapu kilichokuwa na makopo ya asali.
Baadaye alitoa marashi aliyoyapulizia mle chumbani na kumfanya kuwa mahala fulani penye harufu ya kuvutia sana.Hapo ndipo Anord alipojua kuwa kikapu kile hakikuwa si tuu na asali bali vitu vingi ambavyo vilikuwa na matumizi maalum.
Mbali na manukato pia palikuwa na kanga nyepesi nyeupe zilozokuwa zimekunjwa vizuri na kuweka chini ya zile chupa.Sikujua alitoa kanga mbili na moja akajifunga mwenyewe akiacha nusu ya kifua chake kichanga nje na nusu nyingine ikiwa ndani ya kanga.
Kanga nyingine aliikunja nusu na kumfunga Anord kiunoni ambaye muda wote alionekana kupoteza akili yake ya maamuzi kwani alifanya kila alichoelekezwa.
''Sasa ngoja nikufundishe jinsi ya kutumia asali si kujaza tumbo tuu'' alijigamba Sikujua akimpaka asali miguuuni sehemu za nyuma ya magoti na unyayoni kabla ya kuanza kuilamba asali hiyo taratibu na kumfanya Anord atoe sauti kana kwamba alikuwa akipoteza pumzi.
Sikujua aliendelea na zoezi hilo mgongoni kabla ya kumalizia kifuani ambako kulimfanya Anord apate raha za ajabu sana na kuvunja madafu kwa fujo.
Sikujua alimwamuru Anord atoe ile kanga ili amalizie shughuli ya kulila tunda naye huku akiwa amepandwa na mori alishuka kitandani ili atoe hiyo kanga ambayo ilikuwa imeloa madafu sehemu ya mbele.Wakati akishuka kwa bahati mbaya alikanyaga moja ya makopo yaliyokuwa na manukato na kuteleza kabla ya kupigiza kichwa sakafuni na kumfanya atoe ukele wa maumivu.
_____________________
Watu wote waliokuwa wamelizunguka lile gari huku wakishangaa kuona mtu ambaye alikuwa kwenye ajali mbaya kama ile kusinzia ndani ya gari na kuota ndoto ambayo bila shaka na ilikuwa ya mahaba kutokana na jinsi alivyokuwa akifanya kabla ya kujibamiza kwenye Chuma kilichokuwa kimechomoza na kumsababishia jeraha kubwa lililokuwa likitoa damu nyingi sana zikirukia hata nje.Walimtoa mtu yule na kumpa huduma ya kwanza kuzuia damu kutoka kisha kumpakia kwenye gari lingine lililokuwa limesima baada ya njia kuzibwa na magari yaliyokuwa yamepata ajali.
Anord licha ya kuwa na jeraha kubwa lililokuwa likimtisha kila mmoja aliyeliona hakusikia maumivu yoyote huku akikumbuka ndoto aliyokuwa akiiota.Alimkumbuka Sikujua lakini aligundua Sikujua yule alikuwa na nywele ndefu na mweusi zaidi ya Sikujua aliyekuwa akimfahamu.Lakini zaidi alikumbuka kuwa Sikujua alikuwa ameolewa huko Dodoma miaka miwili ikiyopita na ni yeye ndiye aliyempeleka stesheni ili akapande treni.
''Hapana !'' Anord alijikuta akiongea kwa sauti kubwa na kuwashtua wauguzi waliokuwa wamembeba kwenye machela kumwingiza wodini.
Baadaye aliamua kulala tena baada ya kugundua kuwa kushtuka kwake kuliifanya damu iendelee kutoka kichwani pake.Ndani ya wodi madaktari waliendelea kuhangaika kuokoa maisha yake lakini akili ya Anord ilikuwa ikimfikiria mrembo ambaye alikuwa amempa raha usingizini.Hakutaka kabisa kufanya kitu kingine zaidi ya kutaka kupata utamu ambao Sikujua wa usingizini alikuwa akiendelea kumpatia.
Masaa kadhaa ya kusafisha na kushona jeraha lililokuwa kichwani kwa Anord alijaribu kurejesha kumbukumbu kichwani mwake na kurejesha akili hiyo kwenye ulimwengu wa kawaida , alikumbuka tangu alipomwona msichana mrembo ambaye walijibishana kwa macho ,ugomvi na dereva wake na kisha kumfukuza.Akili yake ilimkumbusha pia chanzo cha ugomvi wao, ambacho alijua kabisa kuwa hakuwa sababu ya kumfukuza ndugu yake ambaye alikuwa ameenda kumchukua kijijini kwao.Hakujua kabisa kuwa ndugu yake huyo ambaye ndiye dereva wake aliyekuwa amemfukuza masaa machache yaliyopita hakuwa tena hapa duniani bali alikuwa ameshafariki.
Akili yake haikumwambia kuwa aliyekuwa akiendesha gari alikuwa si yeye bali dereva wake aliyekuwa amefariki.Alifikiria mahali ambako ndugu yake huyo angekuwa, alijua kabisa alikuwa amemsababishia mateso bila sababu yoyote ikizingatiwa kuwa alikuwa ugenini ambako kwa haraka haraka suluhisho lingekuwa ni kushinda kwenye mashamba ya tumbaku kufanya kazi jambo ambalo hakutaka kabisa litokee.
Majira ya saba mchana gari la serikali lilifika hispitalini na kumchuka kwani alikuwa si mtu wa kulazwa huku mwenyewe akiwa hana maumivu yoyote zaidi ya kutishwa na wingi wa damu iliyokuwa imemwagika.
''Pole kwa msiba ndugu yangu'' Aliongea dereva aliyekuwa akiendesha gari walilokuwa wamepanda baada ya kumfikisha nyumbani kwake.
''Msiba nani amekufa?"
“Dereva wako mlipopata ajari alipoteza maisha pale pale''
Anord alijikuta akishindwa kujizuia taratibu machozi yalimshuka na akajikuta akikaa chini pale pale mlangoni.Hapo ndipo kumbukumbu kuwa alikosa nguvu mara tuu alipotaka kuendesha gari.Aligundua kuwa dereva wake ndiye aliyekuwa anaendesha gari pia taswira ya tukio la kuchomwa na chuma ndani ya gari ilijirudia kichwani kwake alijiona akiwa kwenye kiti cha pembeni huku nyama na damu zikiwa zimesambaa ndani na nje ya gari.Alijilaumu sana kwa kitendo chake cha kugombana na dereva wake kwani alihisi kuwa kumgombeza kulimfanya aendeshe gari huku akiwa na mawazo hatimaye alikosa umakini kabla ya kupata ajali hiyo.
Hayo yote yalipita akilini mwake haraka haraka sana akiwa palepale chini mlangoni.
Alisaidiwa kuingia ndani na yule dereva aliyemleta kabla ya kuja wafanyakazi wenzake waliokuja kuandaa mazingira ya msiba kwani marehemu alikuwa akiishi naye kabla mauti kumfika na yeye pekee ndiye aliyekuwa ndugu pale Tabora mjini ndugu wengine walikuwa Sumbawanga ,Kigoma na Dodoma wengi walikuwa Mbeya na kwa jinsi mwili wake ulivyokuwa umeharibiwa isingewezekana kuusafirisha hadi Mbeya.
Siku iliyofuata ndugu na jamaa kutoka sehemu mbalimbali walikuja kujumuika na wafanyakazi wengine kuuweka mwili ule kwenye nyumba yake ya milele.
Hakuna aliyejua kilichokuwa nyuma ya ile ajali wengi wakiamini ilikuwa ni ajali ya kawaida iliyokuwa imetokana na mwendokasi.
Siku, wiki na hatimaye miezi ilipita lakini kidonda kilichotokana na jeraha la ajali kiliendelea kuongezeka na kutoa harufu kali iliyopekelea watu kuogopa kuwa karibu ya Anord.Japokuwa mwenyewe alidai kuwa alikuwa hapati maumivu yoyote lakini wenzake walidai kichwa chake kilikuwa hatarini sana kutokana na hali yake.
Wakati hayo yakiendelea ile ndoto tamu ilikuwa ikijirudia kila siku lakini hakuna siku aliyokuwa amefanikiwa kufikia hatua ya kulila tunda.Ndoto haikuchagua sehemu ya kutokea nyumbani ndani ya gari ofisini na popote pale ilipojisikia kutokea.
Kila mara Anord alijikuta akiaibika kuchafua nguo zake kwa madafu lakini licha ya aibu ile aliifurahia ile ndoto na kutamani imtokee tena.
Sauti za kugugumia utamu ndizo zilizokuwa sababu ya wafanyakazi waliokuwa ama juu yake au chini yake kupata cha kuongea.
" Hivi unajua Anord amekuwa kichaa?" Katibu wa Anord alikuwa akimweleza mfanyakazi mwenzake.
''Yule atakuwa na jini asipotembea atapata shida au kufa kifo kibaya....''Alimjibu mwenzake ambaye kabla ya kumalizia jibu lake alimwona Anord ambaye alionekana amesikia kila kitu.
''Umesema nini?"Anord aliuliza akiwa amefura kwa hasira.
''Sijasema kitu mbona umefura hivi?"Alijibiwa Anord jibu ambalo halikumwingia kabisa akilini.
" Nitapiga mtu hapa si mmesema habari za wehu na majini yenu?"
"Utakuwa umesikia vibaya hatujasema habari hizo ndugu''
"Halafu we mfupi ka Kisebengo unajifanya unajua kiherehere sana'' Anord alionekana kutokuwa na mchezo hata kidogo akimsogelea mfanyakazi mwenzake aliyekuwa akipendelea kumwita Kisebengo kutoka na kimo chake kifupi.
''Jamani mbona unapenda sana kunionea jamani ''Kisebengo alimlalamikia Anord ambaye walitofautiana tuu vitengo ye akiwa mhasibu wa mkoa.
Japokuwa wote walionekana ni vijana wa rika moja Anord daima alionekana mwenye mamlaka juu ya wenzake kwanza kutokana na kuwa na muda mrefu kwenye ile ofisi huku yeye akifanya kazi zote kama mhasibu na afisa manunuzi wa mkoa wa Tabora.
''Samahani jamani lakini jiangalie Anord haya mambo si ya kawaida''Yule mfanyakazi mwingine alishauri akimtetea Kisebengo na kumpa ukweli Anord ambaye kila mtu pale ofisini alijua kuwa alikuwa kwenye matatizo makubwa.
''Na we unanitafuta kila siku ''
''Nani mim?''
''Ndiyo kila siku kazi kuwateta wenzako tuu na kuingilia hata yasokuhusu''
''Eti jamani mie kosa langu nini ?"
''Hulijui kosa lako ehhe ?"
''Ndiyo, au nilivyokushauri?''
''Umenishauri zaidi ya kuongea mambo ya kuongea wanawake?"Anord alionekana kupandwa na jazba kabisa yaani hata mtu angemwita jina lake kwa wakati ule lazima angemgeuzia kibao na kumpa kibao.
''He! Na wewe ukiwa na shida tusikuambie? Ngoja tuu tukuambie ukweli wewe una matatizo makubwa kama ndugu na majirani zako wanaogopa kukuambia ukweli wakisubiri mahoka wa babu zako wakuambie wanakupoteza nakuambia kwa mema kama utanichukia sawa ila hapa umeshapata hasara''Kisebengo alijitutumua na kumwambia Anord ukweli ambao hakupenda kabisa kuusikia kwani alihisi kuonewa.
Kila neno lililokuwa likitafsiriwa na akili yake lilionekana kumchoma lakini si kwa kumfanya awe mpole kwa kuwa ni la kweli bali lilikuwa likimpandisha hasira zake alijitahidi kujizuia lakini hatimaye alijikuta akirusha konde lililokwepwa kiustadi na kisebengo ambaye aliliona tangu likiandaliwa.
Anord hakukubali akatupa jiingine ambalo liliyompata Kisebengo kisawasawa kwani alionekana kuzubaa baada ya kukwepa konde la kwanza.
Kisebengo alipelekwa mlangoni alikojipigiza na kupata maumivu ambayo yalimpandisha hasira.
Aliinuka na kumparamia Anord ambaye hakujiandaa kwa kumchapa ngumi ya uso iliyompata sawasawa na kumpigiza ukutani na kutua chini kama mzigo jambo lililowafanya kisebengo na mwenzake wapate hofu na kumwinua Anord ambaye alikuwa ameshapoteza fahamu.
Pona yao walikuwa watu watatu pekee kwani wafanyakazi wengine hawakuwepo mahali pale ofisini kwa kuwa ilikuwa asubuhi sana tena Siku ya jumamosi ambayo haikuwa siku ya kazi kwa ofisi nyingi pale mkoani na hata ofisi zilizokuwa zikitoa huduma zilichelewa kufunguliwa.
Akiwa katika kupoteza fahamu Sikujua alimtokea kama ndoto zake za siku zote lakini siku ile alionekana mwenye furaha sana.
''Mbona unaonekana umefurahi sana mpenzi?" Anord aliuliza akimwangalia Sikujua kwa macho ya uchu kwani alionekana amependeza kuliko Siku nyingine alizokuwa akimwota.
''Ninakucheka wewe''
''Mimi! Nachekesha?"
" Ndiyo unahangaika kufuta damu na kitambaaa ukihisi jasho"
''Kweli nilijua jasho kweli''Anord aligundua hilo baada ya kujiangalia mkono wake uliokuwa unelowa damu, ajabu hakusikia maumivu yoyoyote.
''Hivi nimeumia sana?"
'Ndiyo lile kovu lako la ajali limefumuka tena, lakini tuachane na hayo leo ni Siku ya furaha sana maana ni siku ambayo nitakuwa na wewe wakati wote maishani mwangu''
''Kweli ?"Anord aliuliza kwa wahka.
''Kweli mpenzi wangu utaishi nami milele na utaijua sababu ya haya yote.
Anord alifurahi sana kwani alijua raha alizokuwa akiziota muda mfupi na kukatishiwa utamu njiani akuwa akizipata kila wakati.
''Au ni ule wakati ambao ulisema nitapata nafasi ya kufaidi tunda lako?".Anord aliuliza akikumbuka kuwa aliambiwa muda ukifika hawataishia njiani wala kufaidi raha usingizini bali wataishi duniani kama watu wengine wakifurahia raha lakini kwa sharti moja la Sikujua kutoonekana nje na angewambia ukweli juu ya maisha yake.
''Bado muda kufika ila ni hatua kuelekea huko''.
Licha ya kuambiwa kuwa muda ulikuwa haujafika Anord aliona ni hatua nzuri kwani hakuna kitu alichokifurahia kama kuja kupata Uhuru wa kula tunda la sikujua wa ndotoni.Alimsogelea Sikujua na kumkumbatia na kwa kuwa alikuwa amemfundishwa mambo mengi Anord alijikuta amebobea katika kumpeleka Sikujua panapohusika bila hata kutumia fimbo yake ya kurekebishia tabia.
Alimmvua gauni lake refu lililokuwa nguo pekee iliyokuwa imeufunika mwili wake na kumbeba na kumshusha kitandani kisha kumshika kiuno chake kuelekea bafuni jambo ambalo lilimshtua sana Sikujua jambo ambalo Anord hakuligundua kwani akili yake ilikuwa katika kwenda kuanzisha raha.
''Nisubiri nakuja mpenzi''Anord aliongea akirudi chumbani kupitia sebuleni jambo ambalo bila kujua lilimtisha Sikujua na ambaye kwa hasira aliinuka na kumfuata Anord na kumpiga mgongoni na kumshitua Anord aliyeshtukia yupo hospitalini huku mbele yake kukiwa na Kisebengo na yule mfanyakazi mwenzake waliyekuwa wote kwenye ugomvi.
____________